WANAMICHEZO UTUMISHI WAPEWA HAMASA KUELEKEKEA MASHINDANO YA MEI MOSI SINGIDA
“Ninaamini wote tuna afya njema na
tuko tayari kupambana na kuendelea kulinda taswira njema ya ofisi yetu, kwa
hiyo twendeni tukashiriki mashindano hayo tukiwa na umoja na ari kubwa, tukilenga
kurudi na vikombe vingi zaidi ya mwaka 2024”
Wito huo umetolewa na Kaimu
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya
Utumishi wa
Umma na Utawala Bora Bw. Xavier Daudi
wakati wa kikao kifupi kilichofanyika katika jengo la ofisi za Utumishi, Mtumba
jijini Dodoma kwa lengo la
kuwaaga Viongozi
na Wanamichezo
wa ofisi yake wanaokwenda Mkoani Singida
kushiriki Mashindano ya Michezo ya Siku ya Wafanyakazi Duniani.
Bw. Daudi aliwasisitiza viongozi
na wanamchezo hao kushiriki michezo
yote kikamilifu na kuzingatia sheria na kanuni za
michezo zilizoandaliwa ili
kupata
ubingwa na vikombe
vingi
zaidi kuliko kipindi kilichopita.
Aidha, aliwataka watumishi hao kuwa na nidhamu
na kuzingatia maadili ya utumishi
wa umma kwa kuwa wamebeba sura chanya ya ofisi ambayo ndiyo yenye dhamana ya kusimamia maadili ndani
ya Utumishi wa Umma.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Uendelezaji Taasisi na Mlezi
wa Wanamichezo hao Bw. Nolasco Kipanda alisema kuwa mwaka
2024 wakati wa mashindano ya
SHIMIWI Ofisi ilishinda Makombe Matatu (3) ikiwa ni pamoja na kombe
la mpira wa miguu, hivyo amewahimiza
wanamichezo hao kuongeza jitihada zaidi ili kuleta heshima kubwa hata katika
mashindano ya Mei Mosi.
Bw. Kipanda kwa niaba ya Wanamichezo hao amewashukuru na
kuwapongeza Viongozi na Timu ya Menejimenti kwa upendo
na ushirikiano wanaoonesha katika
michezo hadi kupata mafaniko ya
kushinda makombe katika mashindano mbalimbali.
Naye, Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Maadili Bi.
Leila Mavika amewataka wanamichezo hao kuwa na
maadili mema wakati wote na kuepuka
unywaji wa pombe kupita kiasi na kukosa staha.
“Nawakumbusha kutunza mbinu na taarifa nyingine za
kambi na kuheshimu sheria, kanuni na miongozo inayoongoza Utumishi wa Umma na
michezo ambayo tunaenda kishiriki”
alisisitiza Bi. Mavika
Awali, Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa
Rasilimaliwatu Bw. Musa Magufuli amesema jumla ya Watumishi 57 wameruhisiwa
kwenda Mkoani Singida kwa ajili ya kushiriki mashindano ya siku ya Wafanyakazi
Duniani na Ofisi itashiriki michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mpira wa
miguu, mpira wa pete, karata, riadha na bao ambayo inatarajiwa kuanza Aprili
15, 2025.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, UTUMISHI na Utawala Bora Bw. Xavier Daudi akizungumza na Viongozi na Wanamichezo wa ofisi yake wanaokwenda Mkoani Singida kushiriki Mashindano ya Michezo ya Siku ya Wafanyakazi Duniani wakati wa kikao kifupi cha kuwaaga kilichofanyika katika jengo la ofisi za Utumishi, Mtumba jijini Dodoma
Timu ya Wanawake ya Mpira wa Pete na Kikapu ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ikiwa katika picha ya pamoja baada ya kuagwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Xavier Daudi (Hayupo pichani) ili kushiriki Mashindano ya Michezo ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yanayofanyika Mkoani Singida.
No comments:
Post a Comment