Thursday, August 11, 2016

SERIKALI YAWAAGA WATANZANIA 12 WALIOPATA FURSA YA MAFUNZO NCHINI JAPANI

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza katika hafla fupi ya kuwaaga watumishi waliopata fursa ya kuhudhuria mafunzo ya Shahada ya Uzamili nchini Japani chini ya ufadhili wa Serikali ya Japani kupitia mpango wa ABE Initiative, iliyofanyika nyumbani kwa Balozi wa Japani nchini.
Balozi wa Japani nchini Tanzania Bw. Masaharu Yoshida akizungumza katika hafla fupi ya kuwaaga watumishi waliopata fursa ya kuhudhuria mafunzo ya Shahada ya Uzamili nchini Japani chini ya ufadhili wa Serikali ya Japani kupitia mpango wa ABE Initiative, iliyofanyika nyumbani kwa Balozi huyo.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi (12)waliopata fursa ya kuhudhuria mafunzo ya Shahada ya Uzamili nchini Japani chini ya ufadhili wa Serikali ya Japani kupitia mpango wa ABE Initiative awamu ya tatu (03), mara baada ya hafla fupi ya kuwaaga watumishi hao iliyofanyika nyumbani kwa Balozi wa Japani nchini.
Watumishi (12) waliopata fursa ya kuhudhuria mafunzo ya Shahada ya Uzamili nchini Japani chini ya ufadhili wa Serikali ya Japani kupitia mpango wa ABE Initiative awamu ya tatu (waliosimama) wakijitambulisha mbele ya  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro ( wa pili kulia mstari wa mbele) na Waandishi wa Habari (kushoto) wakati wa kipindi cha maswali na majibu mara baada ya hafla fupi ya kuwapongeza na kuwaaga watumishi hao iliyofanyika nyumbani kwa Balozi wa Japani nchini. 
Mwandishi wa habari wa gazeti la Dailynews Bi. Hilda Mhagama  (wa kwanza kushoto) akiuliza swali kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro( wa pili kulia mstari wa mbele) wakati wa kipindi cha maswali na majibu mara baada ya hafla fupi ya kuwapongeza na kuwaaga watumishi hao iliyofanyika nyumbani kwa Balozi wa Japani nchini.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro( wa pili kulia mstari wa mbele) akijibu swali aliloulizwa na Mwandishi wa habari wa gazeti la Dailynews Bi. Hilda Mhagama  (wa kwanza kushoto)  wakati wa kipindi cha maswali na majibu mara baada ya hafla fupi ya kuwapongeza na kuwaaga watumishi waliopata fursa ya kuhudhuria mafunzo ya Shahada ya Uzamili nchini Japani chini ya ufadhili wa Serikali ya Japani kupitia mpango wa ABE Initiative awamu ya tatu, iliyofanyika nyumbani kwa Balozi wa Japani nchini.
Balozi wa Japani nchini Tanzania Bw. Masaharu YOSHIDA (wa pili kulia) akijibu swali aliloulizwa na mwandishi wa habari, wakati wa kipindi cha maswali na majibu mara baada ya hafla fupi ya kuwapongeza na kuwaaga watumishi waliopata fursa ya kuhudhuria mafunzo ya Shahada ya Uzamili nchini Japani chini ya ufadhili wa Serikali ya Japani kupitia mpango wa ABE Initiative awamu ya tatu, iliyofanyika nyumbani kwa Balozi huyo.



No comments:

Post a Comment