Na. Veronica Mwafisi-Dodoma
Tarehe 29 Aprili, 2022
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amewasisitiza watendaji katika taasisi za Serikali kuzingatia maelekezo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa ya kuimarisha eneo la ufuatiliaji na tathmini ili kuwa na mipango yenye tija kwa maendeleo ya taifa.
Akifunga
kongamano la kwanza la ufuatiliaji na tathmini
nchini lililofanyika katika ukumbi wa PSSSF (Makole) jijini Dodoma,
Mhe. Ndejembi amesema Mhe. Waziri Mkuu katika hotuba yake ya ufunguzi wa
kongamano hilo alitoa maelekezo ya namna ya kuboresha masuala ya ufuatiliaji na
tathmini pamoja na kongamano kwa miaka ijayo ili kubaini nchi imepiga hatua kwa
kiasi gani katika maendeleo, inakabiliana na changamoto zipi kufikia malengo na
hatua za kuchukua kukabiliana na changamoto hizo.
Mhe.
Ndejembi amesema kongamano hilo lililenga kuwakutanisha watalaam na watendaji
wa ufuatiliaji na tathmini wa ndani na nje ya nchi ili kujadili masuala ya
ufuatiliaji na tathmini.
“Nina
imani kuwa kupitia kongamano hili, mmepata fursa ya kubadilishana uzoezi na
kuongeza uelewa kwenye masuala ya ufuatiliaji na tathmini, uzoefu mlioupata uwe
ni chachu katika kuboresha namna ya kusimamia utekelezaji wa majukumu ya
ufuatiliaji na tathmini katika taasisi zetu,” Mhe. Ndejembi amesisitiza.
Aidha,
Mhe. Ndejembi amezipongeza taasisi zote zilizopata tuzo na kutaka tuzo hizo
ziwe chachu ya kuongeza uwajibikaji na kuzitaka taasisi nyingine za Serikali
kufanya vizuri kwenye eneo la ufuatiliaji na tathmini sio kwa ajili ya kupata
tuzo tu bali kuimarisha utendaji kazi katika taasisi zao.
Kongamano
hilo la kitaifa lililofanyika kwa mara ya kwanza nchini liliwashirikisha watalaam
wa masuala ya ufuatiliaji na tathmini kutoka nchi mbalimbali ambazo ni
Tanzania, Marekani, Uingereza, Ghana, Afrika ya kusini, Kenya, Uganda na
Zimbabwe.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akifunga kongamano la kwanza
la ufuatiliaji na tathmini nchini lililofanyika katika ukumbi wa PSSSF (Makole)
jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wa kongamano la ufuatiliaji na tathmini
wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) alipokuwa akifunga kongamano la kwanza
la ufuatiliaji na tathmini nchini lililofanyika katika ukumbi wa PSSSF (Makole)
jijini Dodoma.
Kaimu Katibu Mkuu, Bw. Hassan Kitenge akimkaribisha Naibu Waziri,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius
Ndejembi kufunga kongamano la kwanza la ufuatiliaji na tathmini
nchini lililofanyika katika ukumbi wa PSSSF (Makole) jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Udara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi, Bw.
Nolasco Kipanda akiwasilisha kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi maazimio ya kongamano la kwanza
la ufuatiliaji na tathmini nchini wakati Naibu Waziri huyo alipokuwa akifunga
kongamano hili jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment