Saturday, October 28, 2023
Friday, October 27, 2023
OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAIDHINISHA VIBALI 930 VYA AJIRA MPYA KWA KADA YA WATUNZA KUMBUKUMBU NA NYARAKA KATIKA MWAKA WA FEDHA 2023/24
Na. Veronica Mwafisi-Dodoma
Tarehe 27 Oktoba, 2023
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, imeidhinisha jumla ya nafasi 930 za ajira mpya za kada ya Watunza Kumbukumbu na Nyaraka katika mwaka wa fedha 2023/24 na kutoa nafasi 443 za ajira mpya kwa kada hiyo katika mwaka wa fedha 2022/23.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa kufungua Mkutano Mkuu wa 11 wa wanachama wa Chama cha Menejimenti ya Watunza Kumbukumbu na Nyaraka (TRAMPA) jijini Dodoma.
Mhe. Simbachawene amesema, uidhinishaji wa vibali hivyo vya ajira mpya unaonyesha ni kwa jinsi gani Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inatambua na kuthamini utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka kwa ustawi wa taifa.
Ameongeza kuwa, kwa kutambua mchango wa kada hii katika ustawi wa Utumishi wa Umma, jumla ya Watunza Kumbukumbu 649 waliokasimiwa katika Ikama na Bajeti ya mwaka 2022/23 wameshapandishwa vyeo na kuidhinishiwa mishahara ya vyeo vipya mwezi Juni, 2023.
Katika kushughulikia changamoto za kiutumishi kwa kada hii ya Watunza Kumbukumbu na Nyaraka, Mhe. Simbachawene amesema Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora imekamilisha zoezi la kuhuisha Muundo wa Maendeleo ya Utumishi wa Kada ya Watunza Kumbukubu na Nyaraka na Muundo ambao ulianza kutumika kuanzia tarehe 01 Julai, 2023.
Ili kuongeza ari na morali ya utekelezaji wa majukumu ya watumishi wa umma, Mhe. Simbachawene amesema Serikali itaendelea kupandisha vyeo Kada hii na Watumishi wa Umma wengine kulingana na upatikanaji wa fedha.
Mhe. Simbachawene amemhakikishia Waziri Mkuu kuwa, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora itaendelea kutoa ushirikiano kwa Viongozi wa TRAMPA na kusimamia utendaji kazi wa Wataalam wa kada hii pamoja na kutatua changamoto mbalimbali za kisera na kiutendaji ili kuwezesha utoaji wa huduma bora na yenye tija kwa maendeleo ya Taifa.
Mkutano wa wanachama wa Chama cha Menejimenti ya Watunza Kumbukumbu na Nyaraka (TRAMPA) hufanyika kila mwaka ambapo wataalam hawa hupata muda wa kujikumbusha masuala mbalimbali yanayohusiana na taaluma yao na mafunzo mbalimbali kuhusu Maadili ya Utendaji kazi, Miundo ya Maendeleo ya Utumishi iliyopo Serikalini ikiwemo kada yao, Uendeshaji wa Serikali, Usalama na Utunzaji Siri za Serikali.
Mkutano huu wa siku tatu unafanyika kwa kaulimbiu isemayo“Utunzaji
bora wa Kumbukumbu na Nyaraka ni Chachu ya Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa”
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Watunza Kumbukumbu na Nyaraka
wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 11 wa Chama cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka
Tanzania (TRAMPA) uliofanyika jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene akitoa maelezo ya awali kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa kuhusu mkutano wa Watunza Kumbukumbu na Nyaraka
wakati wa Mkutano Mkuu wa
11
wa Chama cha Menejimenti ya
Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) uliofanyika jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wa mkutano wa Watunza
Kumbukumbu na Nyaraka wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (hayupo
pichani) wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 11 wa Chama cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka
Tanzania (TRAMPA) jijini Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Kulia) akipokea zawadi ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyotolewa na Chama cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania
(TRAMPA) wakati wa Mkutano Mkuu wa 11 wa Chama hicho uliofanyika jijini Dodoma. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene aliyekabidhi zawadi hiyo
kwa niaba ya chama hicho.
