Na. James K. Mwanamyoto-Masasi
Tarehe 24 Novemba, 2022
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama amesema, Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) umetekeleza maelekezo ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ya kujenga barabara zenye urefu wa kilometa 1.6 kwa gharama nafuu katika Kijiji cha Nangose, Kata ya Temeke, Halmashauri ya Mji wa Masasi ambazo hazikuwahi kujengwa tangu taifa lipate uhuru.
Mhe. Jenista amesema hayo wakati akizungumza na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini na wananchi wa Kijiji cha Nangose mara baada ya kukagua barabara hizo zilizojengwa na TASAF kupitia mradi wa ajira za muda.
Mhe. Jenista amesema, Serikali ya Awamu ya Sita imeweza kujenga barabara zenye urefu wa Kilometa 1.6 katika Kijiji cha Nangose, ambapo tangu nchi ipate uhuru hakukuwa na barabara zaidi ya kuwepo na njia za miguu ambazo zilikuwa ni kikwazo cha kijiji hicho kupata maendeleo.
“Barabara hizi zimejengwa kupitia mradi wa ajira za muda kwa gharama nafuu sana ambayo ni kiasi cha shilingi milioni 3.6, ambapo fedha hiyo ililipwa kwa walengwa wa TASAF waliokuwa wakifanya kazi kwenye mradi wa ujenzi wa barabara hizo,” Mhe. Mhagama amefafanua.
Katika kuhakikisha barabara hizo zinakuwa na tija kwa maendeleo ya wananchi katika kijiji hicho, Mhe. Mhagama amemtaka Meneja wa TARURA Halmashauri ya Mji Masasi kuimarisha barabara hizo ili zitumike kwa muda mrefu na kuwa chachu ya maendeleo katika Kijiji cha Nangose.
Naye, Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Mhe. Claudia Kitta amesema kuwa wananchi wa Kijiji cha Nangose ambao ni walengwa wa TASAF wamefanya kazi ya ujenzi wa barabara hizo zenye urefu wa kilomita 1.6 kupitia mradi wa ajira za muda, na kuongeza kuwa katika Halmashauri ya Mji Masasi zipo barabara 40 ambazo zimejengwa na TASAF kupitia mradi huo wa ajira za muda.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Kijiji cha Nangose, Diwani wa Kata ya Temeke kwa tiketi ya CHADEMA, Mhe. Frank Malanjila amesema kabla ya TASAF kuwezesha ujenzi wa barabara katika kata yake, kulikuwa na changamoto kubwa lakini kwasasa barabara zilizojengwa zimeunganisha vijiji na kuwawezesha wananchi kutoka eneo moja kwenda jingine, ikiwa ni pamoja na kusafirisha bidhaa na mazao yao kwa urahisi tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
Awali akiwasilisha
taarifa ya utekelezaji wa mradi huo wa TASAF wa ajira za muda, Mtendaji wa
Kijiji cha Nangose, Bi. Salma Ngatimwa amesema, mradi ulibuniwa na wananchi na kutekelezwa
kwa kipindi cha miezi sita kuanzia Septemba 2021 hadi Februari 2022 na kuongeza
kuwa, walengwa walianza kutekeleza mradi huo wa ujenzi wa barabara kwa
kusafisha eneo, kung’oa miti na kutengeneza mifereji.
1. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Jenista Mhagama akikagua
barabara iliyojengwa na walengwa wa TASAF kupitia mradi wa ajira za muda katika
Kijiji cha Nangose Kata ya Temeke, Halmashauri ya Mji Masasi wakati wa ziara
yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF wilayani Masasi.
1. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na
walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini na wananchi wa Kijiji cha Nangose
Kata ya Temeke, Halmashauri ya Mji Masasi wakati wa ziara yake ya kikazi ya
kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF wilayani Masasi.
1. Sehemu ya Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini na Wananchi wa Kijiji cha Nangose Kata ya Temeke Halmashauri ya Mji Masasi wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista
Mhagama alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara
yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF Wilayani Masasi.
1. Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Mhe. Claudia Kitta akitoa neno la utangulizi kuhusiana na utekelezaji wa miradi ya TASAF katika wilaya yake kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama kuzungumza na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini na wananchi wa Kijiji cha Nangose Kata ya Temeke Halmashauri ya Mji Masasi wakati wa ziara ya kikazi ya Mhe. Jenista ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF wilayani Masasi.
1. Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Nangose Kata ya Temeke, Halmashauri ya Mji
Masasi, Bi. Salma Ngatimwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mpango wa
Kunusuru Kaya Maskini wa Kijiji cha Nangose kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF Wilayani Masasi.
1. Diwani
wa Kata ya Temeke kwa tiketi ya CHADEMA, Mhe. Frank Malanjila akiishukuru
Serikali kwa kujenga barabara kupitia TASAF wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama ya kukagua
utekelezaji wa miradi ya TASAF katika kata yake.
1. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Jenista Mhagama akimsikiliza Diwani wa Kata ya Temeke kwa tiketi
ya CHADEMA, Mhe. Frank Malanjila (hayupo pichani) alipokuwa akiishukuru
Serikali kwa kujenga barabara kupitia TASAF katika kata yake wakati wa ziara ya
kikazi ya Waziri Jenista
iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF wilayani Masasi.
1.
Mwananchi wa Kijiji cha
Nangose, Kata ya Temeke, Halmashauri ya Mji Masasi, Bw. Daniel Maulana
akiwasilisha hoja kuhusiana na utekelezaji wa miradi ya TASAF kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama wakati wa ziara
ya kikazi ya Waziri Jenista iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF
wilayani Masasi.
1. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na
watendaji wa Wilaya ya Masasi alipowasili wilayani humo kwa ziara ya kikazi ya
kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF wilayani humo.
No comments:
Post a Comment