Friday, June 24, 2022

ZAWADI YA KEKI YA KUMBUKUMBU YA SIKU YA KUZALIWA KWANGU NI KIASHIRIA CHA USHIRIKIANO MZURI KIUTENDAJI TULIONAO OFISI YA RAIS UTUMISHI - Mhe. Jenista

 Na. James K. Mwanamyoto-Dodoma

Tarehe 24 Juni, 2022

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama amesema zawadi ya keki ya kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa aliyozawadiwa na watumishi wa ofisi yake ni kiashiria cha umoja na ushirikiano wa kiutendaji baina yake na watumishi hao.

Mhe. Jenista amesema hayo jana, Siku ya Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, 2022 baada ya kupokea zawadi hiyo ya keki pindi alipomaliza kutoa huduma kupitia Kituo cha Huduma kwa Mteja cha ofisi yake.

Waziri Jenista amesema, amefarijika kupewa zawadi ya keki ya kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwake ambayo kwa namna ya pekee imeenda sambamba na Siku ya Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, tarehe 23 Juni, 2022 na yeye akiwa ndiye waziri mwenye dhamana ya kusimamia masuala ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora nchini.

Mhe. Jenista ameongeza kuwa, mara baada ya kufanya kazi ya kuwahudumia watumishi wa umma kupitia kituo cha huduma kwa mteja, ameona surprise ya menejimenti kumletea zawadi ya keki hivyo ni kitendo kinachoonesha umuhimu wa umoja na kufanya kazi kama timu (team work).

“Mkiwa na team work mahali popote iwe ni kwenye kazi au jambo lolote ni lazima tija itapatikana, hivyo kitendo cha kupatiwa zawadi ya keki kinadhihirisha kuwa Ofisi ya Rais-UTUMISHI yenye dhamana ya kusimamia Utumishi wa Umma inaongoza kwa vitendo katika kuhimiza utekelezaji wa majukumu kwa ushirikiano,” Mhe Jenista amesisitiza.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama ametumia fursa hiyo kutoa wito na kuwahamasisha watumishi wa umma wote nchini kufanya kazi kama timu.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama (kushoto) akikata keki ya kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa, aliyozawadiwa na watumishi wa ofisi yake mara baada ya kumaliza kutoa huduma kupitia Kituo cha Huduma kwa Mteja cha ofisi yake, Siku ya Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, 2022. Anayeshuhudia ni Naibu Waziri wake Mhe. Deogratius Ndejembi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama (kushoto) akisheherekea siku yake ya kuzaliwa na Naibu Waziri wake Mhe. Deogratius Ndejembi mara baada ya kumaliza kutoa huduma kupitia Kituo cha Huduma kwa Mteja cha ofisi yake, Siku ya Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, 2022. 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akitakiwa heri ya maisha marefu na afya njema na Naibu Waziri wake Mhe. Deogratius Ndejembi pamoja na watendaji wa ofisi yake katika siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akifurahia jambo na watendaji wa ofisi yake mara baada ya watendaji hao kumzawadia keki ya siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.











No comments:

Post a Comment