Thursday, March 5, 2020

TASAF YABORESHA MAISHA YA BIBI WA MIAKA 90 CHUNYA


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na Mnufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Bibi Rozena Bilia Mwambogo alipomtembelea mnufaika huyo kijiji cha Mapogoro wilayani Chunya wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo yenye lengo la kukagua utekelezaji wa mpango wa TASAF mkoani Mbeya.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Mnufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, Bibi Rozena Bilia Mwambogo wakielekea kushuhudia banda la nguruwe wanaofugwa na mnufaika huyo kutokana na ruzuku ya TASAF.

Banda la Nguruwe wanaofugwa na Bibi Rozena Mwambogo ambao amewanunua kupia ruzuku ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF).

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na mgonjwa, Mzee Gidison Mwayiyi ambae anauguzwa na mnufaika wa TASAF Bibi Rozena Mwambogo alipomtembelea mnufaika huyo katika kijiji cha Mapogoro wilayani Chunya wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo yenye lengo la kukagua utekelezaji wa mpango wa TASAF mkoani Mbeya.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akimfariji mgonjwa, Mzee Gidison Mwayiyi ambae anauguzwa na mnufaika wa TASAF Bibi Rozena Mwambogo alipomtembelea mnufaika huyo katika kijiji cha Mapogoro wilayani Chunya.


No comments:

Post a Comment