Naibu Waziri, Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete
amesisitiza kuwa maslahi ya watumishi ni kipaumbele katika awamu hii ya Sita
ili kuongeza motisha na kuchochea zaidi utendaji kazi na utoaji wa huduma bora
kwa umma.
“Kila mara tunaona Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akitangaza kutoa haki na stahiki
mbalimbali kwa watumishi wa umma, hivyo, kila mmoja wetu kwa nafasi yake
anatakiwa pia kuwajibika ipasavyo ili kuleta ufanisi zaidi” ameongeza Mhe.
Ridhiwani.
Mhe. Ridhiwani amesema na kusisitiza hayo tarehe 26
Agosti, 2023 alipokuwa akizungumza na viongozi wa Sekretarieti ya Mkoa wa
Singida katika ofisi hizo. Aidha,
amewakumbusha watumishi hao kutoka ofisini na kwenda kuwahudumia wananchi na
kutatua changamoto zilizo ndani ya uwezo wao.
Katika hatua nyingine Mhe. Ridhiwani ametembelea na
kukagua ujenzi wa majengo ya Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Singida
awamu ya pili inayohusu majengo ya madarasa na vyoo vya nje na kuelekeza
viongozi kuhakikisha miundombinu ya watu wenye ulemavu inazingatiwa katika ujenzi huo.
“Chuo cha Utumishi wa Umma ni muhimu sana kwa kuwa
kinaandaa watumishi wa umma bora na ambao ni msingi wa maendeleo ya nchi katika
nyanja zote” ameongeza Mhe. Ridhiwani.
Vilevile, akiwa katika ziara ya kutembelea wanufaika
wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii- TASAF katika Kijiji cha Ughaugha Kata ya
Unyamikumbi, Manispaa ya Singida amesema Serikali imetoa zaidi ya bilioni 51
kwa ajili ya kunusuru kaya maskini nchini ili ziweze kuboresha maisha yao
mathalani kwa kupata chakula milo 3 kwa siku, kusomesha watoto na kupata huduma
za matibabu kwenye vituo vya afya na zahanati.
Naye, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Bw.
Stanislaus Choaji amesema wamepokea maelekezo na
watahakikisha wanatazama kwa jicho pevu maeneo ya pembezoni katika Mkoa wa
Singida kwa kutoa na kupanga watumishi ili kuboresha utoaji wa huduma kwa umma.
Aidha, Bw. Choaji ameongeza kuwa wananchi wa Mkoa wa
Singida wananufaika na uwepo wa TASAF kwa kuwa kaya maskini ambazo ni wanufaika
wamepata fedha na wanafanya shughuli za kiuchumi ikiwemo kufuga
Mbuzi, Kuku na Kondoo kwa ajili ya kujikwamua katika wimbi la umaskini, hivyo
salamu za shukurani zimfikie Mhe. Dkt.
Samia Suluhu Hassan kwa ukombozi huo.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu,
Chuo cha Utumishi wa Umma Dkt. Ernest Mabonesho amesema ujenzi umefikia
asilimia 21 na kazi inayoendelea ni ujenzi wa kuta ambapo hadi sasa mradi huo
umetoa ajira za vibarua kwa wananchi 96 wanaozunguka eneo la mradi ikiwa
wanaume ni 62 na wanawake ni 34.
Mhe. Ridhiwani amehitimisha ziara yake ya siku mbili
katika Mkoa wa Singida kwa tarehe 25-26 Agosti, 2023 ambapo alianzia
Halmashauri ya Wilaya ya Itigi na kumalizia katika Manispaa ya Singida. Ziara
hiyo ililenga kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi na kukagua utekelezaji wa
miradi ya TASAF katika Mkoa huo.
Naibu Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani
Kikwete akizungumza na viongozi wa
Sekretarieti ya Mkoa wa Singida ambapo amesema
kuwa maslahi ya watumishi ni kipaumbele katika awamu hii ya Sita ili
kuongeza motisha na kuchochea zaidi utendaji kazi na utoaji wa huduma bora kwa
umma.
Sehemu ya wanufaika wa
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii- TASAF katika Kijiji cha Ughaugha Kata ya Unyamikumbi,
Manispaa ya Singida wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete ambapo amewaeleza kuwa Serikali
imetoa zaidi ya bilioni 51 kwa ajili ya kunusuru kaya hizo
.
Baadhi ya
Wakurugenzi wa Taasisi mbalimbali za mkoa wa Singida pamoja na Wajumbe wa Kamati
ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo wakimsiliza
Naibu Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani
Kikwete wakati alipotembelea na kukagua ujenzi
wa majengo ya Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Singida awamu ya pili
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akioneshwa ramani ya majengo ya Chuo cha Utumishi wa
Umma, Kampasi ya Singida awamu ya pili mara baada ya kufika katika eneo hilo kwa ajili kukagua ujenzi wa chuo hicho
unavyoendelea
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza mara baada ya
kutembelea na kukagua ujenzi wa majengo ya Chuo cha Utumishi wa
Umma, Kampasi ya Singida awamu ya pili mara baada ya kufika katika eneo
hilo
Muonekano wa
baadhi ya majengo ya Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Singida ambayo
tayari yameshakamilika
Mnufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii- TASAF
katika Kijiji cha Ughaugha Kata ya Unyamikumbi, Manispaa ya Singida, Mariamu
Luguti ambaye amewezeshwa kufuga mbuzi akizungumza mbele ya Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete ambapo ameishukuru Serikali kwa
kumsaidia kuondokana kwenye lindi la umasikini
Kaimu Mkuu wa
Chuo na Mtendaji Mkuu, Chuo cha Utumishi wa Umma Dkt. Ernest Mabonesho
akizungumza mbele ya Naibu Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani
Kikwete
ambapo amesema ujenzi umefikia asilimia
21wa Chuo cha Utumisi wa Umma Kampasi ya Singida
No comments:
Post a Comment