Wednesday, August 3, 2016

SERIKALI YAPOKEA WATAALAM WA KUJITOLEA KUTOKA JAPANI


Naibu Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais-Utumishi  na Utawala Bora Bi. Susan Mlawi akimkaribisha Mwakilishi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) nchini Tanzania Bw. Toshio Nagase baada ya kuwapokea Wataalam  sita wa kujitolea mapema leo kutoka shirika hilo ambao watafanya kazi katika maeneo mbalimbali nchini kwenye sekta za Elimu na Maendeleo ya Jamii.

Naibu Katibu Mkuu- Ofisi ya Rais - Utumishi na Utawala Bora Bi. Susan Mlawi, akizungumza na Wataalam wa kujitolea kutoka Japan mapema leo  ambao watafanya kazi  katika sekta za Elimu na Maendeleo ya Jamii, katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Pwani na Mtwara.

Mwakilishi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) nchini Tanzania Bw. Toshio Nagase (kulia) akimueleza jambo Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Utumishi na Utawala Bora Bi. Susan Mlawi,mapema leo  kuhusu Wataalam  wa kujitolea kutoka shirika hilo waliokuja nchini kutoa huduma katika sekta za Elimu na Maendeleo ya Jamii .

No comments:

Post a Comment