Monday, August 14, 2023

KAMATI YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YAIPONGEZA OFISI YA RAIS-UTUMISHI KWA KUJIPANGA KIKAMILIFU KATIKA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE

 

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama akiongoza kikao kazi cha kamati yake na viongozi pamoja na watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhusu Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa mwaka 2022/23 kilichofanyika jijini Dodoma.

Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) wakati akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti wa Ofisi yake kwa mwaka 2022/23.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti wa Ofisi yake kwa mwaka 2022/23 kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao cha kamati hiyo kilichofanyika jijini Dodoma.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akitoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo kuhusu Utekelezaji wa Mpango na Bajeti wa Ofisi yake kwa mwaka 2022/23 kilichofanyika jijini Dodoma.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete (Wa kwanza kulia), Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi (Wa pili kutoka kulia), Katibu Mkuu-IKULU, Bw. Mululi Majula Mahendeka (Wa tatu kutoka kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, CP Salum Hamduni (Wa nne kutoka kulia) wakisikiliza hoja za Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala Katiba na Sheria wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo kuhusu Utekelezaji wa Mpango na Bajeti wa Ofisi yake kwa mwaka 2022/23.


Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Tumaini Magessa akiwasilisha hoja wakati wa kikao kazi cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria na viongozi pamoja na watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhusu Utekelezaji wa Mpango na Bajeti Kwa Mwaka 2022/23.


Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, CP Salum Hamduni akijibu moja ya hoja ya taasisi yake kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na taasisi zake kuhusu Utekelezaji wa Mpango na Bajeti Kwa Mwaka 2022/23.


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji-TASAF, Bw. Shedrack Mziray akijibu hoja za wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria iliyoelekezwa kwa taasisi yake wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na taasisi zake kuhusu Utekelezaji wa Mpango na Bajeti Kwa Mwaka 2022/23.

Sehemu ya Wakurugenzi wa taasisi zilizopo chini ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na ofisi hiyo kuhusu Utekelezaji wa Mpango na Bajeti Kwa Mwaka 2022/23 kilichofanyika jijini Dodoma.


Sehemu ya Wakurugenzi wa Ofisi ya ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwa katika kikao kazi cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria na watendaji wa ofisi hiyo kuhusu Utekelezaji wa Mpango na Bajeti Kwa Mwaka 2022/23 kilichofanyika jijini Dodoma.

 



No comments:

Post a Comment