Na. James Mwanamyoto-Dodoma
Tarehe 21 Juni, 2021
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema Serikali haitomvumilia Mkuu wa Idara yeyote katika taasisi ya umma atakayesababisha mtumishi kukosa stahili yake na mwananchi kukosa huduma bora.
Mhe. Mchegerwa ameyasema hayo wakati akifungua kikao kazi cha mwaka cha Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichofanyika katika ukumbi wa J.K. Nyerere, Chuo cha Mipango jijini Dodoma.
Mhe. Mchengerwa amewataka wakuu hao kutekeleza majukumu yao kikamilifu ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye ameelekeza viongozi katika taasisi za umma kutenda haki kwa watumishi walio chini yao na kutoa huduma bora kwa wananchi.
Amewaasa viongozi hao kutatua kero za watumishi na wananchi pindi wanapofuata huduma katika maeneo yao ya kazi na kuongeza kuwa, pindi atakapofanya ziara katika maeneo yao hategemei kukuta foleni kubwa ya wananchi wakisubiri huduma pasipokuwa na sababu ya msingi.
“Mimi, Naibu Waziri wangu na Watendaji wa Ofisi yangu tukifanya ziara katika taasisi yako, hatutegemei kukuta mlolongo wa foleni ya wanananchi wakisubiri huduma pasipo na matumaini yoyote,” Mhe. Mchengerwa amesisitiza.
Katika kutatua changamoto zinazowakabili watumishi na wananchi wanapohitaji huduma katika taasisi za umma, Mhe. Mchengerwa ameanzisha mfumo wa kielektroniki unaoitwa SEMA NA WAZIRI WA UTUMISHI ambao unatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni ili kutoa fursa kwa watumishi na wananchi kuwasilisha malalamiko yao na kufanyiwa kazi.
“Kupitia mfumo huu, nitakuwa na uwezo wa kuona malalamiko yanayowasilishwa popote nitakapokuwa na kufanya ufuatiliaji wa namna yalivyofanyiwa kazi na ofisi yangu,” Mhe. Mchengerwa ameongeza.
Kwa upande wake Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Festo Dugange amesema Mhe. Rais Samia amekuwa akisisitiza mara kwa mara matokeo chanya katika utekelezaji wa majukumu ya watumishi kwenye maeneo yao ya kazi.
Ameongeza kuwa ili matokeo hayo yaonekane, Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu hawana budi kusimamia utekelezaji wa majukumu ya watumishi wa umma kwa ufanisi.
Kikao kazi hicho cha siku mbili kinahudhuriwa na Wakurugenzi wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu kutoka kwenye Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala, Taasisi za Umma, Sekretariti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Mada mbalimbali zimewasilishwa ikiwemo Miundo ya Maendeleo ya Utumishi wenye Vyeo Tisa (9), Masuala Muhimu ya Usimamizi wa Utumishi wa Umma, Utekelezaji wa Mfumo Mpya wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara, Usimamizi wa Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa na mafunzo kuhusu uongozi.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akizungumza na Wakuu wa
Idara za Utawala na Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma alipokuwa akifungua
kikao kazi cha wakuu hao kilichofanyika katika ukumbi wa J.K. Nyerere, Chuo cha
Mipango jijini Dodoma.
Baadhi
ya Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma wakimsikiliza
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa alipokuwa
akifungua kikao kazi cha wakuu hao kilichofanyika katika ukumbi wa J.K.
Nyerere, Chuo cha Mipango jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Festo Dugange akitoa salam za
ofisi yake wakati wa kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu
katika Utumishi wa Umma kilichofanyika katika ukumbi wa J.K. Nyerere, Chuo cha
Mipango jijini Dodoma.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Dkt. Laurean Ndumbaro akitoa
neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa kufungua kikao
kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichofanyika
katika ukumbi wa J.K. Nyerere, Chuo cha Mipango jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed
Mchengerwa, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Festo Dugange na
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Dkt. Laurean Ndumbaro wakiwa katika kikao
kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichofanyika
katika ukumbi wa J.K. Nyerere, Chuo cha Mipango jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala
na Utumishi wa Umma, Bw. Mathew Kirama akitambulisha washiriki wa kikao kazi
cha Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma
kilichofanyika katika ukumbi wa J.K. Nyerere, Chuo cha Mipango jijini Dodoma.
Katibu Mkuu, Ofisi ya
Rais-UTUMISHI, Dkt. Laurean Ndumbaro akitoa ufafanuzi wa masuala ya kiutumishi
wakati wa kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu katika
Utumishi wa Umma kilichofanyika katika ukumbi wa J.K. Nyerere, Chuo cha Mipango
jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa akiwa
katika picha ya pamoja na Wakurugenzi na Wakurugenzi Wasaidizi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI
na TAMISEMI mara baada ya kufungua kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na
Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kilichofanyika katika ukumbi wa J.K.
Nyerere, Chuo cha Mipango jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment