Na. James Mwanamyoto - Uyui
Tarehe 26 Januari, 2021
Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wanaopokea ruzuku inayotolewa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) wamekumbushwa wajibu wa kuboresha maisha yao kwa kutumia vizuri fedha za ruzuku wanazopatiwa ili kuondokana na umaskini.
Akiwa katika ziara ya kikazi kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Kijiji cha Kinamagi Wilayani Uyui, Mkoa wa Tabora, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amewaasa wanufaika kutotumia kwa anasa ruzuku inayotolewa na TASAF na badala yake waitumie katika shughuli za maendeleo kama kilimo, ufugaji na ujasiriamali.
Mhe. Ndejembe
amefafanua kuwa, ni wajibu wa kila mnufaika kuhakikisha anajiinua kiuchumi
kupitia fedha inayotolewa na TASAF, kwani Serikali kwa upande wake inaendelea
kutekeleza wajibu wake na maelekezo ya Mheshimiwa Rais ya kuziwezesha kaya zote
maskini nchini kupitia utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.
Mhe. Ndejembi amewataka wanufaika wa TASAF kutosita kujikwamua katika umaskini kwa kuhofia kuondolewa kwenye Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, na badala yake wajisikie fahari kuondokana na umaskini na hatimaye kuwa mfano bora wa kuigwa na wanufaika wengine ambao hawakutumia vema ruzuku inayotolewa na TASAF.
Aidha, Mhe. Ndejembi amezitaka Serikali za Vijiji kuacha kudai tozo ndogo ndogo kama za ujenzi wa shule siku ambayo wanufaika wanapokea ruzuku, kwani tozo hizo zinawakwamisha wanufaika kutumia ruzuku wanayoipata kwa ajili ya shughuli zitakazowasaidia kujiondoa katika umaskini.
Sanjali na hilo, Mhe. Ndejembi amewataka Watendaji wa Vijiji na Kata kutokata ruzuku za wanufaika kwa ajili ya kuchangia huduma za Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwani wanakwamisha jitihada za wanufaika kuboresha maisha yao, hivyo amewataka kuwaacha wanufaika wazalishe fedha ndipo wachangie huduma za mfuko huo.
Mara baada ya kuzungumza na Wananchi na wanufaika wa TASAF katika Kijiji cha Kinamagi, Mhe. Ndejembi aliwatembea wanufaika ili kujionea maendeleo waliyoyapa na hatimaye kushuhudia maendeleo ya Bi. Enviolatha Gerald Kamage ambaye ametumia vizuri ruzuku kununua cherehani, kujenga nyumba, kununua sola na kuweka umeme wa REA.
Mhe. Ndejembi ameshuhudia pia, maendeleo ya mnufaika wa TASAF, Bi. Zena Hussein Maganga ambaye amefanikiwa kutumia vema ruzuku kwa kufuga mbuzi, kuku, kununua mbolea kwa ajili ya kilimo ikiwa ni pamoja na kununua sola inayowawezesha watoto wake kujisomea wakati wa usiku.
Madhumuni
ya utekelezaji wa Mpango wa Kuzinusuru Kaya Maskini nchini ni kuziwezesha kaya
hizo kuboresha maisha kwa kuongeza kipato, fursa na uwezo wa kugharamia
mahitaji ya msingi kama vile chakula, mavazi, malazi, huduma za afya na
mahitaji ya wanafunzi shuleni.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Deogratius Ndejembi akizungumza na wananchi na wanufaika wa TASAF (hawapo
pichani) Kijiji cha Kinamagi Wilayani Uyui, Mkoa wa Tabora wakati wa ziara ya
kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa Mpango wa
Kunusuru Kaya Maskini.
Baadhi
ya wananchi na wanufaika wa TASAF Kijiji cha Kinamagi Wilayani Uyui, Mkoa wa
Tabora wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza
nao wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kukagua
utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Deogratius Ndejembi akiwahimiza wanufaika wa TASAF Kijiji cha Kinamagi Wilayani
Uyui, Mkoa wa Tabora kutumia vizuri ruzuku wanayoipata ili kuboresha maisha yao
na kuondokana na umaskini, wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo
iliyolenga kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (kulia)
akimsikiliza mnufaika wa TASAF, Bi. Zena Hussein wa Maganga wa Kijiji cha
Kinamagi Wilayani Uyui, Mkoa wa Tabora akielezea mafanikio aliyoyapa kupitia
TASAF, wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo iliyolenga kukagua
utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Deogratius Ndejembi akiwatazama mbuzi wa mnufaika wa TASAF Kijiji cha Kinamagi
Wilayani Uyui, Mkoa wa Tabora, Bi. Zena Hussein Maganga alipomtembelea mnufaika
huyo ili kujionea mafanikio aliyoyapata wakati wa ziara yake ya kikazi
iliyolenga kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Deogratius Ndejembi akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu
tathmini ya ziara yake ya kikazi yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Mpango
wa Kunusuru Kaya Maskini, mara baada ya Naibu Waziri huyo kumaliza zoezi la
kuwatembelea wanufaika wa TASAF katika Kijiji cha Kinamagi Wilayani Uyui, Mkoa
wa Tabora.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Deogratius Ndejembi akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na mnufaika wa
TASAF, Bi. Enviolatha Gerald Kamage mbele ya nyumba ya mnufaika huyo ambaye
ametumia ruzuku aliyoipata kujenga nyumba hiyo, kununua cherehani, sola na kuweka
umeme wa REA.
No comments:
Post a Comment