Na. Lusungu Helela-Dar es Salaam
Naibu Waziri Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema kitendo cha Sekretarieti ya Ajira
katika Utumishi wa Umma kuanza kutumia rasmi mfumo wa usaili wa kidigitali unaomuwezesha
mwombaji kusailiwa eneo alilopo badala ya kusafiri umbali
mrefu, ili kupunguza gharama kwa Serikali na kwa wanaosailiwa ni
mafanikio makubwa ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Uongozi wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kukuza
uwazi kwenye mchakato wa kutoa ajira.
Mhe. Kikwete ametoa kauli hiyo jana
Jijini Dar es Salaam mara baada ya
kushuhudia wasailiwa wa kada ya
Tehama wakifanya usaili huo katika Chuo
Kikuu cha St. Joseph , ikiwa ni moja ya kituo cha usaili wa mchujo unaofanyika kidigitali
katika kila Mkoa Nchi nzima, ikiwa ni usaili wa kwanza tangu mfumo huo
ulipozinduliwa hivi karibuni
Amesema mfumo huo
umeanza kutumika wakati sahihi ambapo Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
anaendelea na jitihada za kuimarisha uwazi na kuepuka upendeleo katika suala
zima la utoaji ajira serikalini.
Amesema vituo vipatavyo 32 nchi nzima
leo vimeendesha usaili huo ambapo jumla
ya wasailiwa 2325 wamepata fursa ya kufanya usaili huo pasipo kulazimika kusafiri umbali mrefu
Amefafanua kuwa vituo
32 kulikofanyika usaili huo kunajumuisha Tanzania Bara na Visiwani ambapo kwa
Mkoa wa Dar es Salaam kulikuwa na vituo vinne kutokana na idadi kubwa ya
wasailiwa waliokuwa wameomba .
Mhe.Kikwete amesema suala
la ajira ni maisha ya watu, hivyo mchakato huo leo umefungua ukurasa mpya
wa kukuza uwazi na
uadilifu katika kuondoa
manung'uniko kwa wale ambao wanatafuta ajira serikalini.
Amesema mfumo huo mbali ya kusaidia
kupunguza gharama za wasailiwa ambao walikuwa wanalalamika
kusafiri umbali mrefu kwenda kwenye kituo cha usaili kwa kutumia
muda mwingi na gharama kubwa, ila
leo hii wamesailiwa mahali
walipo na kisha kuendelea kufanya shughuli zingine za
kujiingizia kipato.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara
ya Tehama kutoka Sekretariet ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Mhandisi Samweli
Tanguye amesema mfumo huo mara
baada ya wasailiwa hao kumaliza kufanya mchujo watapata matokeo yao leo tofauti
na ilivyokuwa mwanzo ambapo matokeo hayo yalikuwa yakichukua zaidi ya siku tatu
kutoka.
Amesema mfumo huu unatoa nafasi
kwa Wasailiwa ambao wanafanya usaili zaidi ya mmoja ndani ya siku moja kuwa
wigo wa kufanya usaili mwingine siku hiyo hiyo kwa saa tofauti ambapo awali
haikuwa rahisi.
Kwa upande wake Juma Ali,
Msailiwa wa kada ya Tehama amepongeza ujio wa mfumo huo wa usaili wa kidijitali
huku akisema licha ya kumpunguzia gharama ya kusafiri hadi Jijini Dodoma
lakini amepata fursa ya kuendelea
kufanya shughuli zingine mara baada ya kumaliza usaili wake
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete
akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kushuhudia wasailiwa wa kada ya Tehama wakiwa katika Chuo Kikuu cha St. Joseph, ikiwa ni
moja ya kituo cha usaili wakifanya usaili huo wa mchujo unaofanyika kidigitali katika kila Mkoa, nchi nzima,
ikiwa ni usaili wa kwanza tangu mfumo huo ulipozinduliwa hivi karibuni
Naibu Waziri Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani
Kikwete akishuhudia wasailiwa wa kada ya Tehama wakiendelea na
usaili katika Chuo Kikuu cha St. Joseph
ikiwa ni moja ya kituo cha usaili wakifanya usaili huo wa mchujo
unaofanyika kidigitali katika kila Mkoa,
Nchi nzima, ikiwa ni usaili wa kwanza tangu mfumo huo ulipozinduliwa hivi
karibuni
Baadhi ya wasailiwa wa kada ya Tehama wakiendelea na usaili katika
Chuo Kikuu cha St. Joseph ikiwa ni moja ya kituo cha usaili wakifanya
usaili huo wa mchujo unaofanyika
kidigitali katika kila Mkoa, Nchi nzima, ikiwa ni usaili wa kwanza tangu
mfumo huo ulipozinduliwa hivi karibuni
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete
akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Wajumbe wa timu ya Menejimenti
ya Chuo Kikuu cha St. Joseph, ikiwa ni
moja ya kituo cha usaili wakifanya usaili huo wa mchujo unaofanyika kidigitali katika kila Mkoa, Nchi nzima,
ikiwa ni usaili wa kwanza tangu mfumo huo ulipozinduliwa hivi karibuni
Muonekano wa moja ya jengo la Chuo Kikuu cha St. Joseph, kiwa ni moja ya kituo cha usaili wa kada ya Tehama ambapo leo baadhi ya wasailiwa wameafanya usaili huo wa mchujo unaofanyika kidigitali katika kila Mkoa, Nchi nzima, ikiwa ni usaili wa kwanza tangu mfumo huo ulipozinduliwa hivi karibuni
No comments:
Post a Comment