Saturday, March 14, 2020

SERIKALI YAKANUSHA UVUMI WA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA KAMPASI YA SINGIDA KUHAMISHIWA DODOMA


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Dkt. Jasson Rweikiza (Mb), akitazama ramani ya kiwanja cha Mungumaji ambacho Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Singida kinatarajiwa kujengwa wakati wa ziara ya kamati hiyo ya kukagua kiwanja hicho iliyofanyika jana.

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, wakisikiliza maelezo ya mpango wa ujenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Singida kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma na Mtendaji Mkuu wa Taasisi, Dkt. Selemani Shindika,  wakati wa ziara ya kamati hiyo ya kukagua kiwanja hicho iliyofanyika jana.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George Mkuchika (Mb) akifafanua kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, uvumi ulioenea wa Serikali kukihamishia Dodoma Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Singida wakati wa ziara ya kamati hiyo iliyofanyika jana ya kukagua kiwanja cha Mungumaji ambacho Kampasi ya Singida inatarajiwa kujengwa.

Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Emmanuel Selemani Shindika akitoa ufafanuzi kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, kuhusu kiwanja kilichonunuliwa kwa ajili ya Ujenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Singida wakati wa ziara ya kamati hiyo iliyofanyika jana.

No comments:

Post a Comment