Monday, November 28, 2022

MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AFUNGUA MKUTANO MKUU WA 10 WA CHAMA CHA KITAALUMA CHA MENEJIMENTI YA KUMBUKUMBU NA NYARAKA TANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akifungua mkutano mkuu wa 10 wa Chama cha Kitaaluma cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) jijini Arusha.


Sehemu ya washiriki wa mkutano mkuu wa 10 wa Chama cha Kitaaluma cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) wakifurahia jambo wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akifungua mkutano huo jijini Arusha.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kufungua mkutano mkuu wa 10 wa Chama cha Kitaaluma cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) jijini Arusha.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Lauren Ndumbaro (wa kwanza kushoto mstari wa mbele) akimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa 10 wa Chama cha Kitaaluma cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) jijini Arusha. Wengine ni Katibu Mkuu-TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe, Mwenyekiti wa Kamati ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Abdallah Chaurembo na Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa, Bw. Shaka Hamdu Shaka.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama cha Kitaaluma cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA), Bi. Josephine Manase ya kutambua mchango anaoutoa katika taaluma ya utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka mara baada ya kufungua mkutano mkuu wa 10 wa Chama cha Kitaaluma cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) jijini Arusha.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia zawadi aliyokabidhiwa na Chama cha Kitaaluma cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) ya kutambua mchango anaoutoa katika taaluma ya utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka mara baada ya kufungua mkutano mkuu wa 10 wa Chama cha Kitaaluma cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) jijini Arusha.

 

No comments:

Post a Comment