Monday, September 29, 2025

BODI YA TPSC YATAKIWA KUIMARISHA NIDHAMU NA KUHIMIZA UBUNIFU

Na. Veronica Mwafisi na Antonia Mbwambo

Tarehe 29 Septemba, 2025

 Usimamizi bora wa rasilimali, uimarishaji wa nidhamu na uadilifu katika utendaji kazi, kuhimiza ubunifu na kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia ni masuala msingi katika ukuaji wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC)”.

Ujumbe huo umetolewa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi leo tarehe 29 Septemba, 2025 jijini Dar es Salaam wakati akizindua Bodi mpya ya Ushauri ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania.

Aliwaasa Wajumbe wa bodi kutengeneza mazingira ya ushirikiano kati yao, Menejimenti na wadau wote wa chuo ili kuhakikisha mipango ya chuo inatekelezwa kwa ufanisi.

Aidha, Bw. Mkomi aliongeza kwa kuitaka bodi hiyo kutafsiri maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye imejidhatiti kuimarisha uwajibikaji, uwazi, uzalendo na ushirikishwaji katika utendaji wa taasisi zote za umma nchini.

“Ninawaomba mtumie ujuzi, ubunifu na maadili ya Utumishi wa Umma katika kutekeleza majukumu yenu ili kulinda maslahi ya Chuo na Taifa kwa jumla” alisema Bw. Mkomi.

Bw. Mkomi aliongeza kuwa, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora iko tayari kushirikiana na Bodi katika kutekeleza jukumu lake la kusimamia chuo, kutoa dira, mwongozo na ushauri kwa Waziri mwenye dhamana ya Chuo hicho ili kutoa huduma bora.

Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Chuo hicho, Dkt. Florens Turuka aliishukuru Serikali kupitia Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora kwa kuimarisha miundombinu ya chuo na sasa chuo kinatoa elimu katika mazingira salama.

Dkt. Turuka alimshukuru Katibu Mkuu huyo kwa kuzindua bodi na aliahidi kuwa bodi hiyo mpya itatekeleza majukumu waliyopatiwa kwa ufanisi ili kuleta tija kwa chuo na Taifa kwa jumla.

Awali, Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Ernest Francis Mabonesho alisema Chuo hicho kimekuwa kikiwaandaa Watumishi wa Umma kuanzia wanapoajiriwa kwa kuwafanyia Mafunzo ya Awali, Mafunzo Elekezi, Mafunzo ya Umahiri, Mafunzo ya Misingi ya Utumishi wa Umma, Mafunzo ya Uongozi pamoja na Mafunzo ya kuhitimisha Ajira.

Aliongeza kuwa uwepo wa bodi hiyo mpya utaongeza ufanisi na utekelezaji wa majukumu ya chuo kwa kuwa bodi ina jukumu la kutoa ushauri kuhusu shughuli na utekelezaji wa malengo ya chuo, kutoa ushauri katika mipango yote ya maendeleo, kupitisha mpango kazi na bajeti na kupokea na kujadili taarifa ya chuo ya utendaji kazi na fedha.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (hawapo pichani) pamoja na Menejimenti na Wafanyakazi wa Chuo hicho, katika hafla ya Uzinduzi wa Bodi hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa GLS, jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (wa kwanza kushoto) akisalimiana na Viongozi na Watendaji wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania mara baada ya kuwasili katika eneo ulipokuwa unafanyika uzinduzi wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dr. Ernest Mabonesho akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi (hayupo pichani) kuzungumza na Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania pamoja na Menejimenti na Wafanyakazi wa chuo hicho katika hafla ya uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika katika ukumbi wa GLS, jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (katikati) akikata utepe alipokuwa akizindua Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Makao Makuu ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania katika hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania 

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (kulia) akimkabidhi vitendeakazi Mjumbe wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania Bi. Leila Mavika (wa pili kutoka kushoto) katika hafla ya uzinduzi wa bodi hiyo jijini Dar es Salaam.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dr. Ernest Mabonesho (kushoto) kabla ya uzinduzi wa Bodi hiyo jijini Dar es Salaam.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Utumishi wa umma Tanzania katika hafla ya uzinduzi wa bodi hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam.


Wajumbe wa Bodi ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Menejimenti na Wafanyakazi wa chuo hicho wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais- UTUMISHI (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao katika hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo jijini Dae es Salaam.



Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Makao Makuu ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania katika hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Ushauri ya chuo hicho iliyofanyika jijini Dar es Salaam.


Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (kulia) akimkabidhi vitendeakazi mjumbe wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Balozi John Ulanga katika hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo uliofanyika katika ukumbi wa GLS jijini Dar es Salaam.

Menejimenti na Wafanyakazi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao katika hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo jijini Dae es Salaam.

 


WATUMISHI WATAKIWA KUJENGA IMANI KWA WANANCHI

Na. Mwandishi Wetu

“Wananchi wanaimani na utendaji wa Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, hivyo hakuna budi kuilinda imani hiyo kwa kuendelea kutoa huduma bora kwa umma”.

Maneno hayo yamesemwa Bw. Paul Mashauri ambaye ni Mchumi na Mjasiliamali, Septemba 29, 2025 wakati akitoa mafunzo ya namna bora ya kuboresha utendaji wa Watumishi wa umma yaliyofanyika katika Jengo la Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Mtumba Jijini Dodoma.

Aliongeza kuwa, kila mwananchi anatamani kupata huduma bora haraka na kwa wakati, hivyo watumishi wanatakiwa kuwathamini wananchi na kuwapa huduma wanayohitaji ndani ya muda mfupi ili kuongeza imani kwa Serikali.

“Ni kazi ya Watumishi wa Umma kutafsiri Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kwa kutoa huduma bora kwa wananchi. Wananchi hawawezi kusoma nyaraka za mipango ya maendeleo ya nchi kwa upana wake isipokuwa ni jukumu la watumishi na wananchi wanataka kuona huduma bora tu” alifafanua Bw. Mashauri.

Kwa upande mwingine, Mtaalamu wa Epidemiolojia sehemu ya Magonjwa Yasiyoambukiza kutoka Wizara ya Afya Bw.Jofrey Mtewele aliwataka watumishi hao kuepuka visababishi na kuwa makini na magonjwa yasiyoambukiza kwa kuwa hapa Tanzania yanachangia vifo kwa asilimia 33.

Bw. Mtewele alitaja baadhi ya magonjwa hayo kuwa ni saratani, kisukari, ugonjwa wa mifumo ya upumuaji, moyo na mishipa ya damu.

Naye, Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw. Syrus Kapinga amewashukuru wawezeshaji hao Bw. Mashauri na Bw. Mtewele kwa kutoa mafunzo muafaka kwa watumishi wa ofisi hiyo na kuwaahidi kutekeleza kwa vitendo mafunzo hayo.

Aidha, Bw. Kapinga ametoa rai kwa watumishi wote kufanya uchunguzi wa afya zao mara kwa mara kwa kuwa magonjwa yaliyotajwa na wataalamu yapo na yanaweza kutibika.

Vilevile, Bw. Kapinga ametumia fursa hiyo kuwapongeza watumishi wa ofisi yake waliozaliwa mwezi Septemba na kuwatakia kila kheri katika maisha yao.

Wakurugenzi na Watumishi wa Ofisi ya Rais - UTUMISHI wakifuatilia mada zilizowasilishwa na Wawezeshaji Bw. Paul Mashauri na Bw.Jofrey Mtewele (Hawapo pichani) kuhusu  namna ya kuboresha utendaji wa watumishi na magonjwa yasiyoambukiza mtawalia yaliyofanyika katika Jengo la Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Mtumba Jijini Dodoma, Septemba 29, 2025.





Wakurugenzi na Watumishi wa Ofisi ya Rais - UTUMISHI wakifuatilia mada zilizowasilishwa na Wawezeshaji Bw. Paul Mashauri na Bw.Jofrey Mtewele (Hawapo pichani) kuhusu  namna ya kuboresha utendaji wa watumishi na magonjwa yasiyoambukiza mtawalia yaliyofanyika katika Jengo la Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Mtumba Jijini Dodoma, Septemba 29, 2025.

