Friday, June 24, 2022

WATUMISHI 104 WAHUDUMIWA NA VIONGOZI WA OFISI YA RAIS-UTUMISHI KUPITIA NAMBA 026 2160240 YA KITUO CHA HUDUMA KWA MTEJA CHA OFISI HIYO KATIKA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA, 2022 - Mhe. Jenista

 Na. James K. Mwanamyoto-Dodoma

Tarehe 24 Juni, 2022 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama amesema watumishi wa umma 104 wamehudumiwa na viongozi wa ofisi yake kupitia namba ya simu 026 2160240 ya kituo cha huduma kwa mteja (call center) cha Ofisi hiyo wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, 2022.

Mhe. Jenista amesema hayo jijini Dodoma, mara baada ya kujumuika na watendaji wa ofisi yake kutoa huduma kwa watumishi wa umma na wananchi kupitia kituo cha huduma kwa mteja cha ofisi yake siku ya Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, 2022.

Mhe. Jenista amesema, yeye mwenyewe Waziri mwenye dhamana ya kumsaidia Mhe. Rais kusimamia Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Naibu Waziri wake Mhe. Deogratius Ndejembi, Katibu Mkuu Dkt. Laurean Ndumbaro, Naibu Katibu Mkuu Bw. Xavier Daudi na baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo wametoa huduma kwa watumishi 104 ambao walipiga simu kupitia namba ya kituo cha huduma kwa mteja cha ofisi yake wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, 2022.

Ameongeza kuwa, katika kipindi cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2022, ofisi yake ilidhamiria kuhakikisha changamoto zote zinazowakabili watumishi wa umma zinatatuliwa papo kwa hapo kwa watumishi watakaoziwasilisha kwa kupiga simu ya kituo cha huduma kwa mteja cha ofisi yake.

Tumefanikiwa kutatua kero, changamoto na malalamiko ya watumishi wa umma 21 ambayo yamepatiwa ufumbuzi papo kwa hapo kupitia namba ya simu ya kituo cha huduma kwa mteja, na changamoto za watumishi 83 zimeelekezwa kwenye wizara na taasisi husika ili zifanyiwe kazi, Mhe. Jenista amefafanua.

Akieleza sababu ya changamoto za watumishi wa umma 83 kuelekezwa kwenye wizara na taasisi nyingine za Serikali ili zifanyiwe kazi, Mhe. Jenista amesema kuwa sababu ni mamlaka hizo ndio zimekasimiwa majukumu ya kutatua changamoto hizo za watumishi hao, akitoa mfano wa suala la uhamisho wa Mtendaji Kata wa Nachingwea, Bw. Peter Shimweju ambaye mamlaka yake ya uhamisho ni Ofisi ya Rais-TAMISEMI.

Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma hufanyika kila mwaka kuanzia tarehe 16-23 Juni, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ndiyo yenye jukumu la kuratibu maadhimisho hayo katika ngazi ya taifa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama (aliyekaa) akimhudumia Mtumishi aliyepiga simu kwenye Kituo cha Huduma kwa Mteja (Call Centre) cha Ofisi yake alipojumuika na watendaji wa ofisi yake kutoa huduma kwa watumishi wa umma na wananchi kupitia kituo hicho ikiwa ni kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, 2022. 


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akitoa huduma pamoja watendaji wa ofisi yake kupitia Kituo cha Huduma kwa Mteja (Call Centre) cha Ofisi ya Rais-UTUMISHI, ikiwa ni kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, 2022.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama (aliyekaa) akifuatilia kwa makini mazungumzo ya mwananchi aliyepiga simu kwenye Kituo cha Huduma kwa Mteja (Call Centre) cha Ofisi ya Rais-UTUMISHI alipojumuika na watendaji wa ofisi yake kutoa huduma kwa watumishi wa umma na wananchi kupitia kituo hicho ikiwa ni kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, 2022. 


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na baadhi ya Watendaji wa ofisi yake (hawapo pichani) alipokuwa akitoa takwimu ya watumishi wa umma waliohudumiwa na viongozi wa ofisi yake kupitia namba ya simu 026 2160240 ya kituo cha huduma kwa mteja (call center) cha Ofisi yake wakati wa kile cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, 2022.


Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Maadili, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Leila Mavika (kulia) akimpokea Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama alipowasili katika Ofisi zake za UDOM kujumuika na watendaji wa ofisi yake kutoa huduma kwa watumishi wa umma na wananchi kupitia kituo cha huduma kwa mteja cha ofisi yake ikiwa ni kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, 2022. 


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na baadhi ya Wakurugenzi wa ofisi yake mara baada ya kuwasili katika Ofisi zake za UDOM kujumuika na watendaji wa ofisi yake kutoa huduma kwa watumishi wa umma na wananchi kupitia kituo cha huduma kwa mteja cha ofisi yake ikiwa ni kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, 2022. 



 

No comments:

Post a Comment