MHE. RIDHIWANI KIKWETE AKAGUA MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU WA TRAMPA JIJINI DODOMA
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akisalimiana na baadhi ya Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa umma na Utawala Bora mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kukagua maandalizi ya mkutano Mkuu wa Chama Cha Wahifadhi Kumbukumbu na Nyaraka unaotarajiwa kufunguliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Jijini Dodoma.
Baadhi ya Wahifadhi Kumbukumbu na Nyaraka wakimsiliza Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kukagua maandalizi ya mkutano Mkuu wa Chama Cha Wahifadhi Kumbukumbu na Nyaraka ambapo Mgeni Rasmi wa Mkutano huo anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tnzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa umma, Bw. Xavier Daudi akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kukagua maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Chama Cha Wahifadhi Kumbukumbu na Nyaraka unaotarajiwa kufunguliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Jijini Dodoma.
Thursday, October 26, 2023
KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA,KATIBA NA SHERIA YARIDHISHWA NA OFISI YA RAIS-UTUMISHI KATIKA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE
1. Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala,
Katiba na Sheria, Mhe. Florent Kyombo akiongoza kikao kazi cha kamati yake na
Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
kuhusu Utekelezaji wa Mpango na Bajeti wa Taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo
(Tume ya Utumishi wa Umma, Watumishi Housing, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za
Taifa ) kwa mwaka 2022/23
1. Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwasilisha taarifa ya Utelezaji wa Mpango na Bajeti wa taasisi
zilizo chini ya Ofisi yake (Tume ya Utumishi wa Umma, Watumishi Housing, Idara ya Kumbukumbu
na Nyaraka za Taifa) kwa mwaka 2022/23 kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao cha kamati hiyo
kilichofanyika jijini Dodoma.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakiwa katika kikao kazi cha kamati hiyo na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kilicholenga kuwasilisha Utekelezaji wa Mpango na Bajeti wa taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo (Tume ya Utumishi wa Umma, Watumishi Housing, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa) kwa mwaka 2022/23
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete akitoa ufafanuzi wa
moja ya hoja iliyowasilishwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na
Sheria wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo kuhusu Utekelezaji wa Mpango na Bajeti wa taasisi zilizo chini ya ofisi hiyo (Tume ya
Utumishi wa Umma, Watumishi Housing, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa) kwa mwaka 2022/23 kilichofanyika jijini Dodoma.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala,
Katiba na Sheria, Mhe. Abeid Ramadhan akichangia hoja kuhusu masuala ya ajira wakati wa kikao kazi cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba
na Sheria na viongozi pamoja na watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhusu Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa taasisi zilizo
chini ya ofisi hiyo (Tume ya Utumishi wa Umma, Watumishi Housing,
Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa ) kwa mwaka 2022/23.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala,
Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Alice Kaijage akichangia hoja kuhusu masuala ya ajira wakati wa kikao kazi cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba
na Sheria na viongozi pamoja na watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhusu Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa taasisi zilizo
chini ya ofisi hiyo (Tume ya Utumishi wa Umma, Watumishi Housing,
Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa ) kwa mwaka 2022/23.
Tuesday, October 24, 2023
OFISI YA RAIS-UTUMISHI NA TAASISI ZAKE ZAPONGEZWA NA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA KWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE KIKAMILIFU
Makamu Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Florent Kyombo akiongoza kikao kazi
cha kamati yake na Watendaji wa Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhusu Utekelezaji wa Mpango na
Bajeti wa Taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo (Sekretarieti ya Maadili
ya Viongozi wa Umma, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma na Chuo cha
Utumishi wa Umma) kwa mwaka 2022/23.
Wajumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakiwa
katika kikao kazi cha kamati hiyo na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora kilicholenga
kuwasilisha Utekelezaji wa Mpango na Bajeti wa taasisi zilizo chini ya Ofisi
hiyo (Sekretarieti
ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
na Chuo cha Utumishi wa Umma) kwa mwaka
2022/23.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwasilisha taarifa
ya Utelezaji wa
Mpango na Bajeti wa taasisi zilizo chini ya Ofisi yake (Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma,
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma na Chuo cha Utumishi wa Umma) kwa mwaka 2022/23 kwa Wajumbe wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao cha kamati hiyo kilichofanyika jijini
Dodoma.
Naibu Waziri,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani
Kikwete akitoa ufafanuzi wa moja ya hoja iliyowasilishwa na Wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao kazi cha kamati
hiyo kuhusu Utekelezaji wa Mpango na Bajeti wa taasisi zilizo chini ya
ofisi hiyo (Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Sekretarieti ya Ajira
katika Utumishi wa Umma na Chuo cha Utumishi wa Umma) kwa mwaka
2022/23
kilichofanyika jijini Dodoma.
Kamishna wa Maadili ya Viongozi wa Umma, Mhe. Jaji Sivangilwa Mwangesi akijibu moja ya hoja ya taasisi yake
kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati
wa kikao kazi cha kamati hiyo na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhusu Utekelezaji wa Mpango na
Bajeti kwa taasisi zilizo chini ya ofisi hiyo (Sekretarieti ya Maadili
ya Viongozi wa Umma, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma na Chuo cha
Utumishi wa Umma) kwa mwaka
2022/23.
Kaimu Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa
Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC), Dkt. Ernest Mabonesho akitoa
ufafanuzi wa hoja za masuala ya mafunzo yanayotolewa katika chuo hicho
zilizowasilishwa na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na Watendaji
wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhusu
Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa taasisi zilizo chini ya ofisi hiyo (Sekretarieti
ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
na Chuo cha Utumishi wa Umma) kwa mwaka
2022/23.
Kaimu Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika
Utumishi wa Umma, Bw. Innocent Bomani akijibu moja ya hoja ya masuala
ya ajira kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati
wa kikao kazi cha kamati hiyo na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhusu Utekelezaji wa Mpango na
Bajeti kwa taasisi zilizo chini ya ofisi hiyo (Sekretarieti ya Maadili ya
Viongozi wa Umma, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma na Chuo cha
Utumishi wa Umma) kwa mwaka
2022/23.
Mjumbe wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Jonas Zeeland
(Aliyenyanyua mkono) akichangia hoja
kuhusu masuala ya ajira wakati wa kikao kazi cha Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria na viongozi pamoja na watendaji wa Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhusu
Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa taasisi zilizo chini ya ofisi hiyo (Sekretarieti
ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
na Chuo cha Utumishi wa Umma) kwa mwaka
2022/23.
Katibu Mkuu-IKULU, Bw.
Mululi Majula Mahendeka akitoa ufafanuzi wa hoja iliyowasilishwa na Wajumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao
kazi cha kamati hiyo na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora kuhusu Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa taasisi zilizo chini ya ofisi
hiyo (Sekretarieti
ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
na Chuo cha Utumishi wa Umma) kwa mwaka
2022/23.
Kaimu Katibu Mkuu,
Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Xavier Daudi akitoa ufafanuzi wa moja
ya hoja iliyowasilishwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala
Katiba na Sheria wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhusu
Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa taasisi zilizo chini ya ofisi hiyo (Sekretarieti
ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
na Chuo cha Utumishi wa Umma) kwa mwaka
2022/23.
Sehemu ya Watendaji wa Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwa katika kikao kazi
cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria na Watendaji wa
ofisi hiyo kuhusu Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa taasisi zilizo chini ya ofisi
hiyo (Sekretarieti
ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
na Chuo cha Utumishi wa Umma) kwa mwaka
2022/23.
Thursday, October 19, 2023
WARATIBU WA TASAF HANDENI WAPONGEZWA KWA KUWASHIRIKISHA VIONGOZI WAO KATIKA MATUMIZI YA FEDHA ZA MIRADI YA TASAF
Na. Rainer Budodi- Handeni
Tarehe 19 Oktoba,
2023
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amewapongeza Waratibu wa Mfuko
wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Halmashauri ya Wilaya ya Handeni mkoani
Tanga kwa kuwashirikisha viongozi wao juu ya matumizi ya fedha za miradi ya
TASAF inayopelekwa katika Halmashauri ya Wilaya hiyo.
Mhe. Simbachawene ametoa pongezi hizo
leo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa maendeleo ya miradi
ya TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Handeni mkoani Tanga.
“Nawapongeza sana Waratibu wa Halmashauri hii ya Handeni kwa kuwashirikisha viongozi wenu katika matumizi ya fedha zinazoletwa na TASAF, ushirikiano huu ni mzuri kwa sababu fedha hizi zinatakiwa zitumike kwa uwazi bila kificho chochote ili kutimiza malengo yaliyokusudia,” Mhe. Simbachawene ameongeza.
Amesema viongozi wengi katika Halmashauri za Wilaya hawana taarifa juu ya fedha za miradi ya TASAF zinazoingia katika Wilaya zao lakini imekuwa tofauti kwa Wilaya ya Handeni, ambapo Mkuu wa Wilaya hiyo katika maelezo yake anaonekana kuufahamu vizuri utekelezaji wa mradi huu.
“Mkuu wa Wilaya, nimefurahi sana kuona kuwa mradi huu unauelewa vizuri maana umeuzungumzia vizuri sana, hii inaonyesha kuwa unashirikishwa kikamilifu, na hivi ndivyo inavyotakiwa,” Mhe. Simbachawene ameongeza.
Amemsisitiza Mkuu wa Wilaya hiyo ya Handeni Mhe. Albert Msando kuendelea kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo badala ya kuwaachia waratibu pekee kwa kuwa fedha za miradi zinazopelekwa ni nyingi, hivyo zinahitaji usimamizi ili zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa.
Mhe. Simbachawene amehitimisha ziara yake ya kikazi ya siku tatu ya kuzungumza na watumishi wa umma na kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri za Wilaya ya Mkinga, Korogwe na Handeni mkoani Tanga.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiteta na Mkuu wa
Wilaya ya Handeni, Mhe. Albert Msando wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua
utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Kijiji cha Mkata Mashariki, Kata ya
Mkata, Halmashauri ya Wilaya ya Handeni mkoani Tanga.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akikata utepe
kuzindua mradi wa kivuko uliotekelezwa na walengwa wa TASAF katika Kijiji cha
Mkata Mashariki, Kata ya Mkata, Halmashauri ya Wilaya ya Handeni mkoani Tanga
wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani
Tanga.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akipata maelezo toka
kwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Albert Msando kuhusu mradi wa kivuko
uliotekelezwa na walengwa wa TASAF katika Kijiji cha Mkata Mashariki, Kata ya
Mkata, Halmashauri ya Wilaya ya Handeni mkoani Tanga wakati wa ziara yake ya
kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Tanga.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na wananchi na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Kijiji cha Mkata Mashariki, Kata ya Mkata, Halmashauri ya Wilaya ya Handeni mkoani Tanga wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani humo.
Sehemu ya wananchi na walengwa wa Mpango wa
Kunusuru Kaya Maskini wa Kijiji cha Mkata Mashariki, Kata ya Mkata, Halmashauri
ya Wilaya ya Handeni wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene alipokuwa
akizungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi
ya TASAF mkoani Tanga.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiangalia bango
linaloonyesha miradi inayotekelezwa na walengwa wa TASAF katika Kijiji cha
Mkata Mashariki, Kata ya Mkata, Halmashauri ya Wilaya ya Handeni mkoani Tanga
wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani
Tanga.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akionyesha kutaka
ufafanuzi wa moja ya mradi ulioko kwenye bango linaloonyesha miradi
inayotekelezwa na walengwa wa TASAF katika Kijiji cha Mkata Mashariki, Kata ya
Mkata, Halmashauri ya Wilaya ya Handeni mkoani Tanga wakati wa ziara yake ya
kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF mkoani Tanga.