Veronica Mwafisi-Dodoma
Tarehe 01 Juni, 2021
Watumishi watakaokuwa wakitoa
huduma kupitia Kituo cha Huduma kwa Wateja (Call centre Customer Service) cha
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma wanashiriki mafunzo ya namna
bora ya kutoa huduma kwa umma kupitia kituo hicho kinachotarajiwa kuzinduliwa
hivi karibuni.
Akifungua mafunzo hayo Jijini
Dodoma leo kwa niaba ya Katibu Mkuu-UTUMISHI, Mkurugenzi wa Mipango, Ofisi ya
Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Cosmas Ngangaji
amesema, kituo hicho kitasaidia wadau kupewa mrejesho wa masuala ya kiutumishi
kwa wakati tofauti na ilivyo sasa ambapo wanalazimika kusubiri wajibiwe kwa
barua.
Bw. Ngangaji amesema, utoaji
wa huduma kupitia kituo hicho utapunguza adha ya wanaohitaji huduma na kuongeza
kuwa, utajenga mahusiano mazuri kati ya Ofisi ya Rais-UTUMISHI na wadau wa
masuala ya kiutumishi na utawala bora kwani utarahisisha upokeaji wa maoni na malalamiko
ya kiutumishi yanayowasilishwa na kuyashughulikia kwa wakati.
“Ifahamike kuwa, uanzishwaji
wa kituo hicho hauondoi mifumo rasmi ya utoaji huduma na ushughulikiaji wa
malalamiko, bali ni moja ya utaratibu wa kisasa wa utoaji huduma kwa njia ya TEHAMA.”
Bw. Ngangaji amesisitiza.
Amefafanua kuwa, Kituo hicho
kitaunganishwa na Mfumo wa Kielektroniki wa Kushughulikia Malalamiko
(e-malalamiko) ambao umesanifiwa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa
Umma kwa kushirikiana na Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA).
Mafunzo hayo ya siku tatu yana
lengo la kujenga uelewa wa watumishi juu ya namna bora ya kuendesha kituo hicho
na kubadilishana uzoefu wa ushughulikiaji wa malalamiko na maoni ya wadau
ambayo yatakayoboresha uendeshaji wa Kituo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Idara ya Ukuzaji wa Maadili, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Bi. Leila Mavika, amemshukuru Bw. Ngangaji kwa maelekezo
aliyoyatoa na kuahidi kuwa kituo hicho kitatumika kujenga taswira nzuri ya
Ofisi na Serikali kwa ujumla.
Mkurugenzi wa Mipango, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Cosmas Ngangaji akifungua
mafunzo Jijini Dodoma leo kwa niaba ya Katibu Mkuu-UTUMISHI juu ya namna bora
ya kutoa huduma kwa umma kupitia Kituo cha Huduma kwa Wateja (Call centre
Customer Service) cha Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
kinachotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni.
Washiriki wa mafunzo ya namna bora ya kutoa huduma kwa umma kupitia Kituo cha Huduma kwa Wateja (Call centre Customer Service) cha Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma kinachotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni wakimsikiliza Mkurugenzi wa Mipango, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Cosmas Ngangaji alipokuwa akifungua mafunzo hayo Jijini Dodoma leo kwa niaba ya Katibu Mkuu-UTUMISHI.
Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji
wa Maadili, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi.
Leila Mavika, akitoa neno la shukurani kwa Mkurugenzi wa Mipango, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Ngangaji baada ya
Mkurugenzi huyo kufungua mafunzo kwa niaba ya Katibu Mkuu-UTUMISHI ya kutoa
huduma kwa umma kupitia Kituo cha Huduma kwa Wateja (Call centre Customer
Service) cha Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma kinachotarajiwa
kuzinduliwa hivi karibuni.
Mwezeshaji wa mafunzo ya namna
bora ya kutoa huduma kwa umma kupitia Kituo cha Huduma kwa Wateja (Call centre
Customer Service) cha Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
kinachotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni, Bw. James Sweke akitoa mafunzo kwa
washiriki wa mafunzo hayo leo Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Mipango, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Cosmas Ngangaji (aliyekaa
katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya namna bora ya
kutoa huduma kwa umma kupitia Kituo cha Huduma kwa Wateja (Call centre Customer
Service) cha Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma kinachotarajiwa
kuzinduliwa hivi karibuni baada ya Mkurugenzi huyo kufungua mafunzo hayo Jijini
Dodoma leo kwa niaba ya Katibu Mkuu-UTUMISHI.
No comments:
Post a Comment