Na. Veronica Mwafisi-Dar es Salaam
Tarehe 25 Aprili, 2022
Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama, ameilekeza
Taasisi ya Uongozi kufanya tafiti za kina kwa viongozi ili kubaini mapungufu waliyonayo
kwa lengo la kuandaa programu zitakazosaidia kutoa mafunzo kulingana na
mapungufu yatakayobainishwa hatimaye kuwa na viongozi bora kwa ustawi wa
maendeleo ya taifa.
Mhe. Jenista ameyasema
hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kikazi katika Taasisi ya
Uongozi iliyolenga kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa taasisi hiyo.
“Tunataka mtutizame sisi viongozi ili muweze
kubaini mapungufu tuliyonayo na kututengenezea programu zitakazosaidia
kuboresha mapungufu yetu, kama Taasisi ya Uongozi tunatakiwa tufikiri kwa kina kuona
ni namna gani tunaweza kusaidia katika hili,” Mhe. Jenista amesisitiza.
Mhe. Jenista amesema ari
aliyonayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa
nchi yake ni kubwa sana na ndio maana amekuwa akisisitiza sana suala la kufanya
tathmini na ufuatiliaji hivyo, ni vizuri kujua kinachohitajika na kutumia tathmini
zilizopo ili zisaidie kuboresha kwa maendeleo ya taifa.
Mhe. Jenista ameongeza
kuwa viongozi wanahitaji mafunzo ya kina, kwani mfumo wa kufikiri unaweza ukawa
ni ule ule tangu uhuru lakini ni vizuri wakapata mafunzo ili kuongeza vitu
vipya katika uelewa wa mambo mbalimbali.
Mhe. Jenista amesema ni vema Taasisi ya Uongozi iangalie majukumu shirikishi yanayoambatana na malengo makuu ya taasisi hiyo na kufikiri zaidi kwa kuitazama nchi na kuangalia maeneo yanayoweza kusaidia kufanya mageuzi makubwa kwa ustawi wa maendeleo ya taifa.
Aidha, Mhe. Jenista amewataka
watumishi wa taasisi hiyo kujifunza kutoka nchi nyingine mambo mazuri waliyo
nayo ili kupata ujuzi zaidi kwani taasisi inayofanana na ya kwao zipo kwenye
mataifa mengi ila zinatofautiana kwenye miundo na mifumo, hivyo kujifunza kutoka
kwao kutasaidia kupata ujuzi zaidi kwa maendeleo ya nchi yetu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na watumishi wa Taasisi wa Uongozi jijini Dar es
Salaam wakati wa ziara yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi hao. Kulia kwake ni Afisa Mtendaji Mkuu wa
Taasisi ya Uongozi, Bw. Kadari Singo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiwa kwenye kikao kazi na watumishi wa Taasisi wa Uongozi
jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji kwa
watumishi hao.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Bw. Kadari
Singo akielezea majukumu ya ofisi yake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama wakati
wa ziara ya kikazi ya Mhe. Jenista ya kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa
Taasisi ya Uongozi.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Bw. Kadari
Singo akipokea malekezo toka kwa kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama wakati wa ziara
ya kikazi ya Mhe. Jenista ya kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa Taasisi ya
Uongozi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akiwa katika picha ya pamoja na
watumishi wa Taasisi ya Uongozi baada ya kikao kazi chake na watumishi hao
kilicholenga kuhimiza uwajibikaji.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Mshauri
Mkuu-Ushirikiano, Bw. Konsta Heikkila baada ya kikao kazi chake na watumishi wa
Taasisi ya Uongozi kilicholenga kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa taasisi
hiyo.
No comments:
Post a Comment