Tuesday, January 6, 2026

ZIARA YA KIKAZI YA NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA, MHE. REGINA QWARAY MKOA WA MANYARA

 


WAZIRI KIKWETE AMTEMBELEA MAMA MARIA NYERERE NA MAMA ANNA MKAPA

Na. Veronica Mwafisi-Dar es salaam

Tarehe 06 Januari, 2026

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete amewatembelea na kuwajulia hali Mama Maria Nyerere, mke wa Hayati Baba wa Taifa na Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam na Mama Anna Mkapa, mke wa Hayati Benjamin William Mkapa nyumbani kwake Masaki Jijini Dar es Salaam leo Januari, 2026.

Mhe. Kikwete amesema, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anathamini sana mchango wa Viongozi Wakuu wa Kitaifa waliomtangulia na ataendelea kusimamia na kutunza familia hizo kwa mujibu wa Katiba na Sheria zilizowekwa.

Aidha, Mhe. Ridhiwani amesema, kuwatembelea na kuwajulia hali wake hao wa Viongozi Wastaafu ni moja ya majukumu yake ambayo anayatekeleza kwa lengo la kuwajulia hali, kusikiliza changamoto zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi kwa mujibu wa Katiba na Sheria zilizowekwa.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi amesema ofisi hiyo itafanyia kazi maoni na ushauri uliotolewa na wajane hao.

Aidha, Mama Maria Nyerere amemshukuru Mhe. Kikwete kwa kupata nafasi ya kumtembelea na kumjulia hali na amempongeza Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuijali familia yake wakati wote pasipo kuchoka.

Naye, Mama Anna Mkapa ameishukuru ofisi hiyo kwa kufuatilia kwa karibu masuala yanayowahusu na kuyatafutia ufumbuzi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kushoto) akizungumza jambo na Mama Maria Nyerere (wa kwanza kulia), mke wa Hayati Baba wa Taifa na Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipomtembelea nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam kumjulia hali ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mama Maria Nyerere (kulia), mke wa Hayati Baba wa Taifa na Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipomtembelea nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam kumjulia hali ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake. 


Mama Maria Nyerere, mke wa Hayati Baba wa Taifa na Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (wa kwanza kulia) akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa pili kutoka kushoto) alipomtembelea nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam kumjulia hali ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake. Wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa ofisi hiyo Bw. Juma Mkomi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kulia) akifurahia jambo na Mama Maria Nyerere (hayupo pichani), mke wa Hayati Baba wa Taifa na Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi



Mkurugenzi Msaidizi Utawala na Dawati la Viongozi wa Kitaifa Wastaafu, Bi. Nyasinde Mukono (wa kwanza kushoto) akifurahia jambo wakati Mama Maria Nyerere (hayupo pichani), mke wa Hayati Baba wa Taifa na Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipokuwa akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) alipomtembelea kumjulia hali. Wengine ni Wakurugenzi kutoka katika ofisi hiyo.

Wakurugenzi na Maafisa kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora wakiwa nje ya nyumba ya Mama Maria Nyerere 9hayupo pichani), mke wa Hayati Baba wa Taifa na Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mara baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) kumjulia hali Mama Maria ikiwa ni utekelezaji wa majukumu yake.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kushoto) akifurahia jambo na Mama Anna Mkapa (kulia), mke wa Hayati Benjamin William Mkapa wakati alipomtembelea nyumbani kwake Upanga Jijini Dar es Salaam kumjulia hali ikiwa ni utekelezaji wa majukumu yake leo tarehe 06 Januari, 2026.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (kushoto) akifafanua jambo kwa Mama Anna Mkapa (hayupo pichani), mke wa Hayati Benjamin William Mkapa. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete ambaye alimtembelea Mama Anna Mkapa kumjulia hali ikiwa ni utekelezaji wa majukumu yake leo tarehe 06 Januari, 2026.


Mama Anna Mkapa (wa kwanza kulia), mke wa Hayati Benjamin William Mkapa akimsindikiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (katikati) wakati Waziri huyo akiondoka baada ya kumtembelea nyumbani kwake Upanga Jijini Dar es Salaam kumjulia hali ikiwa ni utekelezaji wa majukumu yake leo tarehe 06 Januari, 2026. Wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa ofisi hiyo Bw. Juma Mkomi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kushoto) akiagana na Mama Anna Mkapa (kulia), mke wa Hayati Benjamin William Mkapa wakati alipomtembelea nyumbani kwake Upanga Jijini Dar es Salaam kumjulia hali ikiwa ni utekelezaji wa majukumu yake leo tarehe 06 Januari, 2026.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (kushoto) akiagana na Mama Anna Mkapa (wa kwanza kulia), mke wa Hayati Benjamin William Mkapa mara baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (katikati) kumtembelea Mama Anna Mkapa nyumbani kwake Upanga Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kumjulia hali ikiwa ni utekelezaji wa majukumu yake leo tarehe 06 Januari, 2026.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa pili kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mama Anna Mkapa (katikati), mke wa Hayati Benjamin William Mkapa wakati Waziri huyo alipomtembelea nyumbani kwake Upanga Jijini Dar es Salaam leo tarehe 06 Januari, 2026.  Wa pili kutoka kulia ni Katibu Mkuu-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi na wengine ni Wakurugenzi kutoka katika ofisi hiyo.







NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA MHE. REGINA QWARAY ATOA WITO WA KUIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA UTOAJI WA HUDUMA KWA WANANCHI

 Na Eric Amani Dodoma, Tanzania

Naibu Waziri Ofisi ya Rais – UTUMISHI, Mhe. Regina Qwaray, ametoa wito kwa watumishi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma kuimarisha ushirikiano na mshikamano katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Mhe. Qwaray ametoa wito huo leo Januari 05, 2026 alipokuwa akizungumza na watumishi wa idara hiyo wakati wa ziara ya kikazi katika Idara hiyo akisisitiza kuwa ushirikiano wa karibu miongoni mwa watumishi ni nguzo muhimu katika kuhakikisha huduma za umma zinatolewa kwa ufanisi, uwazi na kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma.

Amesema kuwa Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuimarisha utendaji kazi katika utumishi wa umma, hivyo ni wajibu wa watumishi kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa weledi, uzalendo na kwa kushirikiana ili kufikia malengo ya Serikali ya kutoa huduma bora kwa wananchi.

“Msingi wa utumishi wa umma ni ushirikiano, kujutuma kwa bidii na kuweka maslahi ya mwananchi mbele. Ushirikiano wetu utaongeza ufanisi na kuimarisha imani ya wananchi kwa Serikali yao,” amesema Mhe. Qwaray.

Aidha, amewahimiza watumishi kuendelea kuzingatia maadili, nidhamu na miongozo ya utumishi wa umma pamoja na kutumia vyema rasilimali zilizopo katika kuwahudumia wananchi kwa haki na usawa.

Kwa upande wao, watumishi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma wameahidi kuendelea kushirikiana na kutekeleza majukumu yao kwa bidii na kuhakikisha huduma zinazotolewa zinakidhi matarajio ya wananchi.

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma Bi. Verediana Ngahega akijitambulisha kwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Regina Qwaray (hayupo pichani) katika kikao kazi Januari 5, 2026 Dodoma Tanzania


Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma Bw. Andrew Ponda akijitambulisha kwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Regina Qwaray (hayupo pichani) katika kikao kazi Januari 5, 2026 Dodoma Tanzania



Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma Bw. Baraka Manono akijitambulisha kwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Regina Qwaray (hayupo pichani) katika kikao kazi Januari 5, 2026 Dodoma Tanzania


Sehemu ya watushi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma Ofisi ya Rais – UTUMISHI katika kikao na Naibu Waziri Ofisi Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Regina Qwaray Januari 5, 2026 Dodoma Tanzania.


Monday, January 5, 2026

WATUMISHI WAKUMBUSHWA KUONGEZA UFANISI NA UWAJIBIKAJI KWA MWAKA 2026

Na. Veronica Mwafisi-Dodoma

Tarehe 05 Januari, 2026

Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera, Bw. Cyrus Kapinga amewakumbusha Watumishi wa ofisi hiyo kuongeza ufanisi na uwajibikaji kwa Mwaka 2026 ili kutimiza malengo waliyojiwekea kwa maslahi mapana ya Taifa.

Bw. Kapinga ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa ofisi hiyo katika eneo maalum la mafunzo kwa watumishi hao kwa lengo la kuwajengea uwezo na uelewa wa masuala mbalimbali ya kiutumishi ambayo hufanyika kila siku ya Jumatatu Mtumba Jijini Dodoma.

Bw. Kapinga amewasisitiza Watumishi hao kushirikiana kutekeleza majukumu yao ili kufikia malengo waliyojiwekea katika kutoa huduma bora kwa kila Mtanzania.

“Mwaka uliopita 2025 tulitekeleza majukumu yetu vema na kutimiza malengo tuliyojiwekea, natoa rai kwa mwaka 2026 tushirikiane pia katika kutekeleza majukumu yetu ili Wadau na Wananchi wetu wanufaike na huduma tunazozitoa” alisisitiza Bw. Kapinga.

Kwa upande wake Mwezeshaji wa mafunzo Bw. Mosses Raymond amesema Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora ina majukumu mengi ikiwemo utoaji wa huduma mbalimbali za kiutumishi hivyo, ni muhimu kila mtumishi akajua wajibu wake ili huduma zitakazotolewa kwa Watumishi wa Umma na Wananchi ziwe zenye manufaa.

Aidha Bw. Raymond amesema, ili kuilinda taswira nzuri ya ofisi hiyo ni vizuri kila mtumishi kuendelea kuwa mwadilifu kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo ya Utumishi wa Umma wanapokuwa ndani au nje ya ofisi.

Kadhalika Bw. Raymond amewapongeza Watumishi wa ofisi hiyo kuwasili kwa wakati katika maeneo yao ya kazi jambo linaloonyesha kwamba kila mmoja anajua wajibu wake na kufurahia mazingira wanayofanyia kazi. 

Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera, Bw. Cyrus Kapinga akizungumza wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi watumishi wa ofisi hiyo yanayofanyika kila Jumatatu kwenye Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.


Mwezeshaji wa mafunzo, Bw. Mosses Raymond akiwasilisha mada mbalimbali wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi watumishi wa ofisi hiyo yanayofanyika kila Jumatatu kwenye Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.


Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, wakiwa kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.


Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, wakiwa kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.


Sehemu ya Wakurugenzi na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, wakiwa kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.


Sehemu ya Wakurugenzi na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, wakifuatilia jambo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.


Mkurugenzi Msaidizi wa Ufuatiliaji na Uzingatiaji wa Maadili, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bi. Janet Mishinga akikata keki ya kuukaribisha Mwaka Mpya kwa niaba ya Watumishi wote wa ofisi hiyo mara baada ya kumaliza mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuimarisha utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma. Wanaoshuhudia ni Maafisa wa ofisi hiyo.