Thursday, June 22, 2017

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAFANYA MKUTANO KAZI NA WATENDAJI WA MKOA WA RUVUMA KUADHIMISHA YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2017

Katibu Tawala, Mkoa wa Ruvuma Bw. Hassan Bendeyeko akiwasilisha taarifa ya utendaji kuhusu mkoa wake wakati wa mkutano kazi uliowahusisha watendaji wa mkoa wa Ruvuma na Ofisi ya Rais - Utumishi wakati wa  Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017.

Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za mkoa wa Ruvuma wakijitambulisha wakati wa mkutano kazi uliowakutanisha na watendaji wa Ofisi ya Rais-Utumishi wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017 mkoani Ruvuma.

Sehemu ya watendaji wa Serikali mkoani Ruvuma wakisikiliza  hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma  na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) kuhusu uwajibikaji katika Utumishi wa Umma , iliyosomwa kwa niaba yake na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Issa Ngimba  mkoani Ruvuma ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2017.

Baadhi ya watendaji na Watumishi wa Umma mkoani Ruvuma wakiwa katika mkutano kazi uliowakutanisha na watendaji wa Ofisi ya Rais-Utumishi  wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017  mjini Songea.


Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma,  Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Issa Ngimba akisoma hotuba kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) ya kuhimiza uwajibikaji kwa viongozi na watumishi wa umma mkoani Ruvuma wakati wa kikao kazi cha  Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2017.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Bw. Hassan Bendeyeko akiwa na viongozi wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakati wa mkutano kazi wa Ofisi ya Rais-Utumishi na watendaji wa mkoa wa Ruvuma ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017.


Afisa Utumishi Mwandamizi wa Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Bw. Thadei Kimati akifafanua kuhusu taratibu zinazohusu masuala ya kiutumishi   kwa Watendaji na  watumishi wa umma mkoani Ruvuma  ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2017.

No comments:

Post a Comment