Wednesday, October 24, 2018

SERIKALI YAWAPATIA HUDUMA YA USAFIRI WAJANE WA ALIYEKUWA MAKAMU WA RAIS WA TANZANIA, HAYATI ALHAJI ABOUD MWINYI JUMBE



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akikabidhi funguo ya gari kwa wajane wa aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Alhaji Aboud Mwinyi Jumbe, Bi.Zeyana Rashid (kushoto) na Bi. Fatma Mohammed Hassan (kulia) jijini Dar es Salaam.

Mmoja wa Wajane wa aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Alhaji Aboud Mwinyi Jumbe, Bi. Fatma Mohammed Hassan akiwasha gari baada ya kukabidhiwa funguo ya gari hilo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) (hayupo pichani) nyumbani kwa wajane hao jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na  wajane wa aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Alhaji Aboud Mwinyi Jumbe, Bi.Zeyana Rashid (kulia) na Bi. Fatma Mohammed Hassan (kushoto) mara baada ya kuwakabidhi gari la kuwahudumia.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akizungumza na familia ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Mzee Alhaji Aboud Mwinyi alipoitembelea familia hiyo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi.Jane Kajiru (katikati) akizungumza na familia ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Mzee Alhaji Aboud Mwinyi jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment