Saturday, March 29, 2025

WAZIRI SIMBACHAWENE AELEKEZA NAMNA BORA ZAIDI YA KUSHUGHULIKIA MASUALA YA KIUTUMISHI IKIWEMO BARUA ZA AJIRA MPYA

 

 

Na. Mwandishi Wetu- Dodoma

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amemuelekeza Katibu Mkuu, UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi kuhakikisha barua za walioshinda usaili na kupangiwa vituo vya kazi zinatolewa kwenye mikoa husika walikofanyia usaili badala ya kuwalazimu kusafiri hadi jijini Dodoma Sekretarieti ya Ajira kufuata barua hizo.

 

Amesema kitendo cha watumishi hao wapya kupatiwa barua katika mikoa husika kitasaidia kupunguza gharama, usumbufu pamoja na muda wanaoutumia kufika hadi Dodoma.

 

Mhe. Simbachawene ametoa maelekezo hayo leo jijini Dodoma wakati akizinda Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

 

Mhe. Simbachawene amefafanua kuwa unaweza ukakuta mwananchi amefaulu usaili Mkoa wa Kigoma anaifuata barua jijini Dodoma halafu pengine kapangiwa tena Mkoa huo huo wa Kigoma au Lindi.

 

Mhe. Simbachawene amesema hayo ni matumizi mabaya ya rasilimali za nchi, ikiwemo mwananchi mwenyewe pamoja na fedha anazotumia.

 

“Hii si sawa kwani tunawasumbua wanachoka hata kabla ya kuanza kazi, tuwahurumie, barua hizo wachukulie kwenye mikoa walikofanyia usaili, tuwaamini Makatibu Tawala wetu, tunaamini wapo wataalam wenye maadili wa kufanya kazi hiyo, hivyo tuwape  dhamana waifanye, Mhe. Simbachawene amesisitiza.

 

Amesema anatamani kuona kwa mfano mwananchi aliyefanyia usaili katika Mkoa wa Rukwa anaifuata barua yake katika Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa kisha  anakwenda pengine  Kigoma alikopangiwa kazi na sio kwenda Dodoma kwanza.

Katika hatua nyingine, Mhe. Simbachawene amemuelekeza Katibu Mkuu, UTUMISHI, kuandaa kituo cha pamoja (One Stop Centre) katika ofisi hiyo kwa lengo la kusikiliza changamoto zinazowakabili Watumishi wa Umma, ikiwa ni ubunifu wa kuzitafutia ufumbuzi changamoto hizo  papo kwa hapo kwa Watumishi wenye changamoto za kiutumishi wanaofika Ofisi ya Rais, UTUMISHI na Utawala Bora zilizopo Mtumba jijini Dodoma.

 

Amesema Kituo hicho kinatakiwa kiwe na Maafisa Waandamizi wa kila kada ikiwemo wanasaikolojia nguli watakaohakikisha mtumishi yeyote mwenye changamoto za kitumishi anayefika katika Kituo hicho anapata ufumbuzi wa changamoto yake inayomkabili papo kwa hapo.

 

Amefafanua kuwa, kituo hicho kitakuwa na mawasiliano ya waajiriwa wote nchini hivyo mtumishi hatalazimika kurudi tena mkoani kwake kurekebisha taarifa zake badala yake suluhu zote za changamoto alizo nazo  zitapatikana hapo.

 

Amesema hali hiyo itapunguza msururu wa Watumishi wanaotoka maeneo mbalimbali nchini ambapo kila mmoja akifika Ofisini hapo  anataka kumuona na Waziri au Katibu Mkuu.

 

Kwa upande wake, Katibu Mkuu, UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi ametumia fursa hiyo kumshukuru Waziri Simbachawene kwa maelekezo aliyoyatoa na kwa ubunifu huo huku akimuahidi kuyatekeleza kikamilifu.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Mhe. George Simbachawene akizungumza wakati wa Mkutano Maalum wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora uliofanyika katika ukumbi wa Kambarage uliopo Hazina jijini Dodoma.

Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza katika Mkutano Maalum wa Baraza hilo uliofanyika ukumbi wa Kambarage uliopo Hazina jijini Dodoma.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora akiongoza Mkutano Maalum wa Baraza la Wafanyakazi la ofisi hiyo kabla ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Mhe. George Simbachawene kuzindua Baraza hilo.

Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza katika Mkutano Maalum wa Baraza hilo uliofanyika katika ukumbi wa Kambarage uliopo Hazina jijini Dodoma.

Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza katika Mkutano Maalum wa Baraza hilo uliofanyika katika ukumbi wa Kambarage uliopo Hazina jijini Dodoma.

Katibu Mstaafu wa Baraza la Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Rocky Setembo akitoa neno la shukrani baada ya kumaliza muda wake katika kulitumikia Baraza hilo kwenye Mkutano Maalum wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora uliofanyika katika ukumbi wa Kambarage uliopo Hazina jijini Dodoma.

Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza Mkutano Maalum wa Baraza hilo uliofanyika katika ukumbi wa Kambarage uliopo Hazina jijini Dodoma.

Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza katika Mkutano Maalum wa Baraza hilo uliofanyika katika ukumbi wa Kambarage uliopo Hazina jijini Dodoma.

Sehemu ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza katika Mkutano Maalum wa Baraza hilo uliofanyika katika ukumbi wa Kambarage uliopo Hazina jijini Dodoma. Wa kwanza kushoto ni Mwakilishi wa TUGHE Mkoa, Bw. Nsubisi Mwasandende.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Mhe. George Simbachawene (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora mara baada ya kuzindua Mkutano Maalum wa Baraza hilo uliofanyika katika ukumbi wa Kambarage uliopo Hazina jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Mhe. George Simbachawene (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora mara baada ya kuzindua Mkutano Maalum wa Baraza hilo uliofanyika katika ukumbi wa Kambarage uliopo Hazina jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Mhe. George Simbachawene (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja Viongozi wapya akiwemo Katibu wa Baraza la Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Mwendesha Mkandya na Katibu Msaidizi, Bi. Catherine Massawe (kulia waliosimama) mara baada ya kuzindua Mkutano Maalum wa Baraza hilo uliofanyika katika ukumbi wa Kambarage uliopo Hazina jijini Dodoma.


Thursday, March 27, 2025

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA KATIBA NA SHERIA YAPITISHA MPANGO NA BAJETI YA OFISI YA RAIS-UTUMISHI NA TAASISI ZAKE KWA MWAKA WA FEDHA 2025/26

Na. Veronica Mwafisi-Dodoma

Tarehe 27 Machi, 2025.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imepitisha Mpango na Bajeti ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora pamoja na taasisi zake kwa Mwaka wa fedha 2025/26 baada ya kupitia mafungu yote yaliyo chini ya ofisi hiyo na kujiridhisha.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Florent Kyombo amezungumza hayo leo tarehe 27 Machi, 2025 katika Ukumbi wa Mikutano wa Bunge jijini Dodoma alipokuwa akikaimu nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo mara baada ya Wajumbe wa Kamati kujadili na kuridhia taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26 ya Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora.

“Kamati imejadili na kuridhia kupitisha Mpango na Bajeti ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora pamoja na taasisi zake kwa Mwaka wa fedha 2025/26, niwapongeze kwa maandalizi mazuri yenye uwazi, Kamati inawaasa kuwa na matumizi mazuri ya fedha pale zitakapopitishwa katika vikao vya Bunge la Bajeti ambapo tunaamini mtafikia malengo ya kuwatumikia watanzania kwa maendeleo ya nchi.” Mhe. Kyombo amesema.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ameishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, kwa kuwa na majadiliano mazuri na ofisi anayoiongoza ambayo wanaamini yatawasaidia kwa kiasi kikubwa katika utekelezaji wa majukumu yao kupitia bajeti hiyo.

“Mhe. Mwenyekiti, nitoe shukrani za dhati kwa niaba ya ofisi ninayoiongoza mara zote tumepokea maoni, ushauri na michango mbalimbali kutoka katika Kamati yako inayolenga kuboresha Utumishi wa Umma nchini kwa lengo la kutimiza azma ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwa na Utumishi wa Umma uliotukuka.

Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya ofisi hiyo, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi amesema Kamati hiyo imekuwa msaada mkubwa wa kuiongoza Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora kwa kuwapatia maarifa mengi kutoka kwa Wajumbe wote wa Kamati hiyo yenye kuboresha utendajikazi.

Mpango na Bajeti ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na taasisi zake kwa Mwaka wa fedha 2025/26 umezingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025, Maelekezo ya Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 na Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo  wa Miaka Mitano (2021/22-2025/26).

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Florent Kyombo akiongoza kikao kazi cha kamati yake na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kiliyolenga kupokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria.

Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Utawala, Katiba na Sheria wakifuatilia taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26 iliyokuwa ikiwasilishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika Ofisi za Bunge jijini Dodoma.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akifafanua baadhi ya hoja zilizowasilishwa na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao kazi kilicholenga kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26.

Sehemu ya Watendaji wa Taasisi zilizopo chini ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwa katika kikao kazi cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26.


Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Mhe. Abeid Ramadhani (katikati) akiwasilisha hoja kwa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakati wa kikao kazi cha Kamati na ofisi hiyo kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26.

Sehemu ya Wakurugenzi na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwa katika kikao kazi cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, na Watendaji wa ofisi hiyo kiliyolenga kupokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (kulia) akiteta jambo na Katibu Mkuu wa ofisi yake Bw. Juma Mkomi (kushoto) wakati wa kikao kazi cha kuwasilisha kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26. 

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Mick Kiliba akijibu hoja kuhusu ajira iliyowasilishwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na taasisi zake kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26.

Sehemu ya Wakurugenzi na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakifuatilia maoni yaliyokuwa yakitolewa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kazi cha Kamati na ofisi hiyo kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26.


Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Florent Kyombo (kushoto) akisikiliza fafanuzi za hoja mbalimbali zilizotolewa na wajumbe wa Kamati yake kwa Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakati wa kikao kazi kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26. Kulia kwake ni katibu wa Kamati hiyo, Bi. Ganjatuni Abel.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi akitoa neno la shukrani kwa  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria mara baada ya kumaliza kikao kazi cha Kamati na Watendaji wa ofisi hiyo kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26.

Sehemu ya Maafisa na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwa katika kikao kazi cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, na Watendaji wa ofisi hiyo kiliyolenga kupokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26.

Sehemu ya Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwa katika kikao kazi cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, na Watendaji wa ofisi hiyo kiliyolenga kupokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26.








 

 

Wednesday, March 26, 2025

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA KATIBA NA SHERIA YAIPONGEZA OFISI YA RAIS-UTUMISHI NA TAASISI ZAKE KWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE KIKAMILIFU

Na. Veronica Mwafisi-Dodoma

Tarehe 26 Machi, 2025.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imeipongeza Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora pamoja na taasisi zake kwa kutekeleza majukumu yake kikamilifu kwa kuishirikisha Kamati hiyo na kutoa uelewa mpana kuhusu shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na ofisi hiyo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama ametoa pongezi hizo leo jijini Dodoma kwa niaba ya kamati yake wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26.

“Kamati inatoa pongezi nyingi kwa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora pamoja na taasisi zake kwa kutekeleza majukumu yake kikamilifu jambo linalodhihirisha kuwa mnaendana na maono ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwa na Serikali inayotekeleza majukumu yake kikamilifu kwa maendeleo ya nchi.” Mhe. Mhagama amesema.

Mhe Mhagama ameitaka Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora pamoja na taasisi zake kuendelea kushirikiana katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali ili kuleta tija na manufaa nchini yatakayokidhi mahitaji na viwango vikubwa katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ameishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, kwa kutoa ushauri, maoni na miongozo mbalimbali ambayo ofisi yake imekuwa ikiifanyia kazi na kwa asilimia kubwa imeisaidia ofisi hiyo kutekeleza majukumu yake kikamilifu.

“Mhe. Mwenyekiti, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora inajivunia kusimamiwa na Kamati yako kwani mmekuwa mkitupatia ushauri, maoni na miongozo mbalimbali ambayo yameleta tija kwetu na kutufanya tutekeleze majukumu yetu kikamilifu na kwa ufanisi mkubwa sana.” Mhe. Simbachawene amesema.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria itapokea taarifa ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora pamoja na taasisi zake kwa siku mbili tarehe 26 na 27 Machi, 2025 kwa lengo la kujadili Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama akizungumza wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kiliyolenga kupokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama akiongoza kikao kazi cha kamati yake na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kiliyolenga kupokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw. Juma Mkomi (wa kwanza kulia) akimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama wakati kamati hiyo ilipokuwa ikipokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26. Kulia kwake ni Katibu Mkuu-IKULU, Bw. Mululi Mahendeka, wa tatu kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi.


Sehemu ya Wakurugenzi na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwa katika kikao kazi cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, na Watendaji wa ofisi hiyo kiliyolenga kupokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26.


Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Bw. Shedrack Mziray akitoa ufafanuzi wa hoja iliyowasilishwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na taasisi zake kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26.


Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Yahya Massare (aliyevaa shati la bluu) akiwasilisha hoja kwa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na ofisi hiyo kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26.


Sehemu ya Wakurugenzi na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwa katika kikao kazi cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, na Watendaji wa ofisi hiyo kiliyolenga kupokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria (mstari wa mbele) wakisikiliza fafanuzi mbalimbali za hoja zilizotolewa wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26.


Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Oscar Kikoyo (katikati) akiwasilisha hoja kwa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na ofisi hiyo kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26.


Sehemu ya Wakurugenzi na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwa katika kikao kazi cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, na Watendaji wa ofisi hiyo kiliyolenga kupokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26.


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Investments (WHI), Arch. Sephania Solomon akijibu hoja ya taasisi anayoisimamia kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na taasisi zake kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Mapango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26.