Sunday, October 28, 2018

SERIKALI YAWAPONGEZA WANUFAIKA WA MIRADI YA MAENDELEO KWA KUTUMIA VIZURI FEDHA ZA MIRADI WANAZOZIPATA KWA KUTEKELEZA SERA YA UCHUMI WA VIWANDA NA KUJIKWAMUA KIUCHUMI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akiangalia moja ya bidhaa iliyotengenezwa na mnufaika wa Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) wa kikundi cha Pamoja, kata ya Gangilonga mkoani Iringa wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani humo yenye lengo la kuzungumza na watumishi wa umma na kutembelea miradi inayotekelezwa na taasisi zilizo chini ya ofisi yake.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akipata maelezo ya bidhaa zilizotengenezwa na wanufaika wa Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) wa kikundi cha Maridadi, kata ya Kihesa mkoani Iringa wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani humo yenye lengo la kuzungumza na watumishi wa umma na kutembelea miradi inayotekelezwa na taasisi zilizo chini ya ofisi yake.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akikabidhi hati ya umiliki wa ardhi kwa mmoja wa wanufaika wa mradi wa MKURABITA, kata ya Igumbilo mkoani Iringa wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani humo yenye lengo la kuzungumza na watumishi wa umma na  kutembelea miradi inayotekelezwa na taasisi zilizo chini ya ofisi yake.
 



No comments:

Post a Comment