Mchumi na Mjasiliamali Bw. Paul Mashauri akiwasilisha mada kuhusu  namna ya kuboresha utendaji wa watumishi wakati wa mafunzo ya kuwajengea uelewa watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI,. Mafunzo yamefanyika katika Jengo la  Utumishi Mtumba Jijini Dodoma, Septemba 29, 2025.



Mtaalamu wa Epidemiolojia sehemu ya Magonjwa Yasiyoambukiza kutoka Wizara ya Afya Bw.Jofrey Mtewele akiwasilisha mada kuhusu  namna ya kuepuka Magonjwa hayo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uelewa watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI. Mafunzo yamefanyika katika Jengo la  Utumishi Mtumba-Dodoma, Septemba 29, 2025.

Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakifuatilia mada mbalimbali
 
Bi. Hulay Mpamka akiandaa keki kwa niamba ya watumishi wa Ofisi ya Rais UTUMISHI waliozaliwa Mwezi Septemba.


Kaimu Katibu Mkuu Bw. Syrus Kapinga akichukua kipande cha keki tayari kwa ajili ya kuwalisha watumishi waliozaliwa Mwezi Septemba.

 Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais UTUMISHI Bw. Syrus Kapinga akimlisha keki Bi. Geva Mbughi ambaye anasherehekea siku ya kuzaliwa kwake.
 Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais UTUMISHI Bw. Syrus Kapinga akimlisha keki Bi. Hulay Mpamka ambaye anasherehekea siku yake ya kuzaliwa.
 Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais UTUMISHI Bw. Syrus Kapinga akimlisha keki Bw. Imani Mtumbi ambaye anasherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais UTUMISHI Bw. Syrus Kapinga akimlisha keki Bw. Innocent Kessy  ambaye anasherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais UTUMISHI Bw. Syrus Kapinga akitoa nasaha kwa watumishi wa ofisi yake wanaoadhimisha siku ya kuzaliwa kwao mwezi septemba.

Keki Maalum kwa ajili ya Watumishi wa Ofisi ya Rais UTUMISHI wanaoadhimisha siku yao ya kuzaliwa mwezi Septemba.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais UTUMISHI Bw. Syrus Kapinga akimlisha keki Bw. Kelvin Munubi ambaye anasherehekea siku yake ya kuzaliwa.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais UTUMISHI Bw. Syrus Kapinga akimlisha keki Bw. Lusanda Kokolo ambaye anasherehekea siku yake ya kuzaliwa.
Watumishi wa Ofisi ya Rais UTUMISHI wakianda Keki Maalumu kwa ajili ya Watumishi wa Ofisi hiyo waliozaliwa mwezi Septemba.

 


Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais UTUMISHI Bw. Syrus Kapinga akimlisha keki Bi. Mariana Kihaya ambaye anasherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais UTUMISHI Bw. Syrus Kapinga akimlisha keki Bw. Rashid Shedafa ambaye anasherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais UTUMISHI Bw. Syrus Kapinga akimlisha keki Bw. Sospeter Tundura ambaye anasherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais UTUMISHI Bw. Syrus Kapinga akimlisha keki Bw. Ally Ngowo ambaye anasherehekea siku yake ya kuzaliwa.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais UTUMISHI Bw. Syrus Kapinga akimlisha keki Bi.Aveline Ilahuka ambaye anasherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais UTUMISHI Bw. Syrus Kapinga akimlisha keki Bi. Zulfa Makaso ambaye anasherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais UTUMISHI Bw. Syrus Kapinga akilishwa Keki Bi. Aveline Ilahuka kwa niaba ya watumishi wote waliozaliwa Mwezi Septemba kama ishara ya upendo.

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais UTUMISHI Bw. Syrus Kapinga akilishwa Keki Bw.Paul Mashauri kwa niaba ya Wawezeshaji ikiwa ni ishara ya upendo wa watumishi wote wa ofisi hiyo waliozaliwa Mwezi Septemba.
Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakifuatilia hafla fupi ya kulishwa keki kwa watumishi wa ofisi hiyo waliozaliwa Mwezi Septemba.

Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakifuatilia hafla fupi ya kulishwa keki kwa watumishi wa ofisi hiyo waliozaliwa Mwezi Septemba.

