Serikali kupitia Ofisi ya Rais ,Menejimenti ya Utumishi wa
Umma, imeendesha mafunzo ya Kanzidata ya Fomu za Serikali yanayolenga kukabilina na changamoto ambazo
zimekuwa zikijitokeza katika usimamizi wa fomu hizo.
Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi, Ofisi ya
Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw.Mick Kiliba akifungua mafunzo hayo
katika Ukumbi wa Utumishi alisema kuwa mafunzo hayo ni muhimu sana katika usimamizi wa Fomu za
Serikali na utoaji huduma kwa ujumla .
“Imebainika kuwa zoezi zima la usimamizi wa Fomu za Serikali lina upungufu mkubwa katika usimamizi ikiwa ni pamoja taasisi kuibua fomu mpya , kuhuisha na kuanza kutumia bila ya ridhaa ya Katibu
Mkuu Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi
Umma” Bw. Kiliba alisema.
Aliongeza “ Jukumu la usimamizi wa utendaji wa serikali liko
chini ya Ofisi ya Rais –Utumishi, Fomu
za Serikali ni njia mojawapo ya kutekeleza jukumu hili na hivyo uthibiti wa fomu za serikali ni jambo muhimu
kuzingatiwa .” Mkurugenzi Kiliba alisisitiza
na kusema kuwa katika uthibiti huo
General Orders ( G.O.C 48)
imeelekeza kuwa mapendekezo ya kuibua
Fomu mpya na kuhuisha fomu zilizopo yapate ushauri
na kibali kutoka Utumishi.
Mkurugenzi Kiliba aliendelea kufafanua kuwa kuna taasisi za serikali zinaenda kinyume na
taratibu kwa kuibua na kutumia fomu
tofauti na zile zinazokubalika katika
kutoka huduma husika, kutumia fomu
zilizopitwa na wakati na kutotambua idadi ya fomu zinazotumika katika taasisi
husika na kutosimamia ipasavyo.
“ Katika ufuatiliaji wa utekelezaji wa mifumo ya viwango vya
utendaji uliofanyika Mei
mwaka 2015 na Mei 2016 katika
Idara zinazojitegemea na Wakala za Serikali kiwango cha usimamizi wa fomu za serikali ni wastani wa asilimia 27 na 53 “ Mkurugenzi Kiliba
aliainisha.
Alisema kutokana na
hali hiyo, Serikali imeona ipo haja ya
kuwa na Kanzidata ya Fomu za Serikali (Government
Forms Database) itakayosaidia kuweka kumbukumbu muhimu na kuratibu
usimamizi wa Fomu ili kufikia
azma ya kuleta ufanisi katika utendaji serikalini.
Akitoa
mafunzo hayo kwa washiriki kutoka katika taasisi mbalimbali za Serikali
Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi, Sehemu ya Mifumo na Viwango
vya Utendaji Kazi – Utumishi Bi.Veila Shoo alisema kuwa Fomu hizo za
serikali ni zile ambazo hutumika
kukamilisha taratibu mbalimbali
za kiutumishi na usimamizi wa fedha katika Utumishi wa Umma .
Mafunzo hayo ya siku moja yamehudhuriwa na wawakilishi wa wizara zote Serikali
No comments:
Post a Comment