Na. Mary Mwakapenda-Manyoni
Tarehe 03 Septemba,2020
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Singida imefanikiwa kuokoa kiasi cha Tsh. 199,559,254/= kufuatia operesheni mbalimbali zilizofanywa ili kuzuia na kupambana na vitendo vya rushwa mkoani humo katika kipindi cha kuanzia Julai 2019 hadi Juni 2020.
Hayo yamesemwa jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst)
Mhe. George H. Mkuchika wakati akimkaribisha Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai kuzindua jengo la Ofisi ya TAKUKURU
Wilaya ya Manyoni mkoani Singida.
Mhe. Mkuchika ameyataja baadhi ya maeneo ambayo operesheni hiyo iliyalenga
kuwa ni pamoja na mikopo umiza ambapo kiasi cha Tsh. 58,150,000/= kiliokolewa, kwa upande wa mapato yatokanayo na
usimamizi wa madini, kiasi cha Tsh.
44,623,254/= kiliokolewa, sanjari na hayo, kiliokolewa kiasi cha Tsh. 11,456,500/= kutokana na mapato ya
usimamizi wa minada, na kiasi cha Tsh.
85,329,500/= kilirudishwa kutoka kwa wanachama wa vyama vya ushirika.
Mhe. Mkuchika amefafanua kuwa, jitihahada zote hizi zilizofanywa na zinazoendelea
kufanywa na TAKUKURU zinatokana na weledi, ujasiri na uzalendo uliopo katika
kushughulikia tatizo la rushwa nchini, hivyo ameitaka TAKUKURU kuendelea na
kasi hiyo ili kudhibiti vitendo vya rushwa na ufisadi nchini.
Katika eneo la utoaji elimu dhidi ya vitendo vya rushwa, Mhe. Mkuchika
ameanisha kuwa, TAKUKURU imefanikiwa kufungua na kuimarisha klabu 234 za
Wapinga Rushwa mashuleni na vyuoni na kutoa semina pamoja na mikutano ya
hadhara 225.
Aidha, Mhe. Mkuchika amemuahidi Mhe. Ndugai kujenga Ofisi ya TAKUKURU
Wilaya ya Kongwa ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa tarehe 22 Julai, 2020
wakati akifungua jengo la Ofisi ya TAKUKURU Wilaya ya Chamwino na kuongeza
kuwa, hatua hii inadhirisha nia ya dhati ya Serikali ya kupambana na vitendo
vya rushwa nchini.
Jengo la Ofisi ya TAKUKURU la Wilaya ya Manyoni ni mojawapo ya majengo saba
ambayo Mhe. Rais Magufuli alitakiwa kuyafungua kwa pamoja tarehe 22 Julai, 2020
wakati akifungua jengo la Ofisi ya TAKUKURU Wilaya ya Chamwino, Dodoma. Hata
hivyo, aliweka utaratibu wa kuyafungua kwa nyakati tofauti na kumuelekeza Mhe.
Ndugai kulifungua jengo hilo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Kapt (Mst) George Mkuchika
akitoa maelezo kuhusu jengo la TAKUKURU Wilaya ya Manyoni kabla ya kumkaribisha
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai kuzungumza
na wananchi na kulizindua jengo hilo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Kapt (Mst) George Mkuchika
akimkaribisha Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job
Ndugai kuzungumza na wananchi kabla ya kuzindua jengo la Ofisi ya TAKUKURU
Wilaya ya Manyoni mkoani Singida.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai
akizungumza na wananchi wilayani Manyoni kabla ya kuzindua jengo la Ofisi
ya TAKUKURU Wilaya ya Manyoni mkoani Singida.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai
(kushoto) akisoma kibao cha ufunguzi wa jengo baada ya kuzindua jengo la Ofisi
ya TAKUKURU Wilaya ya Manyoni mkoani Singida jana. Wanaoshuhudia ni Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) George Mkuchika na Mkuu wa Wilaya
ya Manyoni, Bibi Rahabu Magwisa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) George Mkuchika akiipongeza Klabu ya Wapinga Rushwa ya Shule ya Sekondari ya Mlewa Wilayani Manyoni wakati wakiimba wimbo wa mapambano dhidi ya rushwa kwenye hafla ya uzinduzi wa jengo la Ofisi ya TAKUKURU Wilaya ya Manyoni mkoani Singida.
No comments:
Post a Comment