Wawezeshaji Bw. Paul Mashauri ambaye ni Mchumi na Mjasiliamali (Kulia) na Mtaalamu wa Epidemiolojia sehemu ya Magonjwa Yasiyoambukiza kutoka Wizara ya Afya Bw. Jofrey Mtewele wakifuatilia hafla fupi ya kuwapongeza watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI waliozaliwa mwezi Septemba, iliyofanyika katika Jengo la hiyo, Mtumba Dodoma, Septemba 29, 2025.

Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bi. Mwalibora Saidy (Wa Nne kutoka Kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Ofisi hiyo waliozaliwa mwezi Septemba, Septemba 29, 2025.


Thursday, September 25, 2025

KATIBU MKUU MKOMI APOKEA MAKOMBE YA USHINDI MASHINDANO YA SHIMIWI 2025 ASISITIZA UMUHIMU WA MICHEZO KWA WATUMISHI WA UMMA

Na Eric Amani na Antonia Mbwambo, Mtumba Dodoma

Tarehe 24.09.2025

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi, leo Septemba 24, 2025 amepokea makombe ya ushindi yaliyonyakuliwa na timu ya OfisI yake katika Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) 2025, yaliyofanyika jijini Mwanza huku akisisitiza umuhimu wa michezo kwa Watumishi wa Umma nchini.

Akizungumza katika hafla fupi iliyofanyika sehemu ya wazi ya Ofisi hiyo, Katibu Mkuu Bw. Mkomi amezipongeza timu zote zilizoshiriki katika mashindano hayo ya SHIMIWI jijini Mwanza kwa juhudi na uzalendo waliouonesha hadi kuibuka mabingwa katika michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu (wanaume) mabingwa nafasi ya kwanza, netiboli (wanawake) nafasi ya tatu, mbio za baiskeli na mchezo wa “darts” walipata ushindi wa nafasi ya tatu kwa jumla, aidha kwenye mbio za kupokeza mita 400 (Relay) mshindi wa kwanza kwa wanawake na wa pili kwa wanaume.

Bw. Mkomi amesema ushindi huo ni ishara ya mshikamano, nidhamu na mazoezi ya muda mrefu ya timu nzima. Amesisitiza kuwa michezo si tu burudani, bali pia ni nyenzo muhimu ya kuimarisha afya, mahusiano kazini na kuongeza ufanisi wa kazi.

“Michezo ni afya, hivyo ninawahimiza Watumishi wa Umma msiache kushiriki michezo kwani afya zenu zikiwa nzuri basi huduma zinatolewa kikamilifu kwa wananchi.” Amesisitiza na kuongeza kuwa pamoja na kuimarisha afya, pia inaleta ushirikiano.

Amesema Ofisi yake imeweka utaratibu wa watumishi kufanya mazoezi kila siku ya Jumanne na Alhamisi, hivyo amewasisitiza watumishi hao kushiriki kikamilifu.

“Utaratibu wa kufanya mazoezi kila Jumanne na Alhamisi tumeuweka makusudi ili kila mmoja ashiriki, hivyo ukifika muda uliopangwa wa kuanza mazoezi wote tunatakiwa kuelekea kwenye mazoezi,” ameongeza.

Pamoja na kuhimiza kushiriki michezo, Katibu Mkuu Mkomi amewataka Watumishi wa Umma kujiepusha na tabia zinazoharibu taswira ya Ofisi. “Haipendezi kuona mtumishi wa umma anafanya mambo ya ajabu huko mtaani, sisi ni kioo, hivyo tunatakiwa kuwa mfano wa kuigwa katika kuzingatia maadili ndani na nje ya ofisi," amesema.

Naye Kiongozi wa timu ya UTUMISHI ambaye ni Afisa Tawala Mwandamizi wa Ofisi hiyo, Bw. Charles Shija kwa niaba ya wanamichezo wote, alimshukuru Katibu Mkuu kwa kuwawezesha kushiriki michezo hiyo na kupata ushindi.

Aidha, Bw. Shija pamoja na wanamichezo hao walitumia fursa hiyo kumkabidhi Katibu Mkuu makombe hayo huku wakiahidi kuendelea kujiimarisha zaidi katika michezo kwa ustawi wa taifa.

