Wednesday, June 22, 2022

WAZIRI JENISTA AIPONGEZA NMB KWA KUITIKIA WITO WA MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN WA KUWAJALI WATUMISHI WA UMMA

Na. Veronica E. Mwafisi-Dodoma

Tarehe 22 Juni, 2022

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Jenista Mhagama ameipongeza Benki ya NMB kwa kuitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan wa kuzitaka taasisi binafsi kushirikiana na Serikali katika kuwajali Watumishi wa Umma nchini ili kuinua uchumi wao na kutekeleza majukumu yao kikamilifu kwa maendeleo ya taifa.

Mhe. Jenista ameyasema hayo alipokuwa akifungua warsha ya Walimu wa Mkoa wa Dodoma iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa lengo la kuwajengea uelewa wa elimu ya kifedha na bidhaa mbalimbali za benki hiyo.

Waziri Jenista amesema, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan mara kwa mara amekuwa akizisisitiza taasisi binafsi kushirikiana na Serikali kuendelea kuwajali Watumishi wa Umma popote walipo ambapo benki hiyo ya NMB ikiwa ni miongoni mwa taasisi nyingine za kifedha imekuwa ikibuni mipango mbalimbali katika kutekeleza agizo hilo. 

“Naipongeza Benki ya NMB kwa kutekeleza agizo hilo la Mhe. Rais la kushirikiana na Serikali kwa kuja na wazo la kuwajengea uelewa Walimu ambao ndio kundi kubwa la Watumishi wa Umma nchini na kuanzisha mpango maalum ujulikanao kwa jina la Mwalimu Spesho ili kuwasaidia walimu kuendesha maisha yao,” Mhe. Jenista amesisitiza. 

Mhe. Jenista ameishauri Benki ya NMB kuanzisha mpango huo wa Mwalimu Spesho katika mikoa mingine nchini badala ya kuishia Mkoa wa Dodoma pekee ili Walimu wote nchini wanufaike na mpango huo muhimu katika kuinua uchumi wao. 

Kwa upande wake Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Bw. Filbert Mponzi amesema, warsha hiyo inajumuisha Walimu zaidi ya 400 kutoka shule za Msingi, Sekondari na baadhi ya Wakuu wa Vyuo vya Ualimu katika Halmashauri ya Mkoa wa Dodoma.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizindua huduma mpya zilizotengwa mahsusi na Benki ya NMB kwa ajili ya Walimu wakati wa warsha ya Walimu wa Mkoa wa Dodoma iliyoandaliwa na Benki ya NMB jijini Dodoma.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akimuelekeza jambo Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Bw. Filbert Mponzi wakati wa warsha ya Walimu wa Mkoa wa Dodoma iliyoandaliwa na Benki ya NMB jijini Dodoma.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Walimu wa Mkoa wa Dodoma (hawapo pichani) kwenye warsha ya Walimu wa Mkoa huo iliyoandaliwa na Benki ya NMB jijini Dodoma.


Sehemu ya Walimu wa Mkoa wa Dodoma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa warsha ya Walimu wa mkoa huo iliyoandaliwa na Benki ya NMB jijini Dodoma.


Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Mhe. Jabir Shekimweri akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama kuzungumza na Walimu wa Mkoa wa Dodoma na kufungua warsha ya Walimu wa mkoa huo iliyoandaliwa na Benki ya NMB jijini Dodoma.


Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Bw. Filbert Mponzi akieleza lengo la warsha ya Walimu wa Mkoa wa Dodoma iliyoandaliwa na Benki ya NMB kabla ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama kufungua warsha hiyo jijini Dodoma.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akifurahi baada ya Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Bw. Filbert Mponzi kumuonyesha huduma mpya zilizotengwa mahsusi na Benki ya NMB kwa ajili ya Walimu wakati wa warsha ya Walimu wa Mkoa wa Dodoma iliyoandaliwa na Benki ya NMB jijini Dodoma.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akimpongeza Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Bw. Filbert Mponzi baada ya Waziri Jenista kuzindua huduma mpya zilizotengwa mahsusi na Benki ya NMB kwa ajili ya Walimu wakati wa warsha ya Walimu wa Mkoa wa Dodoma iliyoandaliwa na Benki ya NMB jijini Dodoma.


 

No comments:

Post a Comment