Wednesday, March 18, 2020

UTUMISHI YAPOKEA VITENDEA KAZI TOKA UNDP KUBORESHA UTENDAJI


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (kulia) akimpongeza Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimaliwatu, Mkoa wa Shinyanga, Bw. James Bwana kwa kuwezesha kupatikana kwa vitendea kazi vya kielektroniki toka Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Umoja wa Mataifa (UNDP) mara baada ya Katibu Tawala huyo kukabidhi vitendea kazi hivyo katika ukumbi wa Ofisi ya Rais, Utumishi, Mtumba jijini Dodoma. 


Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimaliwatu, Mkoa wa Shinyanga, Bw. James Bwana akitoa maelezo ya vitendea kazi vilivyotolewa na UNDP kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (kulia) katika ukumbi wa Ofisi ya Rais, Utumishi, Mtumba jijini Dodoma.

Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimaliwatu, Mkoa wa Shinyanga, Bw. James Bwana, akionyesha nyaraka zenye orodha ya vitendea kazi vilivyotolewa na UNDP kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (kulia).

Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi, Ofisi ya Rais, Utumishi, Bw. Victor Ngole, akipokea nyaraka leo toka kwa Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimaliwatu, Mkoa wa Shinyanga, Bw. James Bwana zinazoonyesha orodha ya vitendea kazi vilivyotolewa na UNDP. Anayeshuhudia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro. 

Vitendea kazi vya kielektroniki vilivyotolewa na UNDP kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi wa watumishi wa watumishi wa Ofisi ya Rais, Utumishi vikishushwa leo kwa ajili ya makabidhiano rasmi katika ofisi hiyo, Mtumba jijini Dodoma. 

No comments:

Post a Comment