Na. Veronica Mwafisi-Dodoma
Tarehe 24 Agosti, 2023
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ameipongeza Taasisi ya Watumishi Housing Investments (WHI) kwa kuendelea kujenga makazi bora ya watumishi wa umma nchini na kuwasisitiza kuelekeza nguvu zaidi ya ujenzi jirani na maeneo ambayo watumishi wanafanya kazi ili kuwaondolea changamoto ya makazi kwa lengo la kuboresha utendaji kazi.
Me. Simbachawene amezungumza hayo jijini Dodoma wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua mradi wa ujenzi wa nyumba zilizojengwa na taasisi hiyo eneo la Njedengwa na Kisasa Relini kwa lengo la kuwauzia na kuwapangisha watumishi wa umma na wanachama wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
Mhe. Simbachawene amesema kitendo cha watumishi wa umma kutokuwa na makazi bora na kuwa mbali na maeneo yao wanayofanyia kazi ni changamoto kubwa inayoathiri utendaji kazi, hivyo ameisisitiza taasisi hiyo kuona umuhimu wa kufanya hivyo kwani licha ya kuwasaidia watumishi kupata makazi bora watakuwa wametekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi na maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hasssan ya kuhimiza uwepo wa makazi bora kwa watumishi ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Mhe. Simbachawene ameongeza kuwa, umuhimu wa kuwa na makazi bora karibu na maeneo ya kazi, kutawasaidia watumishi hasa wanaoajiriwa kwa mara ya kwanza maeneo ambayo yana changamoto ya nyumba, kutohangaika.
“Mkijenga nyumba maeneo ya jirani na vituo vya kazi, kutawasaidia sana watumishi hasa wa ajira mpya kutopata changamoto na kuchukia kazi kwa sababu ya kuhangaika kutafuta sehemu nzuri ya kuishi,” Mhe. Simbachawene amesisitiza.
Kwa upande wake Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete ameungana na Mhe. Simbachawene kuipongeza taasisi hiyo kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kujenga nyumba bora kwa ajili ya kuwauzia na kuwapangisha watumishi wa umma na wanachama wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
Naye, Mtendaji Mkuu wa Watumishi Housing Investments (WHI) Dkt. Fredy Msemwa, amewashukuru viongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kutembelea mradi wa ujenzi wa nyumba zinazojegwa na taasisi hiyo katika eneo la Kisasa Relini na Njedengwa na kuhimiza uwajibikaji na ubunifu.
Dkt. Msemwa
amewaahidi viongozi hao kuwa, watayafanyia kazi maelekezo yote ambayo wameyatoa
kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na
Waandishi wa Habari mara baada ya kukagua mradi wa nyumba zilizojengwa na Watumishi
Housing Investments (WHI) eneo la Njedengwa na Kisasa Relini jijini Dodoma wakati wa ziara yake ya kikazi
iliyolenga kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa WHI.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza kabla ya
kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kuzungumza na Waandishi wa Habari mara
baada ya kukagua mradi wa nyumba zilizojengwa na Watumishi
Housing Investments (WHI) eneo la Njedengwa na Kisasa Relini jijini Dodoma wakati wa ziara yake ya kikazi
iliyolenga kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa WHI.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akimsikiliza Mkurugenzi
Mtendaji wa Watumishi Housing Investments (WHI), Dkt. Fred Msemwa alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi
wa nyumba zilizojengwa na WHI eneo la Njedengwa na Kisasa
Relini jijini Dodoma. Kulia kwake ni Naibu
Katibu Mkuu wa Ofisi yake, Bw. Xavier Daudi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiambatana na Naibu Waziri
wake, Mhe. Ridhiwani Kikwete na Naibu Katibu Mkuu
wa Ofisi yake, Bw. Xavier Daudi wakielekea kukagua mradi wa nyumba zilizojengwa na Watumishi
Housing Investments (WHI) eneo la Njedengwa jijini Dodoma wakati wa ziara yake ya kikazi
iliyolenga kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa WHI.
Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi
akimuonyesha Mtendaji wa Watumishi Housing Investments (WHI), Dkt.
Fred Msemwa namna alivyovutiwa na mojawapo ya nyumba zilizojengwa
na Watumishi Housing Investments (WHI) walipokuwa
wakimsubiri Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kukagua
mradi wa nyumba hizo
eneo la Kisasa Relini jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akifurahia jambo na
Menejimenti ya Watumishi Housing Investments (WHI) wakati wa ziara yake ya
kikazi iliyolenga kukagua nyumba zilizojengwa na Watumishi
Housing Investments (WHI) eneo la Njedengwa na Kisasa Relini jijini Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza jambo na
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi
wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene iliyolenga kukagua mradi
wa nyumba zilizojengwa na Watumishi Housing Investments
(WHI) eneo la Njedengwa na Kisasa Relini jijini Dodoma.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Watumishi Housing Investments (WHI), Dkt. Fred Msemwa akitoa ufafanuzi
kwa Waandishi wa Habari kuhusu mradi wa nyumba zilizojengwa na WHI eneo la
Njedengwa na Kisasa Relini jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment