Friday, October 19, 2018

WAKUU WA IDARA ZA UTAWALA NA RASILIMALIWATU SERIKALINI WATAKIWA KUWATUMIKIA VIZURI WATUMISHI WA UMMA WANAOWASIMAMIA ILI KUWAJENGEA ARI YA UTENDAJI KAZI


Naibu Katibu Mkuu,  Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,  Bi.Dorothy Mwaluko akizungumza na Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu waliohudhuria kikao kazi kilichofanyika ukumbi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro (katikati mstari wa mbele), akifuatilia moja ya mada zilizowasilishwa katika kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu kilichofanyika ukumbi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma.Kushoto kwake ni  Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi.Dorothy Mwaluko na kuli kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma Bw.Mathew Kirama.

Baadhi ya Wakuu wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu serikalini wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu  Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi.Dorothy Mwaluko (hayupo pichani) wakati akifunga kikao kazi cha watendaji hao  kilichofanyika ukumbi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment