Na. James K. Mwanamyoto-Moshi
Tarehe 20 Septemba, 2022
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Deogratius Ndejembi amemuelekeza Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU kuweka kipengere
kwenye mkataba wa waajiriwa wapya 553 wa TAKURURU chenye sharti la kutumikia
miaka mitano katika taasisi hiyo kabla ya kufikiria kuhamia taasisi nyingine
ili kutimiza lengo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia
Suluhu Hassan la kutokomeza vitendo vya rushwa nchini.
Mhe. Ndejembi ametoa maelekezo hayo mjini
Moshi, Mkoani Kilimanjaro, wakati akifunga mafunzo ya Maafisa Uchunguzi na
Wachunguzi Wasaidizi wapya wanaoajiriwa na TAKUKURU, yaliyotolewa katika Shule
ya Polisi Tanzani iliyopo Moshi ili kuwajengea uwezo wa kupambana na vitendo
vya rushwa nchini.
Mhe.
Ndejembi amesema, amelazimika kutoa maelekezo hayo ili kukomesha tabia iliyoibuka
ya baadhi ya watu kuomba kazi yoyote inayotangazwa serikalini na pindi
akiajiriwa anataka kuhamia taasisi nyingine kwa maslahi yake binafsi, wakati
serikali imemuajiri ili kuutumikia umma wa watanzania katika taasisi
aliyopangiwa.
“Ninaelekeza
kwa ajira hizi 553 za TAKUKURU, kiwekwe kipengere kinachoainisha kuwa, ni
lazima waitumikie TAKUKURU si chini ya miaka 5 bila kuhamia taasisi nyingine kwani
serikali imewekeza kiasi kikubwa katika kuwapatia mafunzo na kuwaajiri, hivyo
ni lazima muutumikie umma katika mapambano dhidi ya rushwa ili thamani ya fedha
iliyowekezwa ionekane,” Mhe. Ndejembi amesisitiza.
Mhe.
Ndejembi ameongeza kuwa, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amejipambanua kuichukia
rushwa na hataki kuona maendeleo ya taifa yanakwamishwa na vitendo kwa rushwa,
hivyo amewataka waajiriwa hao wapya wa TAKUKURU kuunga mkono kwa vitendo azma
hiyo ya Mheshimiwa Rais.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Nurdin Babu amesema kuwa Mhe.
Rais amefanya mengi mazuri ikiwa ni pamoja na kutoa ajira hizo 553 za TAKUKURU,
ili kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa nchini na amewataka watakaopangiwa
kwenye mkoa wake wafanye kazi kwa bidii na uadilifu katika kusimamia fedha za
miradi ya maendeleo ambazo Mhe. Rais amezitoa kwa ajili ya kuwanufaisha wananchi
mkoani Kilimanjaro.
Naye,
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Kamishna wa Polisi, Salum Hamduni amesema
waliohitimu mafunzo hayo watapangiwa vituo vya kazi na kuwataka kila mmoja
akubali kituo atakachopangiwa kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais
Samia Suluhu Hassan za kupambana na rushwa.
“Sitarajii
kuona vimemo vya kuniomba niwabadilishie vituo vya kazi kwani wakati mnaomba
ajira na wakati mnafanya usaili tuliwauliza kama mko tayari kufanya kazi popote
nchini, na kila mmoja wenu alisema kuwa yuko tayari kufanya kazi sehemu yoyote katika
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” ACP Hamduni amesisitiza.
Serikali
ya Awamu ya Sita, chini ya uongozi wa Mhe. Samia Suluhu Hassan inaendelea na
jitihada za kuijengea uwezo kiutendaji Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU) kwa kuipatia rasilimaliwatu yenye tija katika kuendeleza mapambano
dhidi ya vitendo vya rushwa nchini ambavyo vinakwamisha maendeleo ya taifa.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Deogratius Ndejembi akikagua gwaride la wahitimu wa mafunzo ya Maafisa Uchunguzi na Wachunguzi Wasaidizi wapya
wanaoajiriwa na TAKUKURU kabla ya kufunga mafunzo hayo mjini Moshi.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Deogratius Ndejembi akikaribishwa kukagua gwaride la wahitimu wa mafunzo ya Maafisa Uchunguzi na Wachunguzi Wasaidizi wapya
wanaoajiriwa na TAKUKURU kabla ya kufunga mafunzo hayo mjini Moshi.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Deogratius Ndejembi akipokea heshima ya gwaride la wahitimu wa mafunzo ya Maafisa Uchunguzi na Wachunguzi Wasaidizi wapya
wanaoajiriwa na TAKUKURU wakati akifunga mafunzo hayo mjini Moshi.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Deogratius Ndejembi akishuhudia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakionyeshwa na
wahitimu wa mafunzo ya Maafisa Uchunguzi na
Wachunguzi Wasaidizi wapya wanaoajiriwa na TAKUKURU (hawapo pichani) kabla ya
kufunga mafunzo hayo mjini Moshi. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Kamishna wa
Polisi, Salum Hamduni na kushoto kwake ni Mkuu wa Chuo cha Polisi Tanzania SACP Ramadhani Mungi.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Deogratius Ndejembi akifunga mafunzo ya Maafisa
Uchunguzi na Wachunguzi Wasaidizi wapya wanaoajiriwa na TAKUKURU baada ya
kuhitimu mafunzo hayo katika Chuo cha Polisi Tanzania, mjini Moshi.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Deogratius Ndejembi akifunga mafunzo ya Maafisa
Uchunguzi na Wachunguzi Wasaidizi wapya wanaoajiriwa na TAKUKURU baada ya
kuhitimu mafunzo hayo katika Chuo cha Polisi Tanzania, mjini Moshi.
Sehemu
ya wahitimu wa mafunzo ya Maafisa Uchunguzi na
Wachunguzi Wasaidizi wapya wanaoajiriwa na TAKUKURU wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi
wakati akifunga mafunzo hayo mjini Moshi.
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Nurdin Babu akitoa salamu za mkoa wake kabla ya
kumkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi kufunga
mafunzo ya Maafisa Uchunguzi na Wachunguzi Wasaidizi wapya wanaoajiriwa na
TAKUKURU mjini Moshi.
Mkurugenzi
Mkuu wa TAKUKURU, Kamishna wa Polisi, Salum Hamduni akielezea lengo la mafunzo ya Maafisa Uchunguzi na Wachunguzi Wasaidizi wapya
wanaoajiriwa na TAKUKURU yaliyofanyika katika Chuo cha Polisi Tanzania mjini
Moshi kabla ya Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Deogratius Ndejembi kufunga mafunzo hayo.