Thursday, September 27, 2018

MHE. MKUCHIKA ASHUHUDIA MAFANIKIO YA WANUFAIKA WA TASAF KATA YA MUHUNGA WILAYANI KASULU



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akizungumza na wananchi na wanufaika wa TASAF kata ya Muhunga wilayani Kasulu, alipowatembelea ili kujionea utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini nchini.

Baadhi ya wanakijiji na wanufaika wa TASAF wa kata ya Muhunga wilayani Kasulu wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) (hayupo pichani) alipoitembelea kata hiyo ili kujionea utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini nchini.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) na Mbunge wa Kasulu Mjini (CCM), Mhe. Daniel Nsanzugwanko (Mb) wakiwa katika picha ya pamoja na Bi. Monica Jackson Mavuli mnufaika wa TASAF kata ya Muhunga wilayani Kasulu mbele ya nyumba ya mnufaika huyo iliyojengwa kwa fedha za ruzuku ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini nchini.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akiwa na mmoja wa wanufaika wa TASAF kata ya Muhunga wilayani Kasulu mbele ya nyumba ya mnufaika huyo iliyojengwa kwa fedha za ruzuku ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini nchini.

No comments:

Post a Comment