Thursday, June 22, 2017

KATIBU MKUU-UTUMISHI AWATAKA WAAJIRI KUFANYA MABORESHO YA TAARIFA ZA WATUMISHI MARA TU MABADILIKO YANAPOTOKEA ILI KUWA NA TAARIFA SAHIHI ZA KIUTUMISHI

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (wa kwanza kulia), akifuatilia taarifa ya utekelezaji ya Mkoa wa Shinyanga iliyokuwa ikiwasilishwa na Katibu Tawala Msaidizi Rasilimaliwatu wa Mkoa wa Shinyanga, Bw. Alfred Shayo (aliyesimama) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Sera, Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mathias Kabunduguru.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akisisitiza jambo kwa Watendaji na watumishi wa Mkoa wa Shinyanga wakati wa kikao kazi na watumishi hao ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017. Kushoto kwake ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Bw. Albert Msovela na kulia ni Mkurugenzi wa Sera, Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mathias Kabunduguru.

Sehemu ya Watendaji na Watumishi wa Mkoa wa Shinyanga wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa kikao kazi na watumishi hao ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017.

Katibu Msaidizi Tume ya Utumishi wa Walimu Wilaya ya Kahama, Bw. Bashemela Seif, akitoa maoni wakati wa kikao kazi cha Watendaji na Watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Shinyanga na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017.

Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Bw. Stephen Magoiga, akiwasilisha hoja wakati wa kikao kazi cha Watendaji na Watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Shinyanga na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017.

Afisa Tawala Mwandamizi kutoka Ofisi ya Rais – Utumishi, Bw. Leonard Tumua, akifafanua jambo kwa Watendaji na watumishi wa Mkoa wa Shinyanga wakati wa kikao kazi na watumishi hao ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017. Wa kwanza Kushoto kwake ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro na katikati ni Mkurugenzi wa Sera, Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mathias Kabunduguru.

Mkurugenzi wa Sera, Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mathias Kabunduguru. akifafanua jambo kwa Watendaji na watumishi wa Mkoa wa Shinyanga wakati wa kikao kazi na watumishi hao ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro na Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Bw. Albert Msovela.

No comments:

Post a Comment