Saturday, March 14, 2020

KAMATI YA BUNGE YAIPONGEZA MKURABITA KWA KURAHISISHA MCHAKATO WA URASIMISHAJI WA BIASHARA KATIKA MANISPAA YA SINGIDA



Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Dkt. Jasson Rweikiza (Mb), akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Biashara wa Manispaa ya Singida, Bw. Erick Simkwembe ya namna Kituo cha Pamoja cha Urasimishaji na Uendelezaji Biashara, Manispaa ya Singida kinavyofanya kazi.

Baadhi ya Wafanyabiashara wanaofaidika na uwepo wa Kituo cha Pamoja cha Urasimishaji na Uendelezaji Biashara, Manispaa ya Singida, wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Dkt. Jasson Rweikiza (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao leo wakati wa ziara ya kamati yake mkoani humo yenye lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya Serikali mkoani Singida.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George Mkuchika (Mb) akitoa maelezo kuhusu utekelezaji wa MKURABITA kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakati wa ziara ya kamati hiyo mkoani Singida yenye lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya Serikali mkoani Singida.

Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Biashara na Rasilimali za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), Dkt. Seraphia Mgembe akitoa ufafanuzi kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wa namna MKURABITA ilivyoshiki katika uanzishwaji wa Kituo cha Pamoja cha Urasimishaji na Uendelezaji Biashara, Manispaa ya Singida wakati wa ziara ya kamati hiyo mkoani Singida yenye lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya Serikali mkoani humo.

Mfanyabiashara wa Manispaa ya Singida, Bi. Happy Francis akitoa maelezo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusiana na bidhaa anazozalisha wakati wa ziara ya kamati hiyo mkoani Singida yenye lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya Serikali mkoani humo.

No comments:

Post a Comment