Monday, August 29, 2016

MHE. KAIRUKI AWATA WATUMISHI WA UMMA NCHINI KUJIJENGEA UWEZO KATIKA MAENEO YATAKAYO HARAKISHA MAENDELEO‏

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akitoa ufafanuzi wakati wa kipindi cha TUNATEKELEZA kilichorushwa na Runinga ya Taifa (TBC-1). Kushoto ni muongozaji kipindi hicho Bi. Eshe Muhidin.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akisisitiza jambo katika  kipindi cha TUNATEKELEZA kilichorushwa na Runinga ya Taifa (TBC-1). Mhe. Kairuki aliainisha kuwa wale wanaotarajia kuomba ajira Serikalini wawe na subira wakati zoezi la uhakiki wa taarifa za kiutumishi likikamilishwa. Kushoto ni muongozaji wa kipindi hicho  Bi. Eshe Muhidin waTBC. 

Muongozaji wa kipindi cha TUNATEKELEZA Bi. Eshe Muhidin (kushoto) akiuliza swali kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) wakati wa kipindi cha TUNATEKELEZA kilichorushwa na Runinga ya Taifa (TBC-1). Miongoni mwa aliyosema Mhe. Kairuki ni wito kwa Watumishi wa Umma kujiendeleza katika maeneo yenye tija kwa Taifa ili kufikia malengo ya nchi.

TUMEKAMILISHA: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Muongozaji wa kipindi cha TUNATEKELEZA Bi. Eshe Muhidin (kushoto) baada ya kukamilisha kurusha kipindi mmbashara (live) katika studio za Runinga ya Taifa TBC-1.

Tuesday, August 23, 2016

UTEKELEZAJI WA AGIZO LA KUONDOA WATUMISHI WASIOSTAHILI KUWEPO KATIKA ORODHA YA MALIPO YA MSHAHARA SERIKALINI


MATUKIO KATIKA PICHA: KIKAO KAZI CHA WAZIRI KAIRUKI NA WATUMISHI WA UMMA MKOANI KAGERA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akipitia hoja ya mmoja wa washiriki wa kikao kazi mkoani Kagera
Ufafanuzi wa hoja na kero mbalimbali mkoani Kagera ukitolewa na watalaam wakati wa kikao kazi
Bw. Welanika Sylivester akiwasilisha tatizo kuhusu kutopandishwa cheo kwa muda mrefu
Flora Kaigi akiwasilisha hoja kuhusu utaratibu wa kupandishwa daraja
Mmoja kati ya washiriki akiwasilisha hoja kuhusu walimu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akiongea na Watumishi wa Umma mkoani Kagera kuhusu masuala mbalimbali ya kiutumishi na wajibu wao wa kutoa huduma bora kwa wateja wa ndani na nje wakiwamo wananchi.

Monday, August 22, 2016

MHE. KAIRUKI ASIKILIZA KERO NA MAONI YA WATUMISHI WA UMMA MKOANI KAGERA

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu (kushoto) akiwasilisha taarifa ya Mkoa wake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (kulia).


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (kushoto) akitoa maelekezo kwa uongozi wa Mkoa wa Kagera  ikiwemo  kusafisha taarifa za watumishi mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu (kulia) kuwasilisha taarifa ya Mkoa wake.
Baadhi ya Watumishi wa Umma wa Mkoa wa Kagera wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha waziri huyo na watumishi hao kilichofanyika Mkoani Kagera.

Mmoja wa watumishi wa  Umma  wa Mkoa wa Kagera akiwasilisha malalamiko yake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha waziri huyo na watumishi hao kilichofanyika Mkoani Kagera.

MHE. KAIRUKI AZITAKA TAASISI 145 AMBAZO HAZIJAWASILISHA TAARIFA YA WATUMISHI HEWA KUWASILISHA KABLA YA TAREHE 26/08/2016





Sunday, August 21, 2016

WAZIRI KAIRUKI KUKUTANA NA WATUMISHI WA UMMA MKOANI KAGERA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) kukutana na Watumishi wa Umma mkoani Kagera, Jumatatu tarehe 22 Agusti 2016.

Pichani: Mhe. Kairuki (kushoto) akipokewa na baadhi ya watendaji Mkoani Kagera, katikati ni Katibu Tawala -Mkoa wa Kagera Bw. Amantius Msole.

Saturday, August 20, 2016

MHE. KAIRUKI AFUATILIA ZOEZI LA UHAKIKI WA WATUMISHI HEWA SERIKALINI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.  Angellah J.  Kairuki (Mb) akitoa taarifa kwa Vyombo vya Habari  kuhusu zoezi la kuondoa watumishi hewa katika orodha ya malipo ya mishahara serikalini ofisini kwake

Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.  Angellah J. Kairuki (Mb)  alipozungumza nao ofisini kwake jijini Dar es Salaam

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.  Angellah J.  Kairuki (Mb) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawako pichani) kuhusu utekelezaji wa agizo la kuondoa watumishi hewa katika orodha ya malipo ya mishahara Serikalini ofisini kwake 




Thursday, August 11, 2016

SERIKALI YAWAAGA WATANZANIA 12 WALIOPATA FURSA YA MAFUNZO NCHINI JAPANI

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza katika hafla fupi ya kuwaaga watumishi waliopata fursa ya kuhudhuria mafunzo ya Shahada ya Uzamili nchini Japani chini ya ufadhili wa Serikali ya Japani kupitia mpango wa ABE Initiative, iliyofanyika nyumbani kwa Balozi wa Japani nchini.
Balozi wa Japani nchini Tanzania Bw. Masaharu Yoshida akizungumza katika hafla fupi ya kuwaaga watumishi waliopata fursa ya kuhudhuria mafunzo ya Shahada ya Uzamili nchini Japani chini ya ufadhili wa Serikali ya Japani kupitia mpango wa ABE Initiative, iliyofanyika nyumbani kwa Balozi huyo.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi (12)waliopata fursa ya kuhudhuria mafunzo ya Shahada ya Uzamili nchini Japani chini ya ufadhili wa Serikali ya Japani kupitia mpango wa ABE Initiative awamu ya tatu (03), mara baada ya hafla fupi ya kuwaaga watumishi hao iliyofanyika nyumbani kwa Balozi wa Japani nchini.
Watumishi (12) waliopata fursa ya kuhudhuria mafunzo ya Shahada ya Uzamili nchini Japani chini ya ufadhili wa Serikali ya Japani kupitia mpango wa ABE Initiative awamu ya tatu (waliosimama) wakijitambulisha mbele ya  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro ( wa pili kulia mstari wa mbele) na Waandishi wa Habari (kushoto) wakati wa kipindi cha maswali na majibu mara baada ya hafla fupi ya kuwapongeza na kuwaaga watumishi hao iliyofanyika nyumbani kwa Balozi wa Japani nchini. 
Mwandishi wa habari wa gazeti la Dailynews Bi. Hilda Mhagama  (wa kwanza kushoto) akiuliza swali kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro( wa pili kulia mstari wa mbele) wakati wa kipindi cha maswali na majibu mara baada ya hafla fupi ya kuwapongeza na kuwaaga watumishi hao iliyofanyika nyumbani kwa Balozi wa Japani nchini.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro( wa pili kulia mstari wa mbele) akijibu swali aliloulizwa na Mwandishi wa habari wa gazeti la Dailynews Bi. Hilda Mhagama  (wa kwanza kushoto)  wakati wa kipindi cha maswali na majibu mara baada ya hafla fupi ya kuwapongeza na kuwaaga watumishi waliopata fursa ya kuhudhuria mafunzo ya Shahada ya Uzamili nchini Japani chini ya ufadhili wa Serikali ya Japani kupitia mpango wa ABE Initiative awamu ya tatu, iliyofanyika nyumbani kwa Balozi wa Japani nchini.
Balozi wa Japani nchini Tanzania Bw. Masaharu YOSHIDA (wa pili kulia) akijibu swali aliloulizwa na mwandishi wa habari, wakati wa kipindi cha maswali na majibu mara baada ya hafla fupi ya kuwapongeza na kuwaaga watumishi waliopata fursa ya kuhudhuria mafunzo ya Shahada ya Uzamili nchini Japani chini ya ufadhili wa Serikali ya Japani kupitia mpango wa ABE Initiative awamu ya tatu, iliyofanyika nyumbani kwa Balozi huyo.



Wednesday, August 10, 2016

WASIMAMIZI WA MIRADI YA TEHAMA SERIKALINI WAPEWA MAFUNZO

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. Arnold Mathoyo akieleza utaratibu wa mafunzo ya TEHAMA kwa washiriki wanaosimamia miradi ya TEHAMA chini ya Mradi wa Miundombinu ya Mawasiliano (RCIP) Tanzania katika ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Dodoma.

Washiriki wa mafunzo kuhusu TEHAMA wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Susan Mlawi (hayupo pichani).

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Susan Mlawi akisisitiza jambo wakati akifungua mafunzo kwa wataalam wa TEHAMA wanaosimamia miradi chini ya Mradi wa Miundombinu ya Mawasiliano (RCIP) Tanzania katika ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Susan Mlawii akifungua mafunzo kwa wataalam wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wanaosimamia miradi chini ya Mradi wa Miundombinu ya Mawasiliano (RCIP) Tanzania katika ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Dodoma.




Tuesday, August 9, 2016

MHE. KAIRUKI AWATAKA WATUMISHI WA OFISI YAKE KUWA MFANO WA KUIGWA KATIKA KUTOA HUDUMA BORA KWA UMMA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akisisitiza jambo kwa watumishi wa ofisi yake wakati wa kikao kazi cha robo mwaka cha waziri huyo na watumishi wa ofisi yake kilichofanyika Utumishi leo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na watumishi wa ofisi yake wakati wa kikao kazi cha robo mwaka cha waziri huyo na watumishi wa ofisi yake kilichofanyika Utumishi leo. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Utumishi Bw. Kamugisha Rufulenge.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Utumishi Dkt. Laurean Ndumbaro (katikati) akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi cha robo  mwaka cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) na watumishi wa ofisi yake kilichofanyika Utumishi leo. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) na kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Bw. Aloyce Msigwa.

Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha robo mwaka cha waziri huyo na watumishi wa ofisi yake kilichofanyika Utumishi leo.
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Bw. Aloyce Msigwa (kushoto) akitoa ufafanuzi wa masuala ya kiutumishi wakati wa kikao kazi cha robo  mwaka cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (kulia) na watumishi wa ofisi yake kilichofanyika Utumishi leo.Katikati ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Utumishi Dkt. Laurean Ndumbaro akisikiliza kwa makini.
Mtumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. Victor Kitu (aliyesimama) akiwasilisha malalalamiko yake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha robo mwaka cha waziri huyo na watumishi wa ofisi yake kilichofanyika Utumishi leo.