Wednesday, October 29, 2025

WATENDAJI WAKUU OFISI YA RAIS-UTUMISHI WAPIGA KURA, KATIBU MKUU MKOMI ATOA WITO KWA WATUMISHI WA UMMA NA WANANCHI KUJITOKEZA KUTIMIZA HAKI YAO YA KIKATIBA

 




WATENDAJI WAKUU OFISI YA RAIS-UTUMISHI WAPIGA KURA, KATIBU MKUU MKOMI ATOA WITO KWA WATUMISHI WA UMMA NA WANANCHI KUJITOKEZA KUTIMIZA HAKI YAO YA KIKATIBA

Na. Antonia Mbwambo na Veronica Mwafisi -Dodoma

Tarehe 29 Oktoba, 2025

Watendaji Wakuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora leo tarehe 29.10.2025 wameshiriki zoezi la kupiga kura katika Vituo mbalimbali na kuchagua Viongozi katika ngazi ya Rais, Wabunge na Madiwani.

Akishiriki zoezi hilo katika Kituo cha Kupiga Kura cha Msangalale Mashariki, Kata ya Dodoma Makulu, jijini Dodoma, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi ametoa wito kwa Watumishi wa Umma na Wananchi kujitokeza kuchagua viongozi wanaowahitaji kwa maendeleo ya Taifa.

“Namshukuru Mungu nimeshikiri salama zoezi hili muhimu la Kikatiba, nipende kutoa wito kwa Watumishi wa Umma na Wananchi kwa ujumla kushikiriki pia kwani ni haki yao ya msingi.” Bw. Mkomi amesisitiza.

Amesema hali katika Kituo hicho ni ya utulivu na wananchi wamekua wakimiminika kwenda kupiga kura hivyo amewasisitiza kila mwenye haki ya kushiriki zoezi hilo afanye hivyo.

Aidha, Bw. Mkomi amewapongeza Waratibu wa zoezi hilo katika Kituo hicho kwa kuonyesha ushirikiano kwa wananchi wanaoenda kushiriki katika zoezi hilo na kuhakikisha kila mwenye sifa anashiriki kikamilifu.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Bw. Xavier Daudi ameshiriki zoezi hili muhimu katika Kituo cha Mwatano, Kata ya Miyuji, Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi akiweka fomu ya kupiga Kura katika sanduku la Kura mara baada ya kushiriki zoezi hilo la Uchaguzi Mkuu wa Viongozi katika ngazi ya Rais, Wabunge na Madiwani leo tarehe 29 Oktoba, 2025 katika Kata ya Dodoma Makulu, Mtaa wa Msangalale jijini Dodoma.


Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi akiweka fomu ya kupiga Kura katika sanduku la Kura mara baada ya kushiriki zoezi hilo la Uchaguzi Mkuu wa Viongozi katika ngazi ya Rais, Wabunge na Madiwani leo tarehe 29 Oktoba, 2025 katika Kata ya Miyuji, Mtaa wa Mwatano jijini Dodoma.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi (aliyesimama) akipokea fomu ya kushiriki kupiga Kura kutoka kwa Wasimamizi wa Uchaguzi katika zoezi la Uchaguzi Mkuu wa Viongozi katika ngazi ya Rais, Wabunge na Madiwani leo tarehe 29 Oktoba, 2025 katika Kata ya Dodoma Makulu, Mtaa wa Msangalale jijini Dodoma.


Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi (aliyesimama) akisubiri kupatiwa fomu ya kushiriki kupiga Kura kutoka kwa Wasimamizi wa Uchaguzi katika zoezi la Uchaguzi Mkuu wa Viongozi katika ngazi ya Rais, Wabunge na Madiwani leo tarehe 29 Oktoba, 2025 katika Kata ya Miyuji, Mtaa wa Mwatano jijini Dodoma.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi akionesha jina lake katika orodha ya wapiga Kura iliyobandikwa katika kituo hicho kabla ya kushiriki kupiga kura katika zoezi la Uchaguzi Mkuu wa Viongozi katika ngazi ya Rais, Wabunge na Madiwani leo tarehe 29 Oktoba, 2025 katika Kata ya Dodoma Makulu, Mtaa wa Msangalale jijini Dodoma.


Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi akishiriki kupiga Kura katika zoezi la Uchaguzi Mkuu wa Viongozi katika ngazi ya Rais, Wabunge na Madiwani leo tarehe 29 Oktoba, 2025 katika Kata ya Miyuji, Mtaa wa Mwatano jijini Dodoma.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi akionesha kadi yake ya kupiga Kura kabla ya kushiriki zoezi la Uchaguzi Mkuu wa Viongozi katika ngazi ya Rais, Wabunge na Madiwani leo tarehe 29 Oktoba, 2025 katika Kata ya Dodoma Makulu, Mtaa wa Msangalale jijini Dodoma.


Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi akihakiki jina na picha yake kwenye daftari la kudumu kabla ya kushiriki zoezi la kupiga Kura katika Uchaguzi Mkuu wa Viongozi katika ngazi ya Rais, Wabunge na Madiwani leo tarehe 29 Oktoba, 2025 katika Kata ya Miyuji, Mtaa wa Mwatano jijini Dodoma.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi akipakwa wino mara baada ya kushiriki kupiga Kura katika zoezi la Uchaguzi Mkuu wa Viongozi kwenye ngazi ya Rais, Wabunge na Madiwani leo tarehe 29 Oktoba, 2025 katika Kata ya Dodoma Makulu, Mtaa wa Msangalale jijini Dodoma.


Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi (wa kwanza kushoto) akipokea fomu ya kushiriki kupiga Kura kutoka kwa Wasimamizi wa Uchaguzi katika zoezi la Uchaguzi Mkuu wa Viongozi katika ngazi ya Rais, Wabunge na Madiwani leo tarehe 29 Oktoba, 2025 katika Kata ya Miyuji, Mtaa wa Mwatano jijini Dodoma.


Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi akionesha kidole kilichopakwa wino mara baada ya kushiriki kupiga Kura katika zoezi la Uchaguzi Mkuu wa Viongozi kwenye ngazi ya Rais, Wabunge na Madiwani leo tarehe 29 Oktoba, 2025 katika Kata ya Miyuji, Mtaa wa Mwatano jijini Dodoma.

 



Monday, October 27, 2025

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAWAPONGEZA WASTAAFU WA OFISI HIYO KWA KULITUMIKIA TAIFA KIKAMILIFU

Na. Veronica Mwafisi-Dodoma

Tarehe 28 Oktoba, 2025

Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imewapongeza Watumishi wa Ofisi hiyo waliofikia ukomo katika Utumishi wa Umma kutokana na utumishi uliotukuka kwa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi ambao umechangia kutolewa kwa huduma bora katika Idara walizokuwa wakifanyia kazi.

Akitoa pongezi hizo kwa niaba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, leo tarehe 27 Oktoba, 2025, Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, SACP. Ibrahim Mahumi amesema kufikisha umri wa miaka 60 sio mchezo, ni jambo la kumshukuru Mungu.

 “Hongereni sana, mmeondoka katika Utumishi wa Umma mkiwa na sifa nzuri katika kulitumikia taifa na mkiwa na afya njema ni mfano mzuri wa kuigwa na tunaoendelea kufanya kazi,” amesema SACP. Mahumi.

SACP. Mahumi amemshukuru Katibu Mkuu-UTUMISHI kupitia Idara ya Utawala kwa kuanzisha utamaduni wa kukutana kila Jumatatu na kuwa na ubunifu mbalimbali wa kuwaweka watumishi pamoja kwa lengo la kuboresha utendaji.

“Tangu jambo hili la kukutana pamoja kila siku ya Jumatatu kupata elimu ya kuboresha utendaji kumekuwa na mabadiliko makubwa ya kiutendaji, nawasihi tuendelee kuyatumia mafunzo haya kuboresha utendaji zaidi.” Amesisitiza.

Akitoa neno la shukrani, Mtumishi Mstaafu wa Ofisi hiyo, Bw. Jerome Nchimbi amesema, ndani ya miaka 8 aliyofanya kazi katika ofisi hiyo amejfunza masuala mengi ya Kiutumishi pamoja na kufundishwa upendo, ushirikiano na kuwajali watu.

Kwa upande wake, Mstaafu mwingine, Bi. Godliver Byemerwa ametoa wito kwa Watumishi wa ofisi hiyo kuendelea kuwahudumia Wananchi kwa moyo wa upendo na ufanisi mkubwa kwa kuwa ofisi hiyo ni kioo cha jamii.

Aidha, Ofisi hiyo imewapongeza Watumishi waliozaliwa mwezi Oktoba na kuwatakia heri katika maisha yao ya Utumishi wa Umma ili kuwatumikia wananchi pamoja na kuongeza tija katika utendajikazi.

Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, SACP. Ibrahim Mahumi (wakwanza kulia) akitoa nasaha kwa niaba ya Katibu Mkuu-UTUMISHI kwa Watumishi wa ofisi hiyo waliostaafu na Watumishi wanaoadhimisha Siku ya Kuzaliwa katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma


Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma wa ofisi hiyo, SACP. Ibrahim Mahumi (hayupo pichani) wakati akitoa nasaha kwa niaba ya Katibu Mkuu-UTUMISHI kwa watumishi wa ofisi hiyo waliostaafu na Watumishi wanaoadhimisha Siku ya Kuzaliwa katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma. 


Sehemu ya Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakiwasikiliza Watumishi wastaafu Bw. Jerome Nchimbi na Bi. Godliver Byemerwa (hawapo pichani) wa ofisi hiyo walipokuwa wakitoa shukrani kwa Viongozi na Watumishi mara baada ya kufikia ukomo katika Utumishi wa Umma. 


Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakifurahia jambo wakati Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma wa ofisi hiyo, SACP. Ibrahim Mahumi (hayupo pichani) alipokuwa akitoa nasaha kwa niaba ya Katibu Mkuu-UTUMISHI kwa Watumishi wa ofisi hiyo waliostaafu na Watumishi wanaoadhimisha Siku ya Kuzaliwa katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma. 

Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, waliostaafu na Watumishi wanaoadhimisha Siku ya Kuzaliwa wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, SACP. Ibrahim Mahumi (hayupo pichani) alipokuwa akitoa nasaha kwa niaba ya Katibu Mkuu-UTUMISHI kwa Watumishi hao katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma. 

Sehemu ya Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma wa ofisi hiyo, SACP. Ibrahim Mahumi (hayupo pichani) wakati akitoa nasaha kwa niaba ya Katibu Mkuu-UTUMISHI kwa watumishi wa ofisi hiyo waliostaafu na Watumishi wanaoadhimisha Siku ya Kuzaliwa katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

Sehemu ya Wakurugenzi na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, wa ofisi hiyo, SACP. Ibrahim Mahumi (hayupo pichani) wakati akitoa nasaha kwa niaba ya Katibu Mkuu-UTUMISHI kwa watumishi wa ofisi hiyo waliostaafu na Watumishi wanaoadhimisha Siku ya Kuzaliwa katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

Mtumishi Mstaafu wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Jerome Nchimbi akitoa neno la shukrani kwa Wakurugenzi na Watumishi wa ofisi hiyo baada ya kuhitimisha Utumishi wake wa Umma.

Sehemu ya Wakurugenzi na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, SACP. Ibrahim Mahumi (hayupo pichani) wakati akitoa nasaha kwa niaba ya Katibu Mkuu-UTUMISHI kwa watumishi wa ofisi hiyo waliostaafu na Watumishi wanaoadhimisha Siku ya Kuzaliwa katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma wa ofisi hiyo, SACP. Ibrahim Mahumi (hayupo pichani) wakati akitoa nasaha kwa niaba ya Katibu Mkuu-UTUMISHI kwa watumishi wa ofisi hiyo waliostaafu na Watumishi wanaoadhimisha Siku ya Kuzaliwa katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma. 

Mtumishi Mstaafu wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Godliver Byemerwa akitoa neno la shukrani kwa Wakurugenzi na Watumishi wa ofisi hiyo baada ya kuhitimisha Utumishi wake wa Umma.

Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma wa ofisi hiyo, SACP. Ibrahim Mahumi (hayupo pichani) wakati akitoa nasaha kwa niaba ya Katibu Mkuu-UTUMISHI kwa watumishi wa ofisi hiyo waliostaafu na Watumishi wanaoadhimisha Siku ya Kuzaliwa katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma. 


TUENDELEE KUITUNZA, KUIDUMISHA NA KUILINDA AMANI KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU

 


Monday, October 20, 2025

WATUMISHI WA OFISI YA RAIS – UTUMISHI WAPATIWA MAFUNZO JUU YA MABADILIKO YA MTAZAMO KWENYE ENEO LA KAZI.

 Na Eric Amani, Mtumba Dodoma,

Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi amesema Serikali inaendelea kuweka mkazo katika kujenga utamaduni wa kazi unaozingatia maadili, ubunifu, na mabadiliko ya fikra miongoni mwa watumishi wa umma.

“Mabadiliko ya kweli katika utumishi wa umma yanaanza kwenye fikra na mitazamo ya mtumishi mmoja mmoja. Tunapaswa kubadilika ili tuwe chachu ya mageuzi katika utoaji wa huduma kwa wananchi,” alisema Bw. Daudi.

Leo Oktoba 20, 2025 Watumishi wa Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wamepatiwa mafunzo maalum yanayolenga kubadilisha mitazamo na mienendo yao katika mazingira ya kazi ili kuongeza ufanisi na ubora wa huduma kwa umma.

Mafunzo hayo ambayo hutolewa kila jumatatu yalihusisha mada mbalimbali zikiwemo mbinu za kujitambua, umuhimu wa kuwa na mtazamo chanya, ushirikiano kazini, na namna ya kujenga nidhamu na uwajibikaji katika kutekeleza majukumu ya kila siku ikiwa kwa lengo la kuwajengea uwezo watumishi hao ili kuboresha Utendaji kazi.

Aidha Bw. Daudi amewasisitiza watumishi wa umma kushiriki kikamilifu kwa wale wote ambao waliojiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura kwa ajili ya zoezi la Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025 kwaajili ya kuchagua viongozi sahihi kuanzia ngazi ya Rais, Ubunge na Udiwani.

Kwa upande mwezeshaji, Mosses Raymond, wakati akiwasilisha mada mbalimbali amesema mafunzo hayo yanalenga kuwasaidia watumishi wa umma kuelewa umuhimu wa kujiwekea malengo binafsi na kushirikiana kwa karibu zaidi na wenzao ili kuboresha utendaji wa taasisi.








Monday, October 13, 2025

WITO WATOLEWA KWA WATUMISHI WA UMMA KUBADILIKA KIMTAZAMO KATIKA UTENDAJI ILI KUFIKIA MALENGO YA DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050

 Na Antonia Mbwambo- Dodoma.

Tarehe 13/10/2025

Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Bw. Xavier Daudi ametoa wito kwa Watumishi wa Umma nchini kubadilika kimtazamo katika utendaji ili kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ikiwemo matumizi sahihi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

 Bw. Daudi ametoa wito huo leo tarehe 13/10/2025 alipokuwa akizungumza na watumishi wa Ofisi hiyo eneo maalum linalotumika kutoa mafunzo katika Ofisi hiyo Mtumba jijini Dodoma, yanayofanyika kila siku ya Jumatatu kwa lengo la kuwajengea uwezo watumishi hao ili kuboresha Utendaji kazi.

 

Kaimu Katibu Mkuu Bw. Daudi amesema, Watumishi wa Umma kubadilika kimtazamo katika utendaji ni jambo muhimu kwani kunakuwa na ufanisi wa wa kazi unaowezesha kuwa na Taifa jumuishi lenye ustawi, haki na linalojitegemea.

 

“Ninatoa wito kwenu, msitekeleze majukumu yenu kwa mazoea, kupitia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, mbadilike kiutendaji ili kuendana na mabadiliko yakiwemo ya kidijiti kwa kuleta ubunifu na mawazo chanya yatakayoiwezesha serikali kufikia malengo yake ya kutoa huduma bora kwa wananchi kupitia matumizi sahihi ya mifumo ya TEHAMA,” Bw. Daudi alisema. 

 

Kwa upande wake Meneja Mawasiliano Serikalini kutoka Tume ya Taifa ya Mipango (NPC), Bw. Titus Kaguo wakati akiwasilisha mada kwa watumishi hao kuhusu Malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, amesema mabadiliko makubwa ya Sayansi na Teknolojia ni kichocheo kikubwa cha maendeleo katika Taifa letu ambapo Dira hii imelenga kuwa kufikia mwaka 2050, asilimia 70 ya Watanzania watakuwa wanatumia mifumo ya TEHAMA na asilimia 80 ya  huduma mbalimbali za kiserikali zitakuwa zikitolewa kidiji ili kuleta Ufanisi katika Utendaji.


Wakurugenzi wa Idara na vitengo mbalimbali kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa na mwezeshaji ambaye ni Meneja Mawasiliano Serikalini kutoka Tume ya Taifa ya Mipango (NPC), Bw. Titus Kaguo (hayupo pichani) leo tarehe13/10/2025 katika mafunzo ambayo hutolewa kila siku ya jumatatu kwenye Ofisi hiyo iliyopo Mtumba jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi (aliyesimama mbele) akizungumza na watumishi wa Ofisi hiyo baada ya wasilisho la mada ya Malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 lililotolewa leo tarehe13/10/2025 na Meneja Mawasiliano Serikalini kutoka Tume ya Taifa ya Mipango (NPC), Bw. Titus Kaguo katika mafunzo ya kuwajengea watumishi wa Ofisi hiyo uwezo wa kiutendaji, ambayo hutolewa kila siku ya jumatatu kwenye Ofisi hiyo iliyopo Mtumba jijini Dodoma.

Meneja Mawasiliano Serikalini kutoka Tume ya Taifa ya Mipango (NPC), Bw. Titus Kaguo (aliyesimama mbele) akiwasilisha mada ya Malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 katika mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI,yaliyofanyika leo tarehe 13/10/2025 katika Ofisi hiyo iliyopo Mtumba jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi (wa kwanza kushoto aliyevaa miwani) akifurahia jambo alipokuwa akifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa katika mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji watumishi wa Ofisi hiyo ambayo hufanyika kila siku ya jumatatu katika Ofisi hiyo Mtumba Dodoma.


Watumishi kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI, wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa na mwezeshaji ambaye ni Meneja Mawasiliano Serikalini kutoka Tume ya Taifa ya Mipango (NPC), Bw. Titus Kaguo (hayupo pichani) kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji watumishi wa Ofisi hiyo ambayo hufanyika kila siku ya jumatatu katika Ofisi hiyo Mtumba Dodoma.


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Xavier Daudi akiteta jambo na Mkurugenzi wa Mipango wa Ofisi hiyo Bw. Cosmas Ngangaji wakati wa mafunzo ya kuwajengea watumishi wa Ofisi hiyo uwezo wa kiutendaji yaliyofanyika katika eneo la Ofisi hiyo lililopo Mtumba jijini Dodoma.

Baadhi ya Wakurugenzi wa Idara na vitengo pamoja na watumishi kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa na mwezeshaji ambaye ni Meneja Mawasiliano Serikalini kutoka Tume ya Taifa ya Mipango (NPC), Bw. Titus Kaguo (hayupo pichani) leo tarehe13/10/2025 katika mafunzo ambayo hutolewa kila siku ya jumatatu kwenye Ofisi hiyo iliyopo Mtumba jijini Dodoma.

Meneja Mawasiliano Serikalini kutoka Tume ya Taifa ya Mipango (NPC), Bw. Titus Kaguo (aliyesimama mbele, mwenye miwani) akitoa ufafanuzi na majibu ya maswali yaliyokuwa yakiulizwa na watumishi baada ya kuhitimisha wasilisho la mada ya Malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 lililotolewa katika eneo la Ofisi ya Rais-UTUMISHI leo tarehe 13/10/2025 jijini Dodoma.