Thursday, December 31, 2015

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAWATAHADHARISHA WANANCHI KUHUSU UTAPELI


MHE. KAIRUKI ATEMBELEA WAKALA YA SERIKALI MTANDAO NA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akishuhudia sehemu ya kusimamia mtandao wa mawasiliano wa Serikali alipotembelea Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akizungumza na vyombo vya habari alipotembelea Wakala ya Serikali Mtandao (eGA)

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akishuhudia Mkongo wa Mawasiliano wa Taifa alipotembelea Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akizungumza na vyombo vya habari alipokitembelea Chuo cha Utumishi wa Umma (Magogoni)

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma alipokitembelea

Add caption

Wednesday, December 30, 2015

MHE. KAIRUKI AENDELEA NA ZIARA KUZITEMBELEA TAASISI ZILIZO CHINI YA OFISI YAKE

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) (wa pili kulia) akizungumza na watumishi wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma alipoitembelea ofisi hiyo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) (kushoto) akimsikiliza Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bi. Claudia Mpangala alipoitembelea ofisi hiyo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) (kushoto) akiwahimiza watumishi wa  Tume ya Utumishi wa Umma kuwajibika alipoitembelea ofisi hiyo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akitazama nyaraka inayoandaliwa kutunzwa katika nakala laini (soft copy) alipoitembelea Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) (kulia) akitazama moja ya kifaa cha kutunzia kumbukumbu  alipoitembelea Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa 

Tuesday, December 29, 2015

WATUMISHI WA UMMA WATAKIWA KUZALIWA UPYA KIUTENDAJI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – UTUMISHI na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akishuhudia mfumo wa maombi ya kazi (recruitment portal) unavyofanya kazi alipotembelea ofisi ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Daudi Xavier (kulia) akieleza majukumu ya ofisi yake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – UTUMISHI na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) alipoitembelea ofisi hiyo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – UTUMISHI na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akiwahimiza watumishi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kufanya kazi kwa uadilifu alipoitembelea ofisi hiyo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – UTUMISHI na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) (kulia) akizungumza na watumishi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma alipoitembelea ofisi hiyo.

Tuesday, December 22, 2015

WAZIRI KAIRUKI AKUTANA NA WATUMISHI WA IDARA YA HUDUMA ZA TEHAMA -UTUMISHI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) (kushoto), akipewa ufafanuzi kuhusu kazi za Idara ya Huduma za TEHAMA-Utumishi na Mkurugenzi wa Idara hiyo Bw.Priscus Kiwango (aliyesimama). 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) (kulia), akipewa ufafanuzi kuhusu kazi za Idara ya Huduma za TEHAMA-Utumishi na Mkurugenzi wa Idara hiyo Bw.Priscus Kiwango (aliyesimama).

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akitoa maelekezo kwa watumishi wa Idara ya Huduma za TEHAMA-Utumishi.

Monday, December 21, 2015

WANAOTAKIWA KUSTAAFU WASIPEWE MIKATABA YA KUENDELEA NA KAZI SERIKALINI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akitoa maelekezo kwa watumishi wa Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu-Utumishi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akizungumza na watumishi wa Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu-Utumishi.



Friday, December 18, 2015

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb), alipofanya kikao na Watumishi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri Kazi -UTUMISHI.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) (katikati), alipofanya kikao na Watumishi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri Kazi -UTUMISHI.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) (kushoto), akitoa maelekezo kwa Watumishi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri Kazi -UTUMISHI.



