Tuesday, March 10, 2020

SERIKALI YAFANYA MAPITIO YA RASIMU YA MUONGOZO WA KUANDAA MPANGO WA RASILIMALIWATU KATIKA UTUMISHI WA UMMA


Mkurugenzi wa Uendelezaji Sera Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Agnes Meena akifungua kikao kazi cha wadau cha kupitia Rasimu ya Mwongozo wa kuandaa Mpango wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro katika ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa Dodoma.

Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango ya Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Edith Rwiza akitoa maelezo ya awali kwa wadau juu ya umuhimu na faida za kupitia Rasimu ya Mwongozo wa kuandaa Mpango wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma katika ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa Dodoma.
Mkurugenzi wa Sera Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Agnes Meena (wa tatu kushoto mstari wa mbele) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa kikao kazi cha kupitia Rasimu ya Mwongozo wa kuandaa Mpango wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma.

Baadhi ya wadau walioshiriki kikao kazi cha kupitia rasimu ya Mwongozo wa kuandaa mpango wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma wakimsilikiza Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango ya Rasilimaliwatu, Dkt, Edith Rwiza (hayupo pichani).



No comments:

Post a Comment