Saturday, March 21, 2020

WATUMISHI HOUSING COMPANY IMESHAURIWA KUTENGA NYUMBA ZA KUWAUZIA NA KUPANGISHA WADAU WA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII






Naibu Waziri ,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa akikagua nyumba zilizojengwa na Watumishi Housing Company eneo la Gezaulole jijini Dar es Salaam.Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Company Dkt. Fred Msemwa.

Mkurugenzi wa Watumishi Housing Company, Dkt. Fred Msemwa akitoa maelezo kuhusu mradi wa nyumba za kampuni hiyo kwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi ujenzi wa nyumba eneo la Gezaulole jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary akitoa ushauri juu ya upangishaji na uuzaji wa nyumba kwa watendaji wa Watumishi Housing Company katika mojawapo ya nyumba alizozikagua eneo la Gezaulole  - Kigamboni jijini Dar Es salaam.

Baadhi ya Nyumba za ghorofa za Mradi wa Watumishi Housing Company zilizojengwa kwa madhumuni ya kuuzwa kwa Watumishi wa Umma na kupangishwa zilizopo katika eneo la  Gezaulole Kigamboni nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment