Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wameungana na Wafanyakazi Duniani kote leo Mei Mosi, 2024 kuadhimisha siku yao Adhimu ambapo nchini Tanzania, Kilele cha Siku hiyo Kitaifa imefanyika jijini Arusha na Mgeni Rasmi wa Sherehe hizo ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango.
Kaulimbiu ya siku hii ya Wafanyakazi Duniani kwa mwaka
huu ni “Nyongeza ya Mishahara ni Msingi wa Mafao Bora na Kinga Dhidi ya Hali
Ngumu ya Maisha”
Aidha, kwa upande wa Utumishi wa Umma ulibeba kaulimbiu isemayo “Utumishi wa Umma Ulioboreshwa ni Chachu ya Utendaji Kazi Unaozingatia Haki na Wajibu”.
Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Mgeni Rasmi ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma
Mhe. Rosemary Senyamule (hayupo pichani) wakati wa maadhimisho
ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) 2024 iliyofanyika kimkoa katika
Viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma.
Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwa katika maandamano ya Maadhimisho ya
Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) 2024 yaliyofanyika katika ngazi ya mkoa
jijini Dodoma.
Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwa katika maandamano ya Maadhimisho ya
Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) 2024 yaliyofanyika katika ngazi ya mkoa
jijini Dodoma.
Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakipita mbele ya Mgeni Rasmi ambaye pia ni
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule (hayupo pichani) wakati wa
Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) 2024 yaliyoadhimishwa
kimkoa katika Viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment