Na.
James K. Mwanamyoto-Singida
Tarehe
13 Januari, 2021
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi ametoa maelekezo hayo kwa Maafisa Ugani akiwa kijiji cha Mtinko Wilayani Singida katika ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini mkoani Singida.
Mhe.
Ndejembi amewahimiza Wakurugenzi Watendaji na Maafisa Ugani katika Halmashauri zote
kutoa maelekezo kwa kaya maskini juu ya namna bora ya kulima mazao
yanayostahimili ukame na kuendana na mazingira halisi ya maeneo husika ili kaya
maskini ziweze kunufaika na kilimo.
“Maafisa Ugani katika ngazi ya kata na vijiji waanze kuzitembelea kaya maskini na kuzisaidia namna ya kulima kitaalamu ili ziweze kupata mavuno ya kutosha na kuongeza kuwa, Maafisa Ugani waache kwenda kwenye miradi ya nyama pekee ambayo inawanufaisha kwa kujipatia fedha, Mhe. Ndejembi amesisitiza.
Sanjali na hilo, Mhe. Ndejembi amepokea shuhuda mbalimbali za mafanikio waliyoyapata wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Kijiji cha Mtinko wilayani Singida.
Mmoja
wa wanufaika, Bi. Leah Ibrahimu Shila amesema, ameitumia fedha ya
ruzuku aliyoipokea kujiwekea akiba kidogo kidogo na hatimaye kupata mtaji wa shilingi
200,000/= uliomuwezesha kufungua mgahawa wa kuuza chakula.
Bi. Shila ameeleza kuwa, kabla ya kuwa mnufaika wa TASAF alikuwa akiishi maisha magumu yaliyomsababishia kula mlo mmoja kwa siku lakini hivi sasa anakula milo mitatu na anasomesha watoto wake katika shule za msingi na sekondari.
Naye, Bi. Zena Ramadhani Igwe amemueleza Mhe. Ndejembi kuwa, ametumia vizuri ruzuku aliyoipokea toka TASAF kwa kujenga nyumba bora ya bati kwani aliweza kuwekeza fedha kidogo kidogo ambazo zilimuwezesha kununua saruji na bati.
Ameongeza kuwa, fedha hizo zimemsaidia pia kuanza shughuli ya ufugaji wa kuku ambao wamefikia 30 na ameweza kujishughulisha na kilimo cha bustani, ikiwa ni pamoja na kumsomesha mtoto wake elimu ya sekondari.
Mhe. Ndenjembi ameridhishwa na mafanikio waliyoyapata wanufaika wa TASAF, Bi. Lea Ibrahimu Shila na Bi. Zena Ramadhani Igwe wa Kijiji cha Mtinko Wilayani Singida na kutoa wito kwa wanufaika wote wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini nchini, kuzitumia vema fedha za ruzuku katika shughuli mbalimbali za kiuchumi zitakazoboresha maisha yao na kuondokana na umaskini.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza
na wananchi na wanufaika wa TASAF katika Kijiji cha Mtinko wilayani Singida wakati
wa ziara yake ya kikazi wilayani humo yenye lengo la kukagua utekelezaji wa
Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini mkoani Singida.
Baadhi
ya wananchi na wanufaika wa TASAF katika Kijiji cha Mtinko Wilayani Singida
wakisikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (Hayupo pichani) wakati wa ziara kikazi ya
Naibu Waziri huyo wilayani humo yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Mpango wa
Kunusuru Kaya Maskini mkoani Singida.
Mnufaika
wa TASAF Kijiji cha Mtinko wilayani Singida, Bi. Leah Ibrahimu Shila akieleza
mafanikio aliyoyapata kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) wakati wa
ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo yenye lengo la kukagua utekelezaji wa
Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wilayani Singida.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius
Ndejembi (kushoto) akila chakula kwenye mgahawa wa mnufaika wa TASAF kijiji cha
Mtinko Wilayani Singida, Bi. Leah Ibrahimu Shila (wa kwanza kulia) wakati wa
ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo yenye lengo la kukagua utekelezaji wa
Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Wilayani Singida.
Mnufaika
wa TASAF Kijiji cha Mtinko Wilayani Singida, Bi. Zena Ramadhani Igwe akieleza
mafanikio aliyoyapata kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) wakati wa
ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo yenye lengo la kukagua utekelezaji wa
Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Wilayani Singida.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akisisitiza
jambo mbele ya nyumba ya mnufaika wa TASAF Kijiji cha Mtinko Wilayani Singida,
wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani humo yenye lengo la kukagua utekelezaji
wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wilayani Singida.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akipokea
zawadi ya kuku kutoka kwa mmoja wa wanufaika wa TASAF Kijiji cha Mtinko
Wilayani Singida, wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo yenye lengo la
kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Wilayani Singida.
No comments:
Post a Comment