Thursday, October 25, 2018

MHE. MKUCHIKA AMTEMBELEA MAKAMU WA RAIS MSTAAFU WA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT.MOHAMMED GARIB BILAL

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akisalimiana na Makamu wa Rais Mstaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Garib Bilal alipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam kumjulia hali.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akifafanua jambo kwa Makamu wa Rais Mstaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Garib Bilal alipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam kumjulia hali.

Makamu wa Rais Mstaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Garib Bilal akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) alipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam kumjulia hali.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) (kulia) akiagana na Makamu wa Rais Mstaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Mohammed Garib Bilal alipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam kumjulia hali.

Wednesday, October 24, 2018

SERIKALI YAWAPATIA HUDUMA YA USAFIRI WAJANE WA ALIYEKUWA MAKAMU WA RAIS WA TANZANIA, HAYATI ALHAJI ABOUD MWINYI JUMBE



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akikabidhi funguo ya gari kwa wajane wa aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Alhaji Aboud Mwinyi Jumbe, Bi.Zeyana Rashid (kushoto) na Bi. Fatma Mohammed Hassan (kulia) jijini Dar es Salaam.

Mmoja wa Wajane wa aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Alhaji Aboud Mwinyi Jumbe, Bi. Fatma Mohammed Hassan akiwasha gari baada ya kukabidhiwa funguo ya gari hilo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) (hayupo pichani) nyumbani kwa wajane hao jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na  wajane wa aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Alhaji Aboud Mwinyi Jumbe, Bi.Zeyana Rashid (kulia) na Bi. Fatma Mohammed Hassan (kushoto) mara baada ya kuwakabidhi gari la kuwahudumia.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akizungumza na familia ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Mzee Alhaji Aboud Mwinyi alipoitembelea familia hiyo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi.Jane Kajiru (katikati) akizungumza na familia ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Mzee Alhaji Aboud Mwinyi jijini Dar es Salaam.

Monday, October 22, 2018

SERIKALI YAWATAKA WAHITIMU WA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA KUFANYA KAZI KWA KUZINGATIA WELEDI NA NIDHAMU ILI KUONESHA TOFAUTI YA KIUTENDAJI NA WAHITIMU WENGINE



Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akimtunuku cheti mmoja wa wahitimu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) wakati wa mahafali ya 29 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wahitimu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) wakati akizungumza nao kwenye mahafali ya 29 ya chuo hicho, jijini Dar es Salaam.