Saturday, December 12, 2015

MHE. KAIRUKI AANZA KAZI RASMI OFISI YA RAIS-UTUMISHI NA UTAWALA BORA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli  akimuapisha Ndg. Angellah Jasmine Kairuki kuwa Waziri wa Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ikulu jijini Dar es Salaam.



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Anjella Kairuki (Mb) (wa pili kutoka kushoto) akiwasili ofisini na kulakiwa na watendaji wa ofisi yake mara baada ya kuapishwa. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Bw. Tixon Nzunda.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Anjella Kairuki (Mb) akiweka saini katika kitabu cha wageni baada ya kuwasili rasmi katika ofisi yake.

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- Utumishi na Utawala Bora Bw. Tixon Nzunda (aliyesimama) akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Anjella Kairuki (wa kwanza kutoka kulia) kuongea na watendaji wa ofisi yake baada ya kuapishwa kushika wadhifa huo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Anjella Kairuki (Mb) (kulia) akizungumza na watendaji wa Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora mara baada kufika ofisini kwake kuanza kazi.

No comments:

Post a Comment