Na Veronica Mwafisi-Dodoma
Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imeipongeza Sekretarieti ya Ajira
katika Utumishi wa Umma kwa
kuzingatia maoni na ushauri unaotolewa
na kamati hiyo ili kuhakikisha mchakato wa ajira unafanyika kwa ufanisi mkubwa na uwazi wa hali ya juu.
Mwenyekiti
wa Kamati hiyo, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama ametoa pongezi hizo leo jijini Dodoma
kwa niaba ya Kamati yake wakati wa ziara
ya kikazi ya Kamati hiyo iliyolenga kutembelea na kujifunza utendajikazi wa
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
Mhe. Dkt.
Mhagama ametolea mfano maoni ambayo Kamati yake iliyatoa kuhusu usaili
kufanyika katika ngazi za mikoa badala ya kuwalazimu waombaji kazi wote kufika
jijini Dodoma kumeleta matokeo
chanya kwa waombaji kazi hao.
Vilevile Dkt. Mhagama amezungumzia matumizi
ya mfumo wa Ajira Portal kwa waombaji kazi kuondokana na dhana tofauti ya upendeleo
wa kupata ajira katika Utumishi wa Umma.
“Mfumo wa Ajira Portal umeondoa dhana ya kuwepo kwa upendeleo kwa waombaji kazi, ninaamini wengi wamepata
ajira serikalini pasipo kupitia kwa mtu yeyote.” amesema Mhe. Dkt.
Mhagama.
Kwa
Upande wake Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu ameishukuru Kamati hiyo kwa kutoa maoni na ushauri mara
zote ambao kwa kiasi kikubwa umesaidia kutekeleza majukumu ya Sekretarieti ya
Ajira katika Utumishi wa Umma kikamilifu.
Aidha, Naibu Waziri Sangu amewaomba Wajumbe wa Kamati hiyo kuendelea kuwa Mabalozi wazuri wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma ili kuwahakikishia wananchi kuhusu uwazi wa namna ajira katika Utumishi wa Umma zinavyopatikana kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu
zilizowekwa
na Sekretarieti hiyo wakati wa kuomba kazi.
Akielezea mafanikio baada ya kutumia mfumo wa Ajira Portal, Kaimu
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Mhandisi Samweli Tanguye
amesema, kupitia mifumo wameweza kuajiri Rasilimaliwatu yenye uwezo wa kufanya
kazi na kutoa matokeo chanya pamoja na kuondoa hoja za kuajiri kwa dhana ya upendeleo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe.
Dkt. Kizito Mhagama (katikati) akizungumza
na Viongozi na Watendaji wa
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma wakati wa ziara ya Kamati hiyo iliyolenga kutembelea
na kujifunza kuhusu utendajikazi wa ofisi hiyo jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Kizito Mhagama (watatu
kutoka kulia) akifuatilia wasilisho kuhusu
mchakato wa usaili wa ajira unavyofanyika wakati wa ziara ya kamati hiyo
iliyofanyika jijini Dodoma. Kushoto kwake ni Naibu Waziri, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu na wa kwanza kulia ni Kaimu
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Nolasco Kipanda.
Naibu Waziri,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu akitoa neno la utangulizi kabla ya
kumkaribisha Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Utawala, Katiba na Sheria, Mhe.
Dkt. Kizito Mhagama (hayupo pichani) wakati wa ziara ya Kamati yake iliyofanyika
katika ofisi za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma jijini Dodoma.
Sehemu ya Wajumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Utawala, Katiba na Sheria wakifuatilia wasilisho kuhusu
mchakato wa ajira unavyofanyika wakati wa ziara ya kamati hiyo katika Ofisi ya
Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma iliyofanyika jijini Dodoma.
Wakurugenzi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Viongozi na Watendaji wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Kizito Mhagama (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara ya kamati yake katika ofisi hiyo iliyofanyika jijini Dodoma.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Utawala, Katiba na Sheria Mhe. Omar Kombo
akiwasilisha hoja wakati wa ziara ya Kamati hiyo katika ofisi ya Sekretarieti
ya Ajira katika Utumishi wa Umma iliyolenga kutembelea na kujifunza kuhusu utendajikazi wa ofisi hiyo
jijini Dodoma.
Kaimu Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi
wa Umma, Mhandisi Samweli Tanguye akiwasilisha mada kuhusu TEHAMA ilivyoboresha
mchakato wa ajira wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu
ya Utawala, Katiba na Sheria iliyolenga kutembelea na kujifunza kuhusu utendajikazi wa ofisi hiyo
jijini Dodoma.
Kaimu Naibu Katibu, Menejimenti ya Ajira, Bi. Somwana Manjenga
akiwasilisha mada kwa Wajumbe wa Kamati
ya Kudumu ya Utawala, Katiba na Sheria kuhusu mchakato wa ajira wakati wa ziara
ya kikazi ya Kamati hiyo iliyolenga kutembelea na kujifunza kuhusu
utendajikazi wa ofisi hiyo jijini Dodoma.
Sehemu
ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Utawala, Katiba na Sheria wakifuatilia
wasilisho kuhusu mchakato wa ajira
unavyofanyika wakati wa ziara ya kamati hiyo katika Ofisi ya Sekretarieti ya
Ajira Katika Utumishi wa Umma iliyofanyika jijini Dodoma.
Sehemu ya Maafisa kutoka Sekretarieti ya Ajira katika
Utumishi wa Umma wakisikiliza maoni ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Utawala, Katiba
na Sheria wakati wa ziara ya kikazi ya Kamati hiyo iliyolenga kutembelea na kujifunza kuhusu
utendajikazi wa ofisi hiyo jijini Dodoma.




No comments:
Post a Comment