 

 


 

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi akitoa hotuba fupi kwa watumishi wa Ofisi hiyo katika hafla fupi ya kupokea Makombe ya ushindi wa timu za Ofisi hiyo walioshiriki katika Shirikisho la Michezo ya Wizara, Idara na Wakala wa Serikali, (SHIMIWI) lililofanyika jijini

Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi (wanne kutoka kushoto) akipokea kombe la mchezo wa Darts” kutoka kwa Mtumishi wa ofisi hiyo, Bi Loveness Choga (watatu kutoka kulia) wakati wa hafla fupi ya kupokea makombe hayo yaliyopatikana wakati wa mashindano ya michezo ya SHIMIWI.

Mwenyekiti wa Timu za Michezo mbalimbali kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Charles Shija akitoa maneno ya utangulizi kwa Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Bw. Juma Mkomi (hayupo pichani) kuhusu ushindi walioupata katika  mashindano ya SHIMIWI.

Watumishi wa Ofisi ya Rais, UTUMISHI wakiwa nje ya ofisi hiyo tayari kwa kupokea Makombe ya ushindi kutoka kwa washiriki wa mpira wa miguu, mpira wa pete, riadha ya mbio za kupokezana, darts na mchezo wa baiskeli waliyoyapata katika mashindano ya SHIMIWI yaliyofanyika jijini Mwanza. 


Washiriki wa Shirikisho la Michezo ya Wizara, Idara na Wakala wa Serikali, SHIMIWI kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwa wanafurahia Ushindi walioutwaa katika mashindano hayo baada ya kuwasili katika Ofisi hiyo iliyopo Mtumba jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Timu mbalimbali za Michezo kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Charles Shija akikabidhi Kombe la Ubingwa wa Mpira wa Miguu kwa Mgeni Rasmi ambaye ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Bw. Juma Mkomi wakati wa hafla fupi iliyofanyika jijini Dodoma

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi (aliyenyanyua kombe) akifurahia ushindi walioupata Watumishi wanamichezo wa ofisi hiyo kwenye mashindano ya michezo ya SHIMIWI.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi akifurahia pamoja na Wakurugenzi wa Idara na Vitengo, Watumishi na timu ya michezo ya ofisi hiyo ushindi wa makombe waliyoyapata kwenye mashindano ya michezo ya SHIMIWI.

Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi (katikati mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa Idara na Vitengo kutoka katika ofisi hiyo na timu ya washiriki wa michezo ya SHIMIWI mara baada kupokea makombe ya ushindi ya mashindano ya michezo ya SHIMIWI.

Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi (watano kutoka kulia) akipokea kombe la mchezo wa Baiskeli kutoka kwa Mtumishi wa Ofisi hiyo, Bw. Hassan Ligoneko (wasita kutoka kulia) wakati wa hafla fupi ya kupokea makombe ya ushindi ya mashindano ya michezo ya SHIMIWI.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi akiwa ameongozana na baadhi ya Wakurugenzi wa Ofisi hiyo mara baada ya kupokea makombe ya ushindi ya mashindano ya michezo ya SHIMIWI.

Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakionyesha makombe ya ushindi kwa Katibu Mkuu wa ofisi hiyo Bw. Juma Mkomi (hayupo pichani) waliyoyapata katika mashindano ya michezo ya SHIMIWI.

 Watumishi wa Ofisi ya Rais, UTUMISHI wakiwa nje ya ofisi hiyo tayari kwa kupokea Makombe ya ushindi kutoka kwa washiriki wa mpira wa miguu, mpira wa pete, riadha ya mbio za kupokezana, darts na mchezo wa baiskeli waliyoyapata katika mashindano ya SHIMIWI yaliyofanyika jijini Mwanza. 

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi (kulia) akiwa anateta jambo na Mkurugenzi Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Bw. Musa Magufuli (kushoto) wakati wa hafla fupi ya kupokea makombe ya ushindi walioupata katika michezo ya SHIMIWI.

Mlezi wa Timu za michezo mbalimbali kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi Mwanadawa Nchemwa (watano kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi ambaye ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Juma Mkomi (watatu kutoka kushoto) baada ya kukabidhi Kombe la Ushindi uliotokana na mchezo wa netiboli wakati wakati wa mashindano ya SHIMIWI.