Serikali kuwachukulia hatua watumishi waliobainika kutumia vyeti vya kughushi


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) ameiagiza Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu-UTUMISHI kuwachukulia hatua watumishi waliobainika kutumia vyeti visivyo vyao kupata ajira Serikalini.
Mhe. Kairuki aliyasema hayo jana alipotembelea Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu–UTUMISHI ikiwa ni muendelezo wa ratiba yake ya kutembelea Idara/Vitengo vya Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
“Watumishi wote waliobainika kupitia Mfumo Shirikishi wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS) kutumia vyeti visivyo halali kwao wachukuliwe hatua stahiki” Mhe. Kairuki amesema.
 Aidha, Mhe. Kairuki amemtaka Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu-UTUMISHI Bw. Emmanuel Mlay kutafuta Ufumbuzi wa kumalizana na tatizo la watumishi wanaotumia vyeti vya kughushi.
“Muwasilishe vyeti vyao Baraza la Mitihani kwa ajili ya uhakiki na baada ya uhakiki muwachukulie hatua stahiki watumishi wanaoonekana kutumia vyeti visivyo halali kwao” Mhe. Waziri alisisitiza.
Naye, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu-UTUMISHI Bw. Leonard Mchau alisema kuwa Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma imehakiki jumla ya watumishi 704 ambao kati ya hao watumishi 219 baada ya vyeti vyao kuhakikiwa na Baraza la Mitihani wamegundulika kuwa waliajiriwa kwa vyeti vya kughushi.
Bw. Mchau aliongeza kuwa baadhi ya watumishi hao walioonekana kughushi vyeti ili kujipatia ajira Serikalini wamekimbia vituo vyao vya kazi.
Bw. Mchau aliwaasa wananchi kuepuka mchezo wa kughushi vyeti ili kujipatia ajira Serikalini.
“Ni kosa la jinai kughushi vyeti kwa lengo la kujipatia kazi hivyo endapo utagundulika umeghushi vyeti utachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria za nchi.”  Bw. Mchau alifafanua.
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma inaendelea na zoezi la uhakiki wa vyeti kwa Watumishi wote wa Umma nchini na matarajio ni kuwahakiki watumishi wote.



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) (kushoto), akipewa ufafanuzi kuhusu madai ya malimbikizo ya mishahara ya watumishi wa Umma (arrears) kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu-UTUMISHI Bw. Leonard Mchau. Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu-UTUMISHI Bw. Emmanuel Mlay.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) (kushoto), akitoa maelekezo kwa Watumishi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu-UTUMISHI. 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) (kushoto), akipewa ufafanuzi kuhusu fomu za madai ya malimbikizo ya mishahara ya watumishi wa Umma (arrears) .

Thursday, December 17, 2015

SERIKALI YAWASHUKURU WATAALAM WA KUJITOLEA KUTOKA JAPAN WALIOMALIZA MUDA WAO WA KUTOA HUDUMA NCHINI

Mtaalam wa Kujitolea kutoka nchini Japani Bw. Shinji Miwa (kushoto) akielezea namna alivyofanya kazi katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya ,wakati wa hafla ya kuwaaga wataalam wa kujitolea kutoka nchini Japan waliomaliza muda wao iliyofanyika ukumbi wa Utumishi.

Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Tixon Nzunda (kushoto) akizingumza na wataalam wa kujitolea kutoka nchini Japan waliomaliza muda wao katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Utumishi.

Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Tixon Nzunda (kushoto) akikabidhi zawadi kwa Mtaalam wa kujitolea kutoka nchini Japan Bi. Yuko Inoue aliyemaliza muda wake wa kutoa huduma nchini  katika hafla ya kuwaaga wataalam hao iliyofanyika ukumbi wa Utumishi. 
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Tixon Nzunda (kushoto) akikabidhi zawadi kwa Mtaalam wa kujitolea kutoka nchini Japan Bw. Shinji Miwa aliyemaliza muda wake wa kutoa huduma nchini  katika hafla ya kuwaaga wataalam hao iliyofanyika ukumbi wa Utumishi.  
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Tixon Nzunda (wa nne kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wataalam wa Kujitolea kutoka nchini Japan waliomaliza muda wao wa kutoa huduma nchini baada ya hafla ya kuwaaga iliyofanyika Utumishi. 

Wednesday, December 16, 2015

AZIRI WA UTUMISHI NA UTAWALA BORA MHE. KAIRUKI AENDELEA KUTEMBELEA IDARA/VITENGO - kukaa na Watumishi katika ofisi zao kuwasikiliza

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Anjella Kairuki (Mb), akitoa maelekezo kwa Watumishi wa Idara ya Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais-UTUMISHI mapema leo.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Anjella Kairuki ( Mb), kushoto, akimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bw. Mathias B. Kabunduguru. Waziri Mhe. Kairuki anatembelea kila Idara na Kitengo katika ofisi yake kubaini changamoto mbalimbali na namna ya kuzitatua.

Baadhi ya Wafanyakazi wa Idara ya Uendelezaji Sera wakiwa katika kikao kazi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Anjella Kairuki (Mb).


