Na. James Mwanamyoto-Pemba
Tarehe 27 Juni, 2022
Mhe. Chaurembo amesema hayo wakati wa ziara ya kikazi ya kamati yake iliyolenga kukagua utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi ya kujenga uzio, kukarabati madarasa na ofisi katika Skuli ya Sekondari ya Piki Pemba.
“Mama yetu Samia Suluhu Hassan na Dkt. Hussein Mwinyi ndio walioielekeza TASAF kujenga uzio, kukarabati madarasa, ofisi na stoo katika skuli hii ya Piki ili kuweka mazingira rafiki kwa wanafunzi kupata elimu bora, hivyo kamati yangu imekuja kukagua utekelezaji wa maelekezo hayo na imeridhika na hatua iliyofikiwa,” Mhe. Chaurembo amefafanua.
Mhe. Chaurembo ameongeza kuwa, kamati yake iliidhinisha nyongeza ya fedha kwa TASAF baada ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kuelekeza madarasa ya Skuli ya Piki kukarabatiwa ambaye amedhamiria kuboresha miundombinu ya sekta ya elimu nchini.
Akiainisha kiasi cha fedha kilichotengwa na kuidhinishwa kwa ajili ya utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, Mhe. Chaurembo amesema kiasi ya shilingi milioni 328 kimetolewa na Serikali kupitia TASAF na mpaka sasa ujenzi wa mradi uko katika hatua nzuri kwani umefikia asilimia 85.
Kwa upande wake, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amesema kuwa mradi wa ujenzi wa uzio na madarasa katika Skuli ya Piki ni faida mojawapo ya muungano kati ya Tanzania Bara na Zanzibar kwa sababu Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ni matunda ya muungano na ndio maana ameambatana na kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa (USEMI) kwa ajili ya ukaguzi wa mradi huo ambao Mhe. Rais ameelekeza utekelezwe.
“Uwepo wa kamati hii ya USEMI katika Shehia ya Piki ni taswira ya umoja wa taifa letu, ni taswira ambayo inalindwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi ambao wanapigania utekelezaji wa miradi ya muungano na taifa kwa ujumla,” Mhe. Ndejembi amesisitiza.
Naye, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Hamza Juma amesema mradi huo wa ujenzi wa uzio na ukarabati wa madarasa katika Skuli ya Piki ni matunda ya Muungano hivyo wanaoubeza Muungano wanabeza maendeleo katika sekta ya elimu.
Mhe. Juma amesema licha ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutekeleza miradi ya maendeleo kupitia fedha zake, lakini inatekeleza miradi yenye sura ya muungano kwa kutumia fedha zinazotoka kwenye bajeti ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ukiwemo mradi huo wa ujenzi wa uzio na madarasa katika Skuli ya Piki Pemba.
Wajumbe Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa (USEMI) imehitimisha ziara yake yake ya kikazi ya siku moja mjini Pemba, iliyolenga kukagua utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) katika Shehia ya Piki na Kendwa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa (USEMI), Mhe. Abdallah Chaurembo akizungumza na walengwa wa TASAF wa Shehia ya Piki wakati wa ziara ya kikazi ya kamati yake iliyolenga kukagua utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kujenga uzio, kukarabati madarasa na ofisi katika Skuli ya Sekondari ya Piki Pemba.
Baadhi ya walengwa wa TASAF wa Shehia ya Piki wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa (USEMI), Mhe. Abdallah Chaurembo (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara ya kikazi ya kamati hiyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ya kujenga uzio, kukarabati madarasa na ofisi katika Skuli ya Sekondari ya Piki Pemba.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa (USEMI), Mhe. Abdallah Chaurembo kuzungumza na walengwa wa TASAF wa Shehia ya Piki wakati ziara ya kikazi ya kamati hiyo Pemba.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Hamza Juma akitoa akieleza manufaa ya mradi wa ujenzi wa uzio na ukarabati wa madarasa katika Skuli ya Piki kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa (USEMI) wakati wa ziara ya kikazi ya kamati hiyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ya kuboresha miundombinu ya skuli hiyo iliyopo Shehia ya Piki Pemba.
Mwakilishi wa walengwa wa TASAF Shehia Piki, Bw. Suleiman Massoud akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa uzio na ukarabati wa madarasa katika Skuli ya Piki kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa (USEMI) wakati wa ziara ya kikazi ya kamati hiyo, iliyolenga kukagua utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ya kuboresha miundombinu ya skuli hiyo iliyopo Shehia ya Piki Pemba.
Mwonekano wa uzio unaojengwa na TASAF katika skuli ya Piki, ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ya kuboresha miundombinu ya skuli hiyo iliyopo Shehia ya Piki Pemba.
Mwonekano wa baadhi ya madarasa yanayokarabatiwa na TASAF katika skuli ya Piki, ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ya kuboresha miundombinu ya skuli hiyo iliyopo Shehia ya Piki Pemba.
No comments:
Post a Comment