Na. Veronica Mwafisi-Dodoma
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi amewasisitiza watumishi wa ofisi hiyo kutekeleza majukumu yao kwa weledi na ufanisi ili kuchochea maendeleo katika kuwahudumia wananchi.
Bw. Daudi ameyasema hayo leo wakati wa kikao kazi kilicholenga kumchagua mfanyakazi hodari wa mwaka 2025 wa ofisi hiyo kilichofanyika Mtumba jijini Dodoma.
Bw. Daudi amewataka watumishi wa ofisi hiyo kutoa huduma bora kwa kuzingatia Taratibu, Kanuni na Sheria za Utumishi wa Umma ili kujenga imani kwa Watumishi wa Umma na Wananchi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa azma ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya utoaji wa huduma bora kwa umma.
“Ushirikiano ni moja ya nguzo muhimu za ofisi yetu,
hivyo endeleeni kushirikiana katika kutekeleza majukumu ya kila siku, mfanyakazi
hodari aliyepatikana anatokana na ushirikiano mzuri alioupata kutoka kwa
watumishi wenzake wa ofisi hiyo”alisisitiza Bw. Daudi.
Bw. Daudi ameongeza kuwa, watumishi wote wa Ofisi hiyo ni wafanyakazi hodari
ingawa mshindi ni lazima apatikane hivyo, amewataka watumishi wote kutokata
tamaa kwani kila mmoja anawajibika ipasavyo katika kutekeleza majukumu ya ofisi
hiyo.
Kikao kazi hicho kimemchagua Bw. Charles Shija kuwa mfanyakazi
hodari wa ofisi hiyo kwa mwaka 2025, mshindi wa pili ni Bw. Erick Andrea na washindi
wa nafasi ya tatu ni watumishi wawili ambao ni Bw. Jumbe Mgoha na Bw. Waziri Mkumbo.
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier
Daudi akizungumza baada ya kufanyika uchaguzi wa
mfanyakazi hodari wa mwaka 2025 wa ofisi hiyo uliofanyika katika Mji
wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Sehemu ya Wakurugenzi na Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu
wa
ofisi hiyo Bw. Xavier Daudi (hayupo
pichani) alipokuwa akitoa pongezi kwa mfanyakazi
hodari wa mwaka 2025 wa ofisi hiyo wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Afisa Utumishi Mkuu,
Bw. Elibariki Funga akitaja vigezo vya kumpata mfanyakazi hodari wakati wa kikao kazi cha
kumchagua mfanyakazi hodari wa mwaka 2025 wa ofisi hiyo uliofanyika katika Mji
wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Maafisa wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI (walioshika maboksi) wakikusanya karatasi za kura mara baada ya Wakurugenzi na Watumishi wa ofisi hiyo kupiga kura katika kikao kazi cha kumchagua mfanyakazi hodari wa mwaka 2025 uliofanyika katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Maafisa wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI (walioshika boksi) wakihesabu karatasi za kura mara baada ya Wakurugenzi na Watumishi wa ofisi hiyo kupiga kura katika kikao kazi cha kumchagua mfanyakazi hodari wa mwaka 2025 uliofanyika katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.
Mtumishi hodari wa mwaka
2025 wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw.
Charles Shija (wa kwanza kulia aliyekaa) akifuatilia uhesabuji wa kura wakati
wa kikao kazi cha kumchagua mfanyakazi hodari kilichofanyika katika eneo la
ofisi hiyo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.






No comments:
Post a Comment