Tuesday, December 15, 2015

MHE. KAIRUKI AWAHIMIZA WATUMISHI WA IDARA YA UTAWALA WA UTUMISHI SERIKALINI KUWAJIBIKA IPASAVYO

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) (kushoto) akizungumza na watumishi wa Idara ya Utawala wa Utumishi Serikalini (DE) kuhimiza uwajibikaji wakati wa kikao kazi kati yake na Idara hiyo kilichofanyika ukumbi mdogo wa mikutano wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI alasiri leo. 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi Serikalini (DE) Bw. Nyakimura Muhoji wakati wa kikao kazi cha Mhe. Waziri na watumishi wa Idara hiyo kilichofanyika ukumbi mdogo wa mikutano wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI alasiri leo. 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) (kulia) akitoa maelekezo ya kiutendaji kwa Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi Serikalini (DE) Bw. Nyakimura Muhoji wakati wa kikao kazi cha Mhe. Waziri na watumishi wa Idara hiyo kilichofanyika ukumbi mdogo wa mikutano wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI alasiri leo. 

Monday, December 14, 2015

MHE. ANGELLA KAIRUKI AKABIDHIWA NYARAKA MUHIMU ZA KIUTUMISHI

Waziri wa  Nchi, Ofisi ya Rais – UTUMISHI na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) (kushoto) akikabidhiwa Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma (Standing Order) na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais- UTUMISHI na Utawala Bora Bw. HAB Mkwizu ofisini kwake. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – UTUMISHI na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) (kushoto) akipokea Sera ya Menejimenti na Ajira katika Utumishi wa Umma kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - UTUMISHI na Utawala Bora Bw. HAB Mkwizu ofisini kwake  
Waziri wa  Nchi, Ofisi ya Rais – UTUMISHI na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) (kushoto) akikabidhiwa Nyaraka za Maendeleo ya Utumishi na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais- UTUMISHI na Utawala Bora Bw. HAB Mkwizu ofisini kwake . 
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais- UTUMISHI na Utawala Bora Bw. HAB Mkwizu (kulia) akizungumza baada ya kumkabidhi nyaraka mbalimbali  Waziri wa  Nchi, Ofisi ya Rais – UTUMISHI na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb). 
Waziri wa  Nchi, Ofisi ya Rais –UTUMISHI  na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akiagana na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais- UTUMISHI na Utawala Bora Bw. HAB Mkwizu baada ya kukabidhiwa nyaraka mbalimbali za kiutumishi ofisini kwake. 

Saturday, December 12, 2015

MHE. KAIRUKI AANZA KAZI RASMI OFISI YA RAIS-UTUMISHI NA UTAWALA BORA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli  akimuapisha Ndg. Angellah Jasmine Kairuki kuwa Waziri wa Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ikulu jijini Dar es Salaam.



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Anjella Kairuki (Mb) (wa pili kutoka kushoto) akiwasili ofisini na kulakiwa na watendaji wa ofisi yake mara baada ya kuapishwa. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Bw. Tixon Nzunda.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Anjella Kairuki (Mb) akiweka saini katika kitabu cha wageni baada ya kuwasili rasmi katika ofisi yake.

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- Utumishi na Utawala Bora Bw. Tixon Nzunda (aliyesimama) akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Anjella Kairuki (wa kwanza kutoka kulia) kuongea na watendaji wa ofisi yake baada ya kuapishwa kushika wadhifa huo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Anjella Kairuki (Mb) (kulia) akizungumza na watendaji wa Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora mara baada kufika ofisini kwake kuanza kazi.

Tuesday, December 8, 2015

Taarifa kwa Vyombo vya Habari


Ofisi ya Rais-Utumishi yakanusha taarifa kuhusu Katibu Mkuu Utumishi kusimamishwa kazi na Mhe.Rais

Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma inakanusha habari iliyochapishwa na gazeti la Majira la tarehe 8 Desemba, 2015 yenye kichwa cha habari kinachomhusisha  Katibu Mkuu Utumishi kusimamishwa kazi na Mhe. Rais (Tazama nakala ya gazeti hilo hapa chini). Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu hahusiki na habari hiyo na anaendelea na kazi zake kama kawaida.