Monday, February 16, 2026

WATUMISHI WA UMMA, WANANCHI WAPEWA NYENZO YA KUWASILIANA NA SERIKALI

Na. Veronica Mwafisi- Dodoma.

Tarehe 16 Februari, 2026 

“Mfumo wa e-Mrejesho unalenga kuboresha huduma zinazotolewa na Serikali na ni sehemu ya utekelezaji wa dhana ya Utawala Bora ambayo inajali maslahi ya wengi, kuwa na uwazi, kupiga vita dhidi ya rushwa, kuleta haki na usawa na kuhimiza uwajibikaji”.


Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Msaidizi wa Ufuatiliaji na Uzingatiaji wa Maadili, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Janet Mishinga alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu Mfumo wa e-Mrejesho wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji Watumishi wa ofisi hiyo jijini Dodoma.

Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kupitia Idara ya Usimamizi Maadili imewahimiza Watumishi wa Umma na Wananchi kutumia Mfumo wa Kielektroni wa Kutuma, Kupokea na Kufuatilia Malalamiko, Mapendekezo, Maulizo na Pongezi Serikalini (e-Mrejesho) ili kuongeza ufanisi katika kushughulikia mrejesho wa masuala mbalimbali ya kiutumishi na kuboresha huduma kwa umma.


Aidha Bi. Mishinga alifafanua kuwa, ufuatiliaji wa utekelezaji wa mfumo wa e-Mrejesho una lengo la kubaini mafanikio na changamoto ili kuimarisha uadilifu katika kushughulikia mrejesho wa wananchi ikiwa ni pamoja na kufanya tathmini ya utendaji wa taasisi katika kuhudumia wananchi.

Pia, alibainisha kuwa utaratibu wa kushughulikia mrejesho kuhusu mfumo huo unaongeza ushirikishwaji kwa watumishi wa umma na wananchi.

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi (kushoto) akifuatilia wasilisho la mada kuhusu Mfumo wa e-Mrejesho wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji Watumishi wa ofisi hiyo ambayo hutolewa kila siku ya Jumatatu kwenye ofisi hiyo iliyopo Mtumba jijini Dodoma.


Mkurugenzi Msaidizi wa Ufuatiliaji na Uzingatiaji wa Maadili, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Janet Mishinga akifafanua jambo alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu Mfumo wa e-Mrejesho wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji Watumishi wa ofisi hiyo jijini Dodoma.


Wakurugenzi wa Idara na Vitengo kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakifuatilia wasilisho la mada kuhusu Mfumo wa e-Mrejesho wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji Watumishi wa ofisi hiyo yaliyofanyika katika ofisi hiyo jijini Dodoma.


Wakurugenzi Wasaidizi kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakifuatilia wasilisho la mada kuhusu Mfumo wa e-Mrejesho wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji Watumishi wa ofisi hiyo ambayo hufanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma. Wengine ni Watumishi wa ofisi hiyo.


Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakifuatilia wasilisho la mada kuhusu Mfumo wa e-Mrejesho wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji Watumishi wa ofisi hiyo ambayo hufanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.


Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakifuatilia wasilisho la mada kuhusu Mfumo wa e-Mrejesho wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji Watumishi wa ofisi hiyo ambayo hufanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.


 

 



 

No comments:

Post a Comment