Monday, June 19, 2017

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YATEMBELEA HALMASHAURI YA WILAYA YA WANGING’OMBE KUHIMIZA UWAJIBIKAJI IKIWA NI SEHEMU YA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2017

Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma  Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Ibrahim Mahumi akitoa ufafanuzi kuhusu taratibu zinazohusu  menejimenti ya  Rasilimaliwatu serikalini kwa viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe katika Ofisi za  Halmashauri hiyo  ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2017. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe Bi. Amina Kiwanuka.
 

Viongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakizungumza masuala ya kiutumishi na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo  ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma mwaka 2017.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe, Bi. Amina Kiwanuka akieleza utekelezaji wa masuala ya kiutumishi katika eneo lake la   kwa Viongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma waliomtembelea ofisini kwake leo alasiri kuhimiza uwajibikaji ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2017.


Mkuu wa Idara ya Utumishi na Utawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe Bw. Abdullfariq Mkata (wa pili kulia) akitoa taarifa  ya kiutendaji ya Idara yake kwa Viongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma walipoitembelea Halmashauri hiyo leo kuhimiza uwajibikaji ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2017.


Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma wa Ofisi ya Rais,Menenimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Issa Ng’imba akitoa ufafanuzi kuhusu masuala ya kiutumishi  kwa Mkurugenzi  wa  Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe Bi. Amina Kiwanuka ofisini kwa mkurugenzi huyo leo  ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2017. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bi. Amina Kiwanuka akisikiliza kwa makini.

No comments:

Post a Comment