Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kipindi cha Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imefanikiwa kuweka utaratibu wa mgao wa ajira unaotekelezwa kwa mujibu wa Waraka wa Serikali wa tarehe 10 Mei, 2013 ambapo Tanzania Bara ni asilimia 79 na Tanzania Zanzibar ni asilimia 21.
Ameyasema hayo leo Aprili 15, 2024 jijini Dodoma, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya miaka 60 ya Muungano kwa upande wa Ofisi yake.
Aidha,
matumizi ya mifumo ya TEHAMA katika kipindi hiki cha miaka 60 ya Muungano imesaidia
waombaji kuepuka gharama za usafiri, malazi na changamoto za ajali, wakati Serikali
imepunguza muda wa usaili na gharama za uendeshaji wa zoezi hilo.
Mhe.
Simbachawene amewataka watafuta fursa za ajira wote kutoka pande mbili za
Muungano kufahamu akaunti zao, nywila na kuwa mahiri katika matumizi ya kompyuta
ili kuepukana na usumbufu.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Maelezo, Bi. Zamaradi Kawawa akitoa neon la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kuzungumza na Waandishi wa Habari kuhusu mafanikio ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanzania kwenye eneo la Utumishi wa Umma na Utawala bora leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (katikati) akiwa na baadhi ya Wakurugenzi baada ya kuzungumza na Waandishi wa Habari kuhusu mafanikio ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanzania kwenye eneo la Utumishi wa Umma na Utawala bora, wa kwanza kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Mary Mwakapenda
Baadhi ya Watumishi kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) wakimsiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu mafanikio ya Miaka 60 ya Muungano kwenye eneo la Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
No comments:
Post a Comment