Na Veronica Mwafisi-Arusha
Tarehe 19.02.2026
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amekea tabia ya baadhi ya Waajiri kuwahamisha watumishi wanaowakuta katika Ofisi walizoteuliwa na kutaka wahamishiwe katika vituo vingine vya kazi.
Waziri Kikwete ameyasema hayo leo tarehe 19 Februari, 2026 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC) jijini Arusha wakati akifunga rasmi mkutano wa sita wa Serikali Mtandao ulioanza tarehe 17 Februari, 2026.
Amesema kama ikitokea mtumishi ana tatizo lolote la kiutumishi linalohitaji hatua za kinidhamu, apelekwe kwenye vikao vya kinidhamu ili adhabu stahiki itolewe na sio kuwaonea watu kwasababu ya unyonge wao.
“Nataka niwakumbushe kuwa, kila mmoja aliingia kwa sifa zake, wengine wameingizwa kupitia mitihani ya ajira, wengine kwa nafasi za uteuzi, hivyo kila mmoja akitimiza wajibu wake ni wazi kuwa matokeo mazuri yataonekana.
Aidha, amepiga marufuku watumishi wa umma kutumia barua pepe binafsi kutuma taarifa za ofisi badala ya kutumia barua pepe rasmi za serikali.
“Ni changamoto kubwa sana, bado tunao watumishi wa umma wanaotumia mitandao binafsi kutuma taarifa rasmi za serikali, tunachokifanya ni jambo la hatari sana, tutumie mifumo yetu iliyotengenezwa na wataalam wetu wa ndani,” Mhe. Kikwete ameongeza.
Waziri Kikwete amewapongeza e-GA kwa kazi nzuri wanayofanya na kuwasisitiza Waajiri kutumia wataalam hao kutengeneza mifumo katika taasisi zao.
Ametoa wito kwa wataalamu wa TEHAMA kuendelea kujifunza kila wakati ili waweze kukabiliana na changamoto mbambali ikiwemo shambulio la mifumo ya TEHAMA.
Akitoa salamu kwa niaba ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro amemshukuru Waziri Kikwete kwa kuona umuhimu wa kuishirikisha kamati hiyo. “Mmetambua uwepo wa mhimili wa Bunge, mngeweza hata kufanya wenyewe bila hata ya kutushirikisha,” ameongeza Mhe. Dkt. Ndumbaro.
Amesema yeye sio mtaalam wa TEHAMA, lakini bado anatambua umuhimu wa serikali mtandao na kuongeza kuwa, kwa dunia ya leo hatuwezi kusonga mbele bila ya TEHAMA.
Amesema, Tanzania imepata mafanikio makubwa ambayo yanatokana na kazi nzuri ya Serikali kupitia Chama Cha Mapinduzi pamoja, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA).
“Sisi kama kamati na Bunge tunatambua mafanikio hayo. Mafanikio ya kupeleka huduma kwa umma, kunganisha mifumo, kutuhakikishia usalama mtandaoni ni kazi nzuri yenye mafanikio makubwa
Tuko
tayari kushirikiana na Wizara kuhakikisha changamoto zinazohusu sera, sharia na
bajeti zinafanyiwa kazi. Kila mawasiliano ya Bunge yanakwenda kwa mtandao.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) Mhandisi Benedict Ndomba amemshukuru Waziri Kikwete pamoja na uongozi wa Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa maelekezo na msisitizo
kuhusu uzingatiaji wa Sheria, Kanuni, Viwango na Miongozo ya Serikali Mtandao
kwani vimeongeza uzito, mwelekeo na ari mpya kwa washiriki wote. “Tunathamini
sana mchango wako na w viongozi wote katika kuendeleza ajenda ya mageuzi ya
kidijitali Serikalini,” Mhandisi Ndomba amesisitiza.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani
Kikwete akizungumza na Maafisa Masuuli, Maafisa TEHAMA na watumiaji wa
Mifumo ya TEHAMA Serikalini wakati akifunga mkutano wa
sita wa Serikali Mtandao katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC)
jijini Arusha.
Sehemu
ya Maafisa Masuuli, Maafisa TEHAMA na watumiaji wa Mifumo ya TEHAMA Serikalini
wakiwa kwenye mkutano wa sita wa Serikali Mtandao uliofanyika
katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC) jijini Arusha.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika
viwanja vya AICC Arusha kwa ajili ya kufunga mkutano wa
sita wa Serikali Mtandao.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete (katikati) akisikiliza
maelezo kuhusu mifumo mbalimbali wakati alipotembelea banda la Mamlaka ya
Serikali Mtandao (eGA) kabla ya kufunga mkutano wa sita
wa Serikali Mtandao uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha
(AICC) jijini Arusha. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA),
Mhandisi Benedict Ndomba
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete akifurahia
jambo wakati akitembelea mabanda mbalimbali kabla ya kufunga mkutano wa sita wa Serikali Mtandao uliofanyika katika
Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC) jijini Arusha. Kushoto kwake
ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA), Mhandisi Benedict
Ndomba
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Ridhiwani Kikwete akifurahia
jambo wakati akitembelea mabanda mbalimbali kabla ya kufunga mkutano wa sita wa Serikali Mtandao uliofanyika katika
Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC) jijini Arusha. Kushoto kwake
ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA), Mhandisi Benedict
Ndomba
Sehemu
ya Washirkiki na Wanakamati wa mkutano wa sita wa Serikali Mtandao wakifuatilia
hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) uliofanyika katika Kituo
cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC) jijini Arusha.
Sehemu ya Maafisa Masuuli, Maafisa TEHAMA na watumiaji wa Mifumo ya TEHAMA Serikalini wakiwa kwenye mkutano wa sita wa Serikali Mtandao uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC) jijini Arusha.
Sehemu
ya Maafisa Masuuli, Maafisa TEHAMA na watumiaji wa Mifumo ya TEHAMA Serikalini
wakiwa kwenye mkutano wa sita wa Serikali Mtandao uliofanyika katika Kituo cha
Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC) jijini Arusha.





No comments:
